Flutter somo la 6: Scaffold widget, kazi zake na property zake
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu scaffold widget. Hapa tutakwend kuona properties zake na baadhi ya mifano.
Katika muktadha wa maendeleo ya programu, hasa katika uga wa maendeleo ya programu za simu kwa kutumia fremu kama Flutter, Scaffold ni kipengele msingi kinachotumiwa kuunda muundo na mpangilio wa skrini au ukurasa wa programu.
Katika Flutter, kipengele cha Scaffold hutumika kama chombo cha kuhifadhi kwa vipengele vikuu vya skrini, kama vile app bars, drawers, bottom navigation bars, floating action buttons, na zaidi. Hutoa mfumo wa kuandaa vipengele hivi na kusimamia mwingiliano wao.
Baadhi ya properties za scaffold:
Hivi ni vipengele muhiu kwenye scaffold:
1. AppBar: AppBar kawaida huwekwa juu ya skrini na ina jina la skrini, pamoja na vitendo kama vile batani, ikoni, au menyu.
2. Body: Hii ni eneo kuu la maudhui ya skrini ambapo vitu kama vile maandishi, picha, orodha, au vipengele vingine vya UI vinawekwa. UI ni user interface yaani muonekan wa screen ambao mtumiaji atautumia.
3. FloatingActionButton: Kipengele hiki kinawakilisha batani zinazooelea juu ya maudhui kwenye body, mara nyingi hutumika kwa vitendo vikuu au vitendo vya kipaumbele.
4. Drawer: Paneli ambayo inaingia kutoka upande wa skrini, mara nyingi hutumiwa kwa urambazaji au chaguo zaidi kwenye menu.
5. BottomNavigationBar: Bar ambayo kawaida huwekwa chini ya skrini, inayotoa urambazaji kati ya skrini tofauti au sehemu za programu.
6. BottomSheet: ni kama ukurasa ambao unakunjuka kutoka chini ya skrini, mara nyingi hutumika kuonyesha habari au vitendo zaidi.
Kwa kutumia kipengele cha Scaffold, waendelezaji wanaweza haraka kuunda muundo wa msingi kwa skrini za programu yao na kuongeza kwa urahisi vipengele vya UI vya kawaida bila kulazimika kujenga upya. Hii inasaidia mchakato wa kuunda interfaces za watumiaji zilizo na muundo mzuri na unaofanana kote kwenye skrini tofauti za programu.
Mifano wa scafold:
Sasa ngoja tuone mifano ya scaffold na jinsi inavyowez akufanya kazi. Mifano hii itaangala hizo properties zilizotajwa hapo juu.
Mfano:1 scaffold:
Ili kuandika widget ya scaffold kumbuka kuwa yenyewe ni property ya home , na pia utambuwe kuwa home nayo ni materialApp ambayo ipo nda i ya function ya runApp. Hvyo basi code zetu znaweza kuwa hivi
import 'package:flutter/material.dart';
void main() {
runApp(
MaterialApp(
home: Scaffold(),
),
);
}
Hapo ukirun code hizo app yako itafungyka ikiwa haina kitu. Ni kwa kuwa hatujaweka bado propery yeyote ya scaffold.
Pia tunaweza kuogeza mbwembwe hapo kwenye home. Kwa mfano tunawez akuongeza background color sasa. Ilikuweka background color tutatumia property ya backgroundColor ambapo value yake itakuwa ni hiyo rangi tunayoitaka. Mfano kama tunataka kuweka rang ya kijani tutasema Colors.green.
backgroundColor: Colors.geen
import 'package:flutter/material.dart';
void main() {
runApp(
MaterialApp(
home: Scaffold(
backgroundColor: Colors.blue,
),
),
);
}
Ngoja tuongeze appbar
appBar: AppBar(
title: Text('Bongoclass'),
backgroundColor: Colors.black,
),
Hapo nimetumia propery ya title iki kuweka text za app bar. Pia nimetumia backgroundColor property kuweka rangi.
Body:
body: Text("Mafunzo ya flutter"),
Drawer
drawer: Drawer(backgroundColor: Colors.green,),
Batani:
floatingActionButton: FloatingActionButton(
onPressed: () {},
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Kitabu cha Afya 👉3 Bongolite - Game zone - Play free game 👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Flutter somo la 15: Jinsi ya kuweka icon kwenye App ya flutter
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia icon yaani kuweka icon kwenye App ya flutter.
Soma Zaidi...FLUTTER somo la 19: jinsi ya kubadili app id ama bundle identifier na configuration nyingine
Katika somo hili utajifunza jisni ya kubadili package name ama app id kwenye Android app na Bundle Identifier kwenye iOS app na taarifa nyinginezo.
Soma Zaidi...Flutter somo la 13: widget ya batani
Katika somo hili uatakwenda kujifunz ajinsi ya kutumia batani na kuweka maumbo mbalimbali ya batani.
Soma Zaidi...Flutter somo la 10: Jinsi ya kutumia widget ya container
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu widget ya container pia tutajifunza jinsi widget hii inavyoweza kutumika na widget nyingine.
Soma Zaidi...Flutter somo la 9: Jinsi ya kutumia widget ya Row
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu row widget. Hii ni widget ambayo ina utofauti na column widget kwa kuwa hii yenyewe inapangilia maudhui kwa safu za mlalo, tofauti na iliyopita inapangilia kwa safu za wima.
Soma Zaidi...Flutter somo la 17: Jinsi ya kubadili app icon
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili app icon kwenye app ya Android na iphone kwenye flutter.
Soma Zaidi...