Flutter somo la 14: Jinsi ya kuweka picha
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu widget ya Image ambayo hutumika kuonyesha picha kwenye App.
Kuna aina mbili za kuweka picha kwenye App ya flutter. Kwanza ni picha ya offline, picha hii unaiweka kwenye app yako kama mafaili mengineyo. Njia ya pili ni kuweka picha ambayo ipo online hivyo tunatumia link ya picha hiyo kwenye App yetu.
Property za Image:
1. image: (property hii ni lazima kuwepo) Inabainisha picha itakayotolewa. Unaweza kutumia aina ya ImageProvider kama vile AssetImage, NetworkImage, au FileImage kama chanzo cha picha.
2.width: Inabainisha upana wa picha. Unaweza kutoa thamani ya double kuweka upana wa picha kwa pikseli za mantiki.
3.height: Inabainisha urefu wa picha. Unaweza kutoa thamani ya double kuweka urefu wa picha kwa pikseli za mantiki.
4.fit: Inadhibiti jinsi picha itakavyoingizwa ndani ya nafasi yake. Thamani zinazowezekana ni:
5.BoxFit.contain: Inapanua picha ili kuingiliana na chombo huku ikidumisha uwiano wake wa asili.
BoxFit.cover: Inapanua picha ili kufunika kontena lote, ikikata ikiwa ni lazima.
BoxFit.fill: Inayeyusha picha ili kujaza kontena lote, ikivuruga uwiano wake wa asili.
BoxFit.fitWidth: Inapanua picha ili ifanane na upana wa kontena huku ikidumisha uwiano wake wa asili.
BoxFit.fitHeight: Inapanua picha ili ifanane na urefu wa kontena huku ikidumisha uwiano wake wa asili.
BoxFit.none: Haina mabadiliko yoyote kwenye ukubwa wa picha.
6.alignment: Inabainisha usawazishaji wa picha ndani ya nafasi yake. Thamani inapaswa kuwa ya aina ya Alignment na inaweka picha ndani ya chombo.
7.color: Inatumia kichujio cha rangi kwa picha.
8.colorBlendMode: Inabainisha jinsi rangi iliyowekwa na property ya color itakavyochanganywa na picha.
9.repeat: Inabainisha jinsi picha itakavyorudi ikiwa haijaijaza nafasi yake kikamilifu.
Jinsi ya kuweka Picha:
Sasa ili tuweke picha tutatumia ImageProvider ambazo nimezitaja kwenye property ya image. Ambazo ni asset na network
- Kwa kutumia AssetImage
Kwa kutumia jia hii utaweza kutumia faili ambalo utaliweka kwenye app yako. Hivyo kwanza utafuata njia hizi:-
- Kwanza ingia kwenye folder la project yako. Folda lenyewe ambalo kuna mafaili mengine kama pubspec.yaml
- Utatengeneza folda hapo lipe jina la assets. Unaweza kuweka jina lolote unalotaka. Ndani ya foler hili tengeneza folda linguine liite images pia unawez akuweka jina unalolitaka wewe. Sasa ndani ya folda la images hapo weka picha zako unazotaka zionekane.
- Hatuwa inayofuata nenda kwenye faili linaloitwa pubspec.yaml kisha tafuta mstari ulioandikwa flutter: na hakuna mwingine wenye jina hilo kuelekea chini. Maana mistari yenye flutter ipo mingi ila tafuta ambazo ni wa mwisho. Kisha weka code hizi
assets:
- assets/images/
Weka kama unavyoziona hapo kwa mtiririko huohuo. Code hizi zinasajili folda letu la assets ambalo lina folda la picha. Baada ya hapo sasa tutakuwa tayari kuweza kutumia picha yetu kwenye App.kuna worning unaweza kuziona kwenye faili la main.dart. Bofya hizo warning kupata maelekezo zaidi.
Sasa ili tuweze kutumia picha tutatumia widget ya picha ikifuatiwa na image provider. Mfano
Image.asset("images/bongo.png")
Code nzima hizi hapa
import 'package:flutter/material.dart';
void main() => runApp(MyApp());
class MyApp extends StatelessWidget {
@override
Widget build(BuildContext context) {
return MaterialApp(
home: Scaffold(
 ...
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Simulizi za Hadithi Audio 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 ai web app 👉5 web hosting 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Flutter: somo la 4: Jinsi ya kuandika code za App ya flutter, hatuwa kwa hatuwa
Katika somo hili utakwenda kujifunza sasa jinsi ya kuandika code za app yetu kwenye flutter framework.
Soma Zaidi...Flutter: Somo la 3: Mambo muhimu kuhusu App ya flutter
Katika somo hili tutakwend akuyaona baadhi ya maeneo muhimu ya kuanzia kuyajuwa kwa ajili ya course ya flutter kwneye android studio.
Soma Zaidi...Flutter somo la 11: Matumizi ya text widget
Katika Flutter, Text Widget ni kipengele kinachotumiwa kuonyesha maandishi kwenye programu. Kwa kawaida, hutumiwa kama sehemu ya muundo wa UI ya programu za Flutter.
Soma Zaidi...FLUTTER somo la 19: jinsi ya kubadili app id ama bundle identifier na configuration nyingine
Katika somo hili utajifunza jisni ya kubadili package name ama app id kwenye Android app na Bundle Identifier kwenye iOS app na taarifa nyinginezo.
Soma Zaidi...Flutter somo la 5: widget ni nini na zinafanya nini kwenye flutter
Katika somo hili uatwkeda kujifunza zaidi kuhusu widget, maana yake, aia zake na kazi zake kwneye flutter.
Soma Zaidi...Flutter somo la 17: Jinsi ya kubadili app icon
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili app icon kwenye app ya Android na iphone kwenye flutter.
Soma Zaidi...