image

Flutter somo la 10: Jinsi ya kutumia widget ya container

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu widget ya container pia tutajifunza jinsi widget hii inavyoweza kutumika na widget nyingine.

Widget ya Container ni moja ya vipengele muhimu katika maendeleo ya programu za Flutter. Inatumika kufunga na kupanga vitu vingine kwenye skrini. Container inaruhusu udhibiti mkubwa wa muonekano wa vitu vinavyojumuishwa ndani yake.

 

Container yenyewe inapangilia maudhui kwenye kufungu katika ukubwa maalumu unaohitaji, ama position maalumu unapotaka kikae

 

Property muhimu za Container:

alignment: Inadhibiti jinsi watoto wa Container wanavyopangwa ndani yake. Kwa mfano, Alignment.topLeft, Alignment.center, nk.

 

  1. color: Rangi ya background ya Container.

 

  1. width: Upana wa Container.

 

  1. height: Urefu wa Container.

 

  1. margin: Inadhibiti nafasi kuzunguka Container.

 

  1. padding: Inadhibiti nafasi ndani ya Container.

 

  1. decoration: Inaruhusu kuongeza staili zaidi kwa Container, kama vile mstari wa mipaka, rangi ya mbele, na zaidi.

 

  1. child: Widget ambao utapangwa ndani ya Container. Hii ni lazima iwe mtoto mmoja tu, lakini unaweza kuweka widgets nyingi kwa kutumia Row, Column, au nyingine Container ndani ya Container.

 

import 'package:flutter/material.dart';

 

void main() {

 runApp(MyApp());

}

 

class MyApp extends StatelessWidget {

 @override

 Widget build(BuildContext context) {

   return MaterialApp(

     home: Scaffold(

       appBar: AppBar(

         title: Text('Tehama'),

         backgroundColor: Colors.blue,

       ),

       body: Center(

         child: Container(

           // Rangi ya background ya Container.

           color: Colors.yellow,

           // Upana wa Container.

           width: 200,

           // Urefu wa Container.

           height: 200,

           // Inadhibiti nafasi kuzunguka Container.

           margin: EdgeInsets.all(20),

           // Inadhibiti nafasi ndani ya Container.

           padding: EdgeInsets.all(10),

           // Widget ambao utapangwa ndani ya Container.

           child: const Center(

             child: Text(

               'Hii ni Container!',

               style: TextStyle(fontSize: 20),

             ),

           ),

         ),

       ),

     ),

   );

 }

}

 

Mambo ya kuzingatia:

Container haiscroll hivyo kama text zako ni nyingi na unahitaji ku scroll utahitajika kutumia widget nyingine.

 

 

Widgets zinazoweza kutumika kama watoto wa Container:

 

  1. Text: Kutumika kwa kuonyesha maandishi ndani ya Container.

 

  1. Image: Kutumika kwa kuonyesha picha ndani ya Container.

 

  1. Icon: Kutumika kwa kuonyesha ikoni ndani ya Container.

 

  1. Row: Kutumika kwa kusimamia vitu kwa mstari mmoja ndani ya Container.

 

  1. Column: Kutumika kwa kusimamia vitu kwa mstari mmoja wa wima ndani ya Container.

 

  1. Stack: Kutumika kwa kusimamia vitu vilivyopangwa kwa msingi wa kufunika ndani ya Container.

 

  1. ListView: Kutumika kwa kuonyesha orodha ya vitu katika Container kwa mwelekeo wa wima.

 

  1. GridView: Kutumika kwa kuonyesha orodha ya vitu katika Grid ndani ya Container.

 

  1. Custom widgets: Unaweza pia kutumia widgets zilizoundwa na wewe mwenyewe kama watoto wa Container.

 

Kwa kuchanganya propertyna watoto hawa wa Container, unaweza kuunda miundo mbalimbali na mitindo ya UI katika programu zako za Flutter.

 

 

Jinsi ambavyo container inaweza kutumika na widget nyingine:

import 'package:flutter/material.dart';

 

  1. Container na row

import 'package:flutter/material.dart';

 

void main() {

 runApp(MyApp());

}

 

class MyApp extends StatelessWidget {

 @override

 Widget build(BuildContext context) {

   return MaterialApp(

     home: Scaffold(

       appBar: AppBar(

         title: Text('Container with Row Example'),

         backgroundColor: Colors.blue,

       ),

       body: Center(

         child: Container(

           // Rangi ya background ya Container.

           color: Colors.yellow,

           // Upana wa Container.

           width: 300,

           // Urefu wa Container.

           height: 100,

           // Widget ambao utapangwa ndani ya Container.

           child: Row(

             mainAxisAlignment: MainAxisAlignment.center,

             children: <Widget>[

               Container(

                 color: Colors.red,

                 height: 100,

                 width: 100,

 

 

                 child: const Text(

                   'Text 1 ',

                   style: TextStyle(color: Colors.blue), // Rangi ya kwanza

                 ),

     ">...



Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Flutter Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 457


Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Flutter somo la 11: Matumizi ya text widget
Katika Flutter, Text Widget ni kipengele kinachotumiwa kuonyesha maandishi kwenye programu. Kwa kawaida, hutumiwa kama sehemu ya muundo wa UI ya programu za Flutter. Soma Zaidi...

FLUTTER somo la 18: Jinsi yakubadili App name kwenye flutter
Katika somo hili utakwenda kujifunzajinsi ya kubadilisha, jinala App yaani App name. Soma Zaidi...

FLUTTER somo la 19: jinsi ya kubadili app id ama bundle identifier na configuration nyingine
Katika somo hili utajifunza jisni ya kubadili package name ama app id kwenye Android app na Bundle Identifier kwenye iOS app na taarifa nyinginezo. Soma Zaidi...

Flutter somo la 17: Jinsi ya kubadili app icon
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili app icon kwenye app ya Android na iphone kwenye flutter. Soma Zaidi...

Flutter somo la 7: jinsi ya kutumia Widget ya AppBar
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu widget ya AppBar. Hata tutaona inavyofanya kazi na baadhi ya property zake. Soma Zaidi...

Flutter somo la 8: Jinsi ya kutumia widget ya column
Katika somo hili utakweda kujifunza kuhsu widget ya column. Widget hii ni moja katika widget zilizo muhimu sana kuzifaham. Soma Zaidi...

Flutter somo la 1: Nini flutter na nini hasa inafanya
Katika somo hili utajifunza historia fupi ya flutter, kazi zake, nini hasa inafanya. pia utajifunza jinsi ya ku install flutter Soma Zaidi...

FLUTTER somo la 21: Jinsi ya kutengeneza faili la apka na faili la aab
Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kutengeneza faili la apk kwa ajili ya ku share app yako, na faili la aab kwa ajili ya ku publih app yako. Soma Zaidi...

FLUTTER somo la 20: Jinsi ya ku sign App ya android kwenye flutter
Somo hili litakufundisha hatuwa kwa hatuwa jinsi ya ku sign app ya android kwenye flutter Soma Zaidi...

Flutter somo la 15: Jinsi ya kuweka icon kwenye App ya flutter
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia icon yaani kuweka icon kwenye App ya flutter. Soma Zaidi...

Flutter somo la 5: widget ni nini na zinafanya nini kwenye flutter
Katika somo hili uatwkeda kujifunza zaidi kuhusu widget, maana yake, aia zake na kazi zake kwneye flutter. Soma Zaidi...

FLUTTER somo la 2: Jinsi ya kutengeneza App ya flutter
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutengeneza App yako ya kwanza ya Flutter hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...