FLUTTER somo la 2: Jinsi ya kutengeneza App ya flutter
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutengeneza App yako ya kwanza ya Flutter hatuwa kwa hatuwa.
Kama kilakitu kipo sawa kulingana na maelekezo ya somo la kwanza, funguwa android studio. Kisha utakuja ukurasa wenye batani 3 kubwa ambazo zina majina New Flutter Project, New Project, na Open. sasa hapo utabofya hiyo ya kwanza kushoto ya new flutter project. Angalia video hii kupata maelekezo yote
Kisha ukurasa mwingine utafunguka, huo utakuhitaji kuweka jina la project. Kwa mfano unaweza kuweka tehama kisha bofua neno Next kwa chini upande wa kulia.
Ukurasa unaofuata una vibox vingi vinavyohitaji kujazwa. Rejea video yatu kwa maelekezo zaidi. Sasa wacha tuone kila kijumba katika hivyo na kazi zake.
- Project name: katika kijumba hiki utaweka jina la App unayotaka kutengeneza weka tehama
- Project Location: katika kichumba hiki utaweka location mahala ambapo kwenye kompyuta yako hiyo project itakuwepo. Unaweza kuacha hivyo hivyo kama huelewi jinsi ya kuset location.
- Description: hapo utaweka maelezo kuhusu App yako. Mfano inahusu nini. Sio lazima kujaza kichumba hiki.
- Project type: hapo utaweka aina ya application yako. Unaweza kuacha hivyohivyo hapo
- Organization: hapo weka package name
- Android language: hapo utachaguwa lugha ya android. Unaweza kuacha kama palivyo.
- iOS Language: hapa napo utachaguwa ligha ya app ya ios pia unaweza kuacha kama palivyo
- Platform: hapo utachaguwa platform ambazo app yakoitafanya kazi. Chaguwa unazotaka, kwa mfano hapo chaguwa web na android kwa kuwa hutahitaji configuration nyingine.
- Module name: weka jina la mudulehapo unaweza kurudia jina la app yako kwa herufi ndogo
- Content root: hapo ni folder ambalo project yako itakuwepo. Wacha hivyo hivyo kama huelewi
- Module file location: mahala ambapo faili la module litakuwepo. Wacha hivyo hivyo kama huelewi
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Madrasa kiganjani 👉2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 web hosting 👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Post zinazofanana:
Flutter somo la 16: Jinsi ya kuweka drawer menu
Katika somo hili utakwenda kujifunza jisni ya kuweka drawer menu kwenye app ya flutter.
Soma Zaidi...Flutter somo la 15: Jinsi ya kuweka icon kwenye App ya flutter
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia icon yaani kuweka icon kwenye App ya flutter.
Soma Zaidi...Flutter somo la 9: Jinsi ya kutumia widget ya Row
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu row widget. Hii ni widget ambayo ina utofauti na column widget kwa kuwa hii yenyewe inapangilia maudhui kwa safu za mlalo, tofauti na iliyopita inapangilia kwa safu za wima.
Soma Zaidi...Flutter somo la 14: Jinsi ya kuweka picha
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu widget ya Image ambayo hutumika kuonyesha picha kwenye App.
Soma Zaidi...FLUTTER somo la 18: Jinsi yakubadili App name kwenye flutter
Katika somo hili utakwenda kujifunzajinsi ya kubadilisha, jinala App yaani App name.
Soma Zaidi...Flutter: Somo la 3: Mambo muhimu kuhusu App ya flutter
Katika somo hili tutakwend akuyaona baadhi ya maeneo muhimu ya kuanzia kuyajuwa kwa ajili ya course ya flutter kwneye android studio.
Soma Zaidi...