Ksomo hili litakwenda kukufundisha kuhusu object kwenye javascript, kazi zake na sheria zake katika kuiandika.
Katika post hii tutajifunza kuhusu javascript object. Utajifunza jinsi ya kutengeneza javascript object. Pia tutajifunza kuhusu kutimia method kwenye javascript.
Object ni nini?
Object ni data ambayo ina sifa na tabia (property). Mfano unaposema gari linakuwa na sifa kama rangi, mwendo kasi, aina ya injini. Hivyo kwa mfano huu gari ni object ambayo inaweza kuandikwa kama hivi:

Ukiangalia code hizo utagundua kuwa:-
OBJECT ni variable kama unavyoona hapo bar gari, ambapo OBJECT yetu ni gari ambayo ni variable
OBJECT ina jina la OBJECT na thamani ama sifa zake kwa mfano hapo jina ni gari na sifa zake ni mwendo, injini, manufacture, jina la gari.
Jina la OBJECT linaitwa object name, na hizo sifa huitwa object property au behaviour na hizo thamani kwa mfano Toyota, dizel, 180kh/h hizo zote huitwa property values.
Kutoka property moja kwenda nyingine hutenganishwa na alama ya koma (,).
Property na value yake kutenganishwa na alama ya nukta pacha (:)
Jinsi ya kuandika OBJECT katika javascript.
Utaweka jina la object. Jina hili halitakiwibkuanza na namba ama special character wala javascript keywords
Kisha utaweka jina la object likifuatiwa na mabano {}
Ndani ya mabano ndio utaweka hizo property zake.
Kuandika property ataandika. Jina la hiyo property ikifuatiwa na alama ya nukta pacha kisha itafuatiwa na value. Kama ni string utaweka ndani ya alama za "".
Mfano:

Katika mfano huo hapo utagundua kuwa object inaweza kuwa na array ndani yake kwa mfano hapo juu property mafunzo value zake zipo kwenye array.
Si hivyo tu bali object pia inaweza kuwa na function kama tutakavyoona katika mifano inayokuja.
Jinsi ya ku access object
Ku access object ni sawa na kuitumia hiyo objectvkwenye code zako. Kwa nfano katika mifano miwili iliyotangulia baada ya kuandika object tuliweza kuzitumia na ku out put code ndipo tukapata matokeo ya hizo code.
Kuna njia kuu tatu ambazo hutumika ku access object. Yaani njia tatu ambazo hutumika ili uweze kuitumia object kwenye code zako. Njia hizo ni: -
Kwa kutumia doti. Kama tulivyoona katika mfano wa kwanza gari.jina
Njia ya pili ni kwa kutumia mabango kama ilivyo katika mfano wa pili tovuti[jina]
Njia ya tatu ni kwa kutumia this keyword kama tutakavyojifunza.
KWA KUTUMIA DOTI
ili uweze ku access object kwa kutumia doti kwanza utaandika jina la hiyo Object kisha itafuatiwa na kidoti kisha ndipo itafanya jina la property.
Mfano:

2.KWA KUTUMIA MABANO []
Kutumia njia hii kwanza utaweka jina ka object kisha litafuatiea na mabano, ndani ya mabano utaweka jina la hiyo property. Zingatia kama ni string kuiweka ndani ya alama za ""
Mfano:

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowJe umeipenda post hii ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku dili na html form kwenye javascript. Javascript inaweza kufanya mengi kwenye html form.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunz kuhusu baadhi ya function ambazo hutumika kwenye namba
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu condition statemant. Darasa hili ni moja katika madarasa muhimu programming. Katika somo hili tutajifunza kwa vitendo zaidi. Tutatumia mifano ya somo lililo tangulia.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu historia ya javacsript pamoja na kazi za javascript. Pia utayajuwa makampuni makubwa yanayotumia javascript.
Soma Zaidi...Katika post hii utakwenda kujifunza kutengeneza game ya tic toc ya mchezaji mmoja na kompyuta yaani single player
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria ama syntax za kuandika javascript. Hii itakuwezesha kuelwa zaidi code za javascript.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu user input. Somo hili litaangalia html form na attribute zake na jinsi zinavyohusiana na user input. Mwisho wa somo hili utaweza kutengeneza simple Calculator kwa kutumia javascript.
Soma Zaidi...Hii ni game ambayo utafikiria namba, ambayo inatakiwa iwe sawa na namba ambayo game imeiweka.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia logical operator kwenye javascript. Katika somo hili tutakwenda kutumia mahesabu.
Soma Zaidi...