JAVASCRIPT - somo la 4: Jinsi ya kuandika variable kwenye javascript

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika variable. Hapa utajifunza sheria zinazohusu variable katika javascript

 

JINSI YA KUWEKA VARIABLE KWENYE JAVASCRIPT.

Katika somo hili tutakwenda kujifunza jinsi ya kutengeneza variable kwenye javascript na kuweza kuzitumia. Pia tutaona kanuni zinazoambatana na variable kwenye javascript.

 

Je variable ni nini?

Variable ni kama chombo kinachohifadhia taarifa. Chukulia mfano una ndoo ambayo ndani yake ina maji, mikate, na mchele. Hapa ndoo ni variable ambayo inahifadhi. Ama mfano kusema x inawakilisha 8. hapa x ni variable ambayo inahifadhi 8.

 

Variable hutambulika kwa jina lake ambalo halitakiwi lijirudie tena kuwakilisha variable nyingine. Jina hili ni unique ambalo hutambulika kama identifier.  Variable inatakiwa iwe na zifa zifuatazo:-

  1. Jina hili linaweza kuwa na herufi, namba, underscore (_) na alama ya dola ($)
  2. jina lazima lianze na herufi au alama ya dola ($) au underscore (_)
  3. jina linatakiwa lizingatiwe matumizi ya herufi kubwa na ndogo. kwani katika javascript juma na JUMA ni majina mawili tofauti.
  4. majina yote ambayo ni javascript keyword hayaruhusiwi kwenye variable. Tumezungumzia kuhusu keyword kwenye somo lililotangulia.

 

Namna ya kuipa thamani javascript

Tunatumia alama ya = ili kuipa thamani variable. Kwenye javascript alama hii huitwa assignment operator na sio alama ya sawasawa kama ilivyo kwenye hesabu.

 

Kuna njia kuu tatu ambazo hutumika kwenye javascript ili kuipa variable thamani yake. Njia hizo ni kwa kutumia keyword kama:-

  1. var
  2. let
  3. const

 

1. Kwa kutumia var:

Hii hutumika pale unapotaka kuweka variable ambayo itaweza kutumiaka kwenye ukurasa mzima wenye block code nyingi yaani globally. Block code tulisha izungumzia katika masomo yaliyopita.

 

Mfano 1:

<script>

   var bc = "www.bongoclass.com";

   document.write(bc)

</script>

 

Hii itakupa matokeao haya:

Mfano 2

<script>

   var x = 2;

   var X = 3;

   document.write(x + X)

</script>

Hii itakupa matokeo haya

2. Kwa kutumia let

Let hutumika kuipa thamani variable ambayo itatumika kwenye block code moja tu yaani locally.

Mfano 3

<script>

   let web = "www.bongoclass.com";

   document.write(web)

</script>

 

H">...

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: JavaScript Main: ICT File: Download PDF Views 653

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 web hosting    👉4 Dua za Mitume na Manabii    👉5 kitabu cha Simulizi    👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana:

Game 1: Jinsi ya kutengeneza game ya tic toc ya wachezaji wawili kwa kutumia html, css na javascript

Katika post hii utakwenda kujifundisha jinsi ya kutengeneza game ya tic toc ya wachezaji wawii kwa utumia html, css na javascript

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 22: Jinsi ya ku set time na tarehe

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu ku set time. Yaani tutaweka muda ambao code zinatakiwa ndio zilete matokeo.

Soma Zaidi...
Game 2: Jinsi ya kutengeneza tic toc game ya single player kwa kutumia javascript, html na css

Katika post hii utakwenda kujifunza kutengeneza game ya tic toc ya mchezaji mmoja na kompyuta yaani single player

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 2: Jisi ya ku print output ya code za javascript.

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza ku display matokeo ya code za javascript.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 7: Jinsi ya kutumia logical operator kwenye javascript

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia logical operator kwenye javascript. Katika somo hili tutakwenda kutumia mahesabu.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 10: Jinsi ya kuandika object na matumizi yake kwenye javascript

Ksomo hili litakwenda kukufundisha kuhusu object kwenye javascript, kazi zake na sheria zake katika kuiandika.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT -somo la 1: Kwa nini ni muhimu kujifunza javascript

Katika somo hili utajifunza kuhusu historia ya javacsript pamoja na kazi za javascript. Pia utayajuwa makampuni makubwa yanayotumia javascript.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 5: Jinsi ya kupangilia maandishi wakati wa ku output kwenye javascript

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa maandishi (text) wakati wa ku out put matokeo ya code

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 9: Jinsi ya kuandika function kwenye javascript

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 16: Jinsi ya kutumia html form kwenye javascript

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku dili na html form kwenye javascript. Javascript inaweza kufanya mengi kwenye html form.

Soma Zaidi...