picha

FLUTTER somo la 20: Jinsi ya ku sign App ya android kwenye flutter

Somo hili litakufundisha hatuwa kwa hatuwa jinsi ya ku sign app ya android kwenye flutter

Kabla ya ku sign App kwanza tutahitajika kutengeneza faili la keystone. Hii ni kwa ajili ya App za android tu na sio ios. Hivyo basi tutafufuata hatuwa kwa hatu.

 

Mambo ya kuzingatia:

Kabla ya kuanza kutengeneza keystone kwanza tunatakiwa tuhakikisha kuwa flutter path ipo kwenye environment variable.kama bado rejea video yetu hii jinsi ya ku add flutter 

 

Pia hakikisha umesha add java path kwenye environment variable. Utafanya kama ulivyofanya wakati wa ku add flutter kwenye environment variable.

 

Ili kucheki kama vyote hivyp vipo, start button ya window tafuta program inaitwa cmd. Hapo ni uwanja wa kuandika commamd. Andika flutter doctor hii command itakuletea maelezo kuhusu flutter. Kama hutopata maelezo hayo huwenda huja add enviromnent vyema.

 

Ili kuakikisha kama java ipo tayari kwa matumizi andika command hii java -version utaona itakuletea maelekezo kuhusu toleo a java unalotumia na maelekezo mengineyo. Kama haitakuwepo badi unaweza ku download jdk kwenye tovuti ya oracle.

 

Jinsi ya kutegeneza keystore file

Kwa watumiaji wa windo, ingia kwenye cmd kisha run command hii

keytool -genkey -v -keystore %userprofile%\upload-keystore.jks -storetype JKS -keyalg RSA -keysize 2048 -validity 10000 -alias upload

 

Command hii unakuwezesha kutengeneza faili hilo kwenye location ya user wa kompyuta. Yaani kwenye disk c -> user -> username

 

Kwa watumiaji wa macOS au linux tumia command hii

keytool -genkey -v -keystore ~/upload-keystore.jks -keyalg RSA \

        -keysize 2048 -validity 10000 -alias upload

 

Baada ya apo utafatamaelekezo. Kwanza utatakiwa kuweka password na kuzirudi, kisha utaandika jina lako, unapoishi, na nyinginezo. Cheki picha hapo chini, baada ya kujaza swali bofya enter 

 

Haya ni maswali utakayoulizwa na mfano wa majibu yake

  1. Enter keystore password   mfano: bongoclass  angalau password ziwe character 8

  2. Re-enter password  mfano: bongoclass

  3. What is your first name and last name  Mfano: Bongo class

  4. What is the name of your organizational unit  mfano: bongo255

  5. What is the name of your organization mfano Bongoclass

  6. What is the name of your city or locality mfano: Tanga

  7. What is the name of your state or province  mfano: Pangani

  8. What is the two-letter country code for this unit  mfano : 255

  9. Mwisho utaulizwa kama taarifa ni sahihi. Taandika yes.

 

 

Baada ya kubofya hapo utatakiwa kutengeneza key password. Kumbuka zile za kwanza ulizoweka zinaitwa keystore password. Hivyo basi hapa utaweka password nyingine ambazo zinaitwa keypassword angalau password ziwe character 8



Mpaka kufikia hapo tumeshatengeneza keystone file angaliakwenye profile user wa kompyuta yako utalikuta. Jina linaitwa upload-keystore.jks

Sasa tutaliamisha faili letu na kuliweka sehemu rahisi kulifikia kwenye app yetu.nakwenda kuliweka kwenye flolder la app. Ila usifanye hivi kwa app ambayo sio ya mafunz...

Ingia sasa ili uweze kusoma makala hii yote.

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-07-15 23:27:03 Topic: Flutter Main: Masomo File: Download PDF Views 1345

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 web hosting     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    

Post zinazofanana:

Flutter somo la 17: Jinsi ya kubadili app icon

Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili app icon kwenye app ya Android na iphone kwenye flutter.

Soma Zaidi...
Flutter somo la 11: Matumizi ya text widget

Katika Flutter, Text Widget ni kipengele kinachotumiwa kuonyesha maandishi kwenye programu. Kwa kawaida, hutumiwa kama sehemu ya muundo wa UI ya programu za Flutter.

Soma Zaidi...
Flutter somo la 16: Jinsi ya kuweka drawer menu

Katika somo hili utakwenda kujifunza jisni ya kuweka drawer menu kwenye app ya flutter.

Soma Zaidi...
FLUTTER somo la 19: jinsi ya kubadili app id ama bundle identifier na configuration nyingine

Katika somo hili utajifunza jisni ya kubadili package name ama app id kwenye Android app na Bundle Identifier kwenye iOS app na taarifa nyinginezo.

Soma Zaidi...
Flutter somo la 14: Jinsi ya kuweka picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu widget ya Image ambayo hutumika kuonyesha picha kwenye App.

Soma Zaidi...
FLUTTER somo la 21: Jinsi ya kutengeneza faili la apka na faili la aab

Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kutengeneza faili la apk kwa ajili ya ku share app yako, na faili la aab kwa ajili ya ku publih app yako.

Soma Zaidi...