Katika somo hili utajifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa maandishi (text) wakati wa ku out put matokeo ya code
JINSI YA KUPANGILIA MAANDISHI WAKATI WA KU OUT PUT JAVASCRIPT
Katika somo lililotangulia tulikutana na shida moja kuwa maandishi yametoka yakiwa yamebanana banana. Sasa katika somo hili tutajifunza namna ya kupangilia muonekano wa maandishi.
Njia zinazotumika kupangilia muonekano wa maandishi:
Kwa kutumia html tag
Kwa kutumia html tag unaweza kupangilia muonekano wa text zako kwa namna utakayo. Angalia mfamo hapo chini:-
Mfano 1
<script>
document.write('<p style="color:blueviolet">Haloo bongoclass</p>');
</script>
Hii itakupa matokeo haya
Unaweza kufanya mengi kwa kutumia html ili kupangilia muonekano wa maandishi kwenye javascript. Lakini hebu tuangalie namna ambavyo mfano unaofuata utakavyotupa changamoto iliyojitokeza katika somo lililopita:-
Mfano 2:
<script>
let a = 'mama anapika', b = 'ugalina dagaa';
document.write(a, b);
</script>
code hizi zitakupa matokeo haya:-
Hapo utaona kuna changamoto kuwa variable ya kwanza na ya pili zimebanana. Hivyo unaweza kutengenisha nafasi hizi kwa kutumia html tag. Tunaweza kutatuwa changamoto hiyo kwa kutumia html tag <br> ila kwa kuwa hii ni string utahitajika kuiweka ndani ya zile alama za kufunga na kufunguwasemi yaani ‘<be>’
Mfano 3
<script>
let a = 'mama anapika', b = 'ugalina dagaa';
document.write(a, '<br>', b);
</script>
Hii itakupa matokeo haya
...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu array pamoja na method zinazohusiana na array. Pia nitakujuza tena kuhusu array ni nini. Utajifunza pia jinsi ya kutengeneza array.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function maaumu zinazotumika kwenye string yaani string method.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ambavyo utaweza kutumia javascript kutengeneza kikokotoo cha hesabu yaani calculator
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza khusu while loop na do while loop.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutumia forOfLoop. Hii ni aina ya loop ambayo yenyewe inahusisha item zote kwenye array.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz kuhusu baadhi ya function ambazo hutumika kwenye namba
Soma Zaidi...Kwa kutumia mfano huu na iliyotangulia unaweza kuweka masharti kadiri uwezavyo. Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu switch statement.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu matendo ya hesabu ambayo ni kugawanya, kujumlisha, kuzidisha na kutoa
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia logical operator kwenye javascript. Katika somo hili tutakwenda kutumia mahesabu.
Soma Zaidi...