Flutter somo la 12: widget ya padding

Katika somo hili utakweda kujifunza jinsi ya kutumia widget ya padding kwenye App yako.

Kwenye Flutter, "padding" ni widget ambayo inatumika kuzunguka widget nyingine na kuongeza nafasi kati ya mipaka ya widget hiyo na yaliyo ndani yake. Hii ni muhimu sana kwa kurekebisha muundo wa programu yako na kufanya mambo kuonekana vizuri.

 

Unapofaset padding maana yake unaset je unataka text zako ama maudhui ya app yako yaanzie wapi kwenye screen kutoka kwenye ukuta wa screen. Na hapa tunazungumzia pande zote za screen.

 

Matumizi ya padding:

Katika padding tutatumia class ya  EdgeInsets ambayo ina property kama :- 

 

all hii utaset padding sawa kwa pande zote yaani juu, chni, kulia na kshoto. Mfano kama utataka ianzie pixel ya 8 kutoka kwenye ukuta wa screen basi itakuwa hivyo hivyo kwa pande zote. Mfano padding: EdgeInsets.all(16.0) hii itaset padding kuanzia pixel ya 16 kwa pande zote. Kipimo hapa ni dp yaani device pixel.

 

only hii itakulazimu kutaja padding kwa kila upande katika pande hizo nne. Pande zinajulikana kwa majina top yaani juu, bottom  yani chini,  left yaani kushoto na right yaani kulia. Mfano 

padding: EdgeInsets.only(

    top: 16.0,

    left: 24.0,

    right: 24.0,

    bottom: 16.0,

  )

 

symmetric hii hutumika kama unataka kuset kwa wima ama kwa mlalo. Wima ni vertical na mlalo ni horizontal. Mfano

padding: EdgeInsets.symmetric(

    vertical: 16.0,

    horizontal: 24.0,

  )

 

fromLTRB hii ni kama ya only inaset kutoka katika pande zote. L ni left, R ni right, T ni top na B ni botom. Utofauti mkubwa uliopo ni kuwa hapa kwenye fromLTRB tunaset kila moja kivyake, na ambayo hatuhitaji kuset utaiwekea 0. Lakini zile za oly utaset unazotaka ambayo hutaki kuset utaiwaca kabisa. Inamaana kwenye only unaweza kujaza pande mbili tu, lakini kwenye fromLTRB lazima ujaze zote nne, usioitaka utaweka 0.

padding: EdgeInsets.fromLTRB(

    10.0, // left

    20.0, // top

    30.0, // right

    40.0, // bottom

  ),

 

Zingatia kuwa kama ilivyo kwenye LTRB basi na kwenye kuweka value ni hivyo hivyo, ya kwanza ni left, ya pili ni top, ya tatu ni right na ya nne ni bottom.

 

import 'package:flutter/material.dart';

 

void main() {

 runApp(MyApp());

}

 

class MyApp extends StatelessWidget {

 ">...

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Flutter Main: ICT File: Download PDF Views 803

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 web hosting    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Tafasiri ya Riyadh Swalihina   

Post zinazofanana:

Flutter somo la 9: Jinsi ya kutumia widget ya Row

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu row widget. Hii ni widget ambayo ina utofauti na column widget kwa kuwa hii yenyewe inapangilia maudhui kwa safu za mlalo, tofauti na iliyopita inapangilia kwa safu za wima.

Soma Zaidi...
Flutter somo la 16: Jinsi ya kuweka drawer menu

Katika somo hili utakwenda kujifunza jisni ya kuweka drawer menu kwenye app ya flutter.

Soma Zaidi...
Flutter somo la 7: jinsi ya kutumia Widget ya AppBar

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu widget ya AppBar. Hata tutaona inavyofanya kazi na baadhi ya property zake.

Soma Zaidi...
Flutter somo la 14: Jinsi ya kuweka picha

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu widget ya Image ambayo hutumika kuonyesha picha kwenye App.

Soma Zaidi...
Flutter: Somo la 3: Mambo muhimu kuhusu App ya flutter

Katika somo hili tutakwend akuyaona baadhi ya maeneo muhimu ya kuanzia kuyajuwa kwa ajili ya course ya flutter kwneye android studio.

Soma Zaidi...
Flutter somo la 6: Scaffold widget, kazi zake na property zake

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu scaffold widget. Hapa tutakwend kuona properties zake na baadhi ya mifano.

Soma Zaidi...
FLUTTER somo la 18: Jinsi yakubadili App name kwenye flutter

Katika somo hili utakwenda kujifunzajinsi ya kubadilisha, jinala App yaani App name.

Soma Zaidi...
FLUTTER somo la 19: jinsi ya kubadili app id ama bundle identifier na configuration nyingine

Katika somo hili utajifunza jisni ya kubadili package name ama app id kwenye Android app na Bundle Identifier kwenye iOS app na taarifa nyinginezo.

Soma Zaidi...
Flutter somo la 11: Matumizi ya text widget

Katika Flutter, Text Widget ni kipengele kinachotumiwa kuonyesha maandishi kwenye programu. Kwa kawaida, hutumiwa kama sehemu ya muundo wa UI ya programu za Flutter.

Soma Zaidi...
Flutter somo la 10: Jinsi ya kutumia widget ya container

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu widget ya container pia tutajifunza jinsi widget hii inavyoweza kutumika na widget nyingine.

Soma Zaidi...