JAVASCRIPT - somo la 12: Function zinazotumika kwenye namba

Katika somo hili utajifunz kuhusu baadhi ya function ambazo hutumika kwenye namba

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu method ambazo hutumika kwenye namba na mahesabu yaani Math property na Number property. Kama ambavyo somo lililotangulia ulijifunza method zinazofanya kazi kwenye string.

isInteger()

Hii hutumika katika kuthibitisha kama hiyo taarifa ni namba ama sio namba. Kama itakuwa ni namba itakupa jibu true na kama sio namba itakupa jibu la false

Utaona hapo variable a ni namba hivyo imekuja true na hiyo variable b imeleta false kwa kuwa sio namba.

isNaN()

Hii hutumika huthibitisha kuwa hiyo taarifa ilioingizwa sio namba. Huleta majibu ya true kama sio namba na false kama ni namba.

parseInt()

Hii hutumika kuchukuwa namba kutoka kwenye data iliyoingizwa. Kwa mfano unahitaji mtu aingize mwaka wake wa kuzaliwa kwenye program ambayo inauliza umri. Sasa unakuta ameandika hivi 26 ndio miaka yangu wakati alichotakiwa kuandika ni 26 tu. Hivyo Method hii itanyakuwa hiyo 26 na kuacha hizo zisizo husika.

Medhod hii itachukuwa namba yeyote itakayokuwa mwanza. Kwa mfano ameandika 4 miezi na miaka 26 hapa itakayichukuliwa ni hiyo 4 hivyo program itatambuwa kuwa ana miaka 4.

Pia endapo ataandika hivi miaka 26 program haitatambuwa kitu. Kwa kuwa yenyewe inachukuwa character ya kwanza hivyo itakupa jibu NaN Angalia mfano hapo chini nimekuekea mitindo yotebhiyo.

parse    Float()

Hii hutumika kuchukuwa namba zenye viwango vya desimali kutoka kwenye string. Inafanana na hiyo ya hapo juu parseInt kuwa huchukuwa character ya kwanza, na huketa NaN kama imeanza na hefuri.

toFixed()

Hii hutumika katika kukadiria viwango maalumu kwenye desimali. Kwa mfano namba hii 2.63698 tunataka kuiandika kwenye viwango viwili vya desimali hivyo itakuwa 2.64 utaona hapo imekuwa 4 baada ya kuikadiria na endapo tutaiandika kwenye kiwango kimoja itakuwa 2.6 kufanya hivi utatumia toFixed()

toExponential()

Hii hutumika kubadili namba iliyo katika viwango vya desimali kwa katika exponent. Hivyo kuiandika namba ki sayansi zaidi.

toString()

Hii hutumika katika kubadili namba kuwa string. Kwa mfano ukiweka namba hii 24 program itatambuwa hii namba kama string hivyo itaichakata hii namba kama "24" kisha kuirudisha matokeo yake kama 24 ila utofauti ni kuwa hatambuliki tena kuwa ni namba ila ni string .

ceil()

Hii hutumika katika kukadiria viwango vya desimali round up kwa maana kuwa bila kujali kwamba ni kubwa kuliko 5 yenyewe itaongeza moja kwenye namba husika.

Katika matumizi ya kawaida chukulia kuwa unakokotoa ni watu wangapi wanaweza kupita kwenye daraja husika kwa wakati mmoja. Sasa unapata jibu kuwa ni watu 2.3 kiuhalisia hapo inamaana watu 2 na kidogo. Sasa ni vyema kitaalamu useme ni watu watatu ndio wanapita hapo.  Hivyo tunapuuzia desimali zilizopo na kuweka 3. Ina maana kuwa hatuna shaka kabisa kuwa watu watatu watapita.

floor()

Hii hutumika kukadiria namba kwa kupuuza viwango vyote vya desimali vilivyopo na kulibakisha nmab yenyewe. Kwa mfano 6.9 hii itasomeka 6 bila kujali viwango vya desimali. Hii ndio kitaalamu huitwa roun down

Katika matumizi ya kawaida mfano unataka kulipa wafanyakazi lakini katika mahesabu yako mfanyakazi atatakiwa kulipwa Tsh 424900.28 hivyo hapa tutatumia floor na kuondoa hizo .28 na kwa mahesabu haya mfanyakazi atapokea 424900

round()

Hii sasa ndio ile namna ya kukasirika ambayo tuneizo">...

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: JavaScript Main: ICT File: Download PDF Views 395

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)

Post zinazofanana:

Game 3: Mchezo wa kufikiria namba kwa kutumia javascript

Hii ni game ambayo utafikiria namba, ambayo inatakiwa iwe sawa na namba ambayo game imeiweka.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 24: Jinsi ya kutengeneza online keyboard

Katika project hii utakwenda kufunza jinsi utakavyoweza kutengeneza keyboard ya online kwa kutumia javascript

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 9: Jinsi ya kuandika function kwenye javascript

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kuandika function kwenye javascript. Utajifunz apia namna ya kuitumia function hiyo

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 11: function maalumu zinazotumika kwenye string yaani string method

Katika somo hili utakwenda kujifunza baadhi ya function maaumu zinazotumika kwenye string yaani string method.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 21: Jinsi ya kutumia while loop na do while loop

Katika somo hili tutakwenda kujifunza khusu while loop na do while loop.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 5: Jinsi ya kupangilia maandishi wakati wa ku output kwenye javascript

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kupangilia muonekano wa maandishi (text) wakati wa ku out put matokeo ya code

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 18: Jinsi ya kutumia switch case kwenye javascript

Kwa kutumia mfano huu na iliyotangulia unaweza kuweka masharti kadiri uwezavyo. Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu switch statement.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 4: Jinsi ya kuandika variable kwenye javascript

Katika somo hili utajifunza jinsi ya kuandika variable. Hapa utajifunza sheria zinazohusu variable katika javascript

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 16: Jinsi ya kutumia html form kwenye javascript

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya ku dili na html form kwenye javascript. Javascript inaweza kufanya mengi kwenye html form.

Soma Zaidi...
JAVASCRIPT - somo la 13: Function zinazofanya kazi kwenye array.

Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu array pamoja na method zinazohusiana na array. Pia nitakujuza tena kuhusu array ni nini. Utajifunza pia jinsi ya kutengeneza array.

Soma Zaidi...