image

Kazi za vitamini B na vyakula vya vitamini B

Makala hii inakwenda kukuletea kazi za vitamini B, pia tutajwenda kuona makundi ya vitamini B na kazi za kila kundi. Pia makala hii inakwenda kukufundisha vyanzo na vyakula vya vitamini B. Utajifunza pia kazi kuu za vitamini B kwa ujumla wake.

KAZI ZA VITAMINI B NA MAKUNDI YAKE

Vitamini B ni moja kati ya vitamini ambavyo vinahitajika sana mwilini. Athari yeyote ya upungufu wa vitamini hivi inaweza kuonekana moja kwa moja kwenye miili yetu. vitamini B vimegawanyika katika makundi mengi sana ikiwemo B1, B2, B3, B5, B6, B7, B9 na B12. je ungependa kujuwa kazi za vitamini hivi kulingana na aina zake. Endelea na makala hii upate kujifunza kazi za vitamini B.

 

 

Kazi za vitamini B kulingana na kila kundi la vitamini B

 

 

Basi tambuwa kuwa kazi za vitamini B ni kuhakikishha kuwa mipambano ya kikemikali inafanyika ndani ya seli. Sasa hapa tutaona kazi za vitamini hivi kulingana na makundi yake:-

 

 

B1 hii husaidia mfumo wa fahamu (mfumo wa neva) kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi B1 huweza kuleta maatizo kwenye mfumo wa fahamu, moyo na mupotea kwa misuli.

 

 

 

 

B2 huhitajika kwa ajili ya uzalishwaji wa nishati, lipi, vitamini, madini na husaidia katika utengenezwaji wa antioxidant. Upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha kuvimba (imflamation) kwenye ngozi, ulimi, midomo, na matatizo kwenye mfumo wa fahamu.

 

 

 

 

B3 hii huhitajika katika kufanyika mchakato wa metabolism kwenye seli. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea ngozi kuwa na matatizo kama miwasho, mapele, ukurutu na kadhalika. Pia upungufu wa vitamini hivi huweza kusababisha tumbo kuvurugika na kuleta misongo ya mawazo

 

 

 

 

B6 hii hufanya kazi ya kuhakikisha metabolisma inayohusima katika kuchakata hamirojo asidi za amino, kuchakata hemoglobin hizi ni chembechembe za kwenye seli nyekundu za damu zinazo saidia katika kusafirisha hewa mwilini, pia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea madhara kwenye ubongo, shida kwenye fahamu ya mtu na pia ugonjwa wa anemia unaonasibiana na upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini.

 

 

 

 

B9 huhusika katika kuchakata DNA, kuchakata amino acid, katika kukua na kukomaa kwa seli mwilini hasa hasa seli hai nyekundu. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea matatizo katika ukuaji, utengenezwaji na ukomaaji wa seli hai nyekundu za damu, uchovu, maumivu ya kichwa, kutokea uvimbe kwenye mdomo na hata kuathiri mtoto aliyepo tumboni.

 

 

 

 

B12 huhitajika kwa ajili ya utengenezwaji wa seli mpya, utengenezwaji wa damu na pia kwa ajili ya mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema. Upungufu wa vitamini hivi huweza kupelekea kuvurugika kwa tumbo, shida kwenye mfumo wa fahamu pamoja na matatizo kwenye ulimi.

 

 

Kazi za vitamini B kwa ujumla

Kwa ujumla vitamini B vina kazi nyingi kama ulivyojifunza hapo juu. Kazi hizi tunaweza pia kuziweka katika ufupisho ufuatao. Lengo la kufupisha ni kukuwezesha msomaji kukumbuka kwa wepesi kazi za vitamini B. Kazi hizo ni kama zifuatazo:-

 

1. Husaidia mfumo wa fahamu kufanya kazi vyema
2. Huhitajika kwa ajili ya uzalishaji wa nishati (nguvu) mwilini
3. Husaidia katika utengenezwaji wa seli mwilini
4. Husauidia katika utengenezwaji wa hemoglobin hizi ni chembechembe katika seli nyekundu za damu
5. Husaidia katika kuchakata DNA
6. Husaidia katika utengenezwaji wa seli mpya na kukomaa kwa seli

 

 

VYAKULA VYA VITAMINI B.

 

Kwa kuwa umesha jifunza kazi za vitamini B kulingana na makundi yake. Je ungependa kujuwa ni wapi unaweza kupata vitamini B? Sehemu hii utajifunza vyakula ambavyo husaidi kutupatia vitamini B. Vyakula hivyo ni kama:-

1. Nyama
2. Mapalachichi
3. Mboga za majani
4. Mimea jamii ya karanga
5. Alizeti
6. Mayai
7. Pilipili
8. Ndizi
9. Viazi
10. Maharagwe na kunde
11. Nafaka kama mchele, mtama na mahindi



           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2021-06-05     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1019


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Naomba mnielekeze jinsi ya matayarisho ya Mbegu za papai mpaka nianze kuzitumia kama tiba
Mbegu za papai ni katika baadhi ya mbegu ambazo hutumika kama dawa, na tunda lake ni katika matunda yenyevirutubisho vingi sana. Mbegu za papai zinatumka kwa matumizi mengi sana kiafya. Je ungependa kujuwa faida za papai na jinsi ya kuandaa mbegu zake kam Soma Zaidi...

Faida za kula chungwa na chenza (tangarine)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula chungwa na chenza (tangarine) Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Zabibu
Soma Zaidi...

Umuhimu wa kutumia maembe kiafya.
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kutumia maembe kiafya, tunajua wazi kuwa maembe ni tunda ambalo lina umuhimu kwenye afya na uwa na vitamini C kwa hiyo tunapaswa kujua faida zake kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

Faida za kula parachichi
Somo hili litakwenda kukueleza na kukuelimisha kuhusu umuhimu wa kula parachichi kiafya Soma Zaidi...

Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini
hapa Tutakwenda kuona Vyakula Vya vitamini B, kazi za Vitamini B na dalili za Upungufu wa Vitamini B mwilini Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula ukwaju
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula ukwaju Soma Zaidi...

Nini maana ya protini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu maana ya protini Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Bamia
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula kisamvu
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kisamvu Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula karanga
Somo hili linakwenda kukuletea faida za kiafya za kula karanga Soma Zaidi...

Upungufu wa vitamini C na dalili zake mwilini
makala Soma Zaidi...