Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu condition statemant. Darasa hili ni moja katika madarasa muhimu programming. Katika somo hili tutajifunza kwa vitendo zaidi. Tutatumia mifano ya somo lililo tangulia.
Ili uelewe vyema somo hili soma kwanza habari hii. Umetakiwa kusajili wanafunzi katika darasa la kwanza. Sharti mwanafunzi awe na umri kati ya miaka 6 hadi 8. Program itasema umefanikiwa kumsajili mwanafunzi Endapo mwanafunzi atakuwa na umri wa miaka chini ya 6 program inatakiwa iseme anatakiwa kurudi darasa la chekechea na endapo umri utakuwa zaidi ya miaka 8 basi program imwambie anatakiwa asome memkwa . Darasa letu litakuwa linachezea kwenye habari hiyo.
Condition statement ni nini?
Neno statement ni neno la kiingereza lenye maana maelezo na neno condition lina maana ya masharti. Hivyo kwa ujumla tunasema kuwa condition statement ni maelekezo ambayo yanakuwa na masharti. Maelekezo haya yanaweza kubeba pande mbili pande yabkwanza itabeba maelezo na pande ya lili itatupa matokeo.
Mfano: "endapo umri ea mtoto ni miaka 5". Haya ni maelekezo na matokeo yake anatakiwa kurudi darasa la chekechea. Hivyo shart hapa la kusajiliwa ni kuwa na umri kuanzia miaka 6.
Aina za condition statement:
Condition statement zipo katika aina kuu 3 ambazo ni:-
Katika somo hili tutaona aina kwanza. Kisha switch na loop tutaisoma kwenye somo linalofuata.
Tunataka tuanze kuona endapo umri wa mtoto utakuwa chinivya miaka 6.
Kwanza tutatiloa prompy() kwa ajili ya kudaka user input. Rejea somo la 15 tumezungumzia sana habari hii.
Pili tutatumia variable kwa ajili ya ku store user input kutoka kwenye prompt(). Variable yetu tutaiita umri. Hivyo code itasomeka hivi
let umri = prompt("Weka umri wa mtoto");
Tatu tutakwenda kutengeneza condition statement. Jinsfi ya kutengeneza condition statemen
Kwa mujibu wa mfano wetu, shart amavcondition ni kuwa na umri kuanzia miaka 6. Ikiwa ni chini ya hapo program itatoa maelekezo.
Kanuni ya kuandika if… else
if(weka sharti hapa){
weka maelekezo hapa
}
Kumbuka tayari tunayo vatiable yabkukusanya data ambazo zitajazwa. Variable hiyo ni umri rejea hapo juu.
Sasa tunakwenda kusema kwenye shart ikiwa umri ni chini ya miaka sita. Kama tulivyoona hapo juu kuwa shart huwekwa ndanibya mabano (). Kumbuka alama hizi ambazo tulishasomaga masomo ya mwanzoni: -
> Kubwa kuliko
< Ndogo kuliko
== Sawa sawa na
=> Kubwa kuliko au sawa sawa na
<= Ndogo kuliko au sawa sawa na
& and au na hutumika kuunganisha mfano Juma na Ali
! hii hutumika katika kukanusha
|| hii hutumika kumaanisha au
Hivyo itaandikwa hivi: -
if(umri ) sas kwa kuwa umri tunaujuwa nibchini yabmiaka 6 tutasema if(umri < 6) hapo sharti limekamilika.
Hatuwa inayofuata ni kuandika statement na kama nilivyotangulia kusema kuwa statement huandikwa ndani ya {} hivyo itakuwa hivi
if(umri <6){"Anatakiwa kurudi darasa la chekechea"} sasa kumbuka ili statement yetu ionekane tunatakiwa tutumie zile njia za ku onyesha matokeobya code kama document.write(). Hivyo code zetu zitasomeka hivi: -
if(umri <6){
document.write("Anatakiwa kurudi darasabla chekechea");}
Pia unaweza kitia rangi maandishi kwa kitumia html. Kwa mfano hapo tutatumia <b style='color:blue'> Anatakiwa arudi darasa la chekechea</b>
Hivyo code nzima zitakuwa hivi: -
<html>
<head>
<title>Mafunzo ya javascript</title>
</head>
<body>
<script>
let umri = prompt("Weka umri wa mtoto");
if(umri < 6){
document.write("<b style='color:blue'> Anatakiwa arudi darasa la chekechea</b>");
}
</script>
</body>
</html>
Sasa hapo utaona nimeweka namba 4 ambayo ni ndogo kuliko 6. Ukibonyeza ok utapata majibu haya.
Kwa mfano huo huo sasa utaona kama utajaza umri kuanzia 6 na kuendelea haitaonyesha chochote. Sasa itatakiwa tuseme else yaani ukiwa umri ni zaidi ya mika 6 ama zsidi program iseme umefanikiwa kumsajili mwanagunzi.
Kufanya hivi tutaongeza neno&">...
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwenda kujifunza sheria ama syntax za kuandika javascript. Hii itakuwezesha kuelwa zaidi code za javascript.
Soma Zaidi...Kwa kutumia mfano huu na iliyotangulia unaweza kuweka masharti kadiri uwezavyo. Tukutane somo linalofuata tutajifunza kuhusu switch statement.
Soma Zaidi...Ksomo hili litakwenda kukufundisha kuhusu object kwenye javascript, kazi zake na sheria zake katika kuiandika.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu aina za data ambazo hutumika kwenye javascript
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu array pamoja na method zinazohusiana na array. Pia nitakujuza tena kuhusu array ni nini. Utajifunza pia jinsi ya kutengeneza array.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu user input. Somo hili litaangalia html form na attribute zake na jinsi zinavyohusiana na user input. Mwisho wa somo hili utaweza kutengeneza simple Calculator kwa kutumia javascript.
Soma Zaidi...Katika project hii utakwenda kufunza jinsi utakavyoweza kutengeneza keyboard ya online kwa kutumia javascript
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwenda kujifunza kuhusu ku set time. Yaani tutaweka muda ambao code zinatakiwa ndio zilete matokeo.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutumia forOfLoop. Hii ni aina ya loop ambayo yenyewe inahusisha item zote kwenye array.
Soma Zaidi...Katika somo hili utajifunza kuhusu matendo ya hesabu ambayo ni kugawanya, kujumlisha, kuzidisha na kutoa
Soma Zaidi...