image

Flutter somo la 7: jinsi ya kutumia Widget ya AppBar

Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu widget ya AppBar. Hata tutaona inavyofanya kazi na baadhi ya property zake.

AppBar ni sehemu muhimu sana katika maendeleo ya programu za Flutter. Inaruhusu kuunda vichwa vya skrini (sasa hivi ni pamoja na kichwa cha juu cha skrini kwenye programu ya simu au kichwa cha programu ya wavuti) na huja na propertynyingi za kawaida kama vile kichwa cha programu, menyu za kushoto na kulia, vifungo vya kuingia, na zaidi.

 

Baadhi ya property zake:

Hapa kuna baadhi ya propertymuhimu za AppBar katika Flutter:

 

1. title: Widget inayoonyeshwa kama kichwa cha AppBar.

2. leading: Widget inayoonyeshwa kushoto ya AppBar, mara nyingi hutumika kwa ikoni ya kurudi nyuma.

3. actions: Orodha ya Widgets zinazoonyeshwa kulia ya AppBar, kawaida hutumika kwa vifungo vya kuingia.

4. backgroundColor: Rangi ya asili ya AppBar.

5. elevation: Kivuli cha AppBar kwa kina fulani.

6. brightness: Mwanga wa mwonekano wa AppBar (Brightness.light au Brightness.dark).

7. centerTitle: Boolean inayoonyesha ikiwa kichwa cha AppBar kinapaswa kuwa katikati au la.

8.iconTheme: Mwonekano wa ikoni kwenye AppBar.

9.textTheme: Mwonekano wa maandishi kwenye AppBar.

10.automaticallyImplyLeading: Boolean inayoamua ikiwa AppBar itajumuisha kiatu cha kurudi nyuma moja kwa moja kulingana na hali ya Scaffold.

11.toolbarOpacity: Utupu wa mwonekano wa chombo cha zana kwenye AppBar.

12.bottom: Widget inayoonyeshwa chini ya AppBar, kama vile TabBar.

 

Hizi ni baadhi tu ya propertyzinazopatikana kwa AppBar katika Flutter. Unaweza kuchunguza propertyzaidi na kujifunza jinsi ya kuzitumia kwa undani kwenye docs rasmi za Flutter kwa AppBar.

 

Katika como hili tunakwedna kufanyia kazi code hizi:

import 'package:flutter/material.dart';

 

void main() {

 runApp(

   MaterialApp(

     home: Scaffold(

       appBar: AppBar(

         title: Text('Bongoclass'),

         backgroundColor: Colors.blue,

       ),

     ),

   ),

 );

}

 

 

Sasa tutaanza kuweka widget moja moja kwenye AppBar. Kama ukiangalia code hapo juu ni zile zile ambazo tunazifahamu. Hapo utapata title na backround color kwenye appbar. Sasa sisi tunataka kuongeza vitu vifutavyo:

 

Kuziweka text katikati (center):

Kufanya text ziwe katikati tutatumia property ya centerTitle: true, utaweka true kama unahitaji ziwe katikati. Mfano

appBar: AppBar(

 title: Text('Bongoclass'),

 centerTitle: true,

),

 

Kuongezastyle kwenye text:

Unaweza pia kurembesha hizo text kw amfano kuweka rangi, kuongeza ukubwa, kuzifanya bold, italics na style nyinginezo. Kuweka style tutatumia property ya style. Kisha kuongeza ukubwa utatumia property ya TextStyle() ambapo ndani yake utaweka prpperty unazotaka. Kama ni ukubwa utatumia fontSize kisha utaweka value. style: TextStyle(fontSize: 24.0). Na kama nirangi utaweka color: mfano color: Colors.green. Kuweka style kwenye maandisha kama italics utatumia fontStyle na kuweka mandishi yawe bold utatumia font Weight mfano fontStyle: FontStyle.italic,

 

Mafano wa code:

import 'package:flutter/material.dart';

 

void main() {

 runApp(

   MaterialApp(

     home: Scaffold(

       appBar: AppBar(

         title: const Text(

           'Bongoclass',

           style: TextStyle(

             fontSize: 24.0,

             color: Colors.green,

             fontStyle: FontStyle.italic, // Set text to italic

             fontWeight: FontWeight.bold, // Set text to bold

           ),

         ),

         centerTitle: true,

         backgroundColor: Colors.blue,

       ),

     ),

   ),

 );

}

 

 

Utaona hapo nimetumia keyword const hii sio lazima ila ni vyema kuiweka ilikwamba endapo text itakuwa tupu basi program itatafuta text zilizopo ili kuziweka hapo kwenye bar. Hivyo ni vyema kuiweka hapo ijapokuwa hata ukitowa haina athari endapo text zitakuwepo.

 

Kuweka action kwenye appbar:

Hizi zinaweza kuwa ni batani ala text chochote ambacho utakiweka kwenye appbar il kiwe mlango wa kufikia taarifa nyingine. Tunatumia hizi action kufanya jambo.">...



           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2024-02-18 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 211


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Flutter somo la 15: Jinsi ya kuweka icon kwenye App ya flutter
Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia icon yaani kuweka icon kwenye App ya flutter. Soma Zaidi...

Flutter: somo la 4: Jinsi ya kuandika code za App ya flutter, hatuwa kwa hatuwa
Katika somo hili utakwenda kujifunza sasa jinsi ya kuandika code za app yetu kwenye flutter framework. Soma Zaidi...

Flutter somo la 13: widget ya batani
Katika somo hili uatakwenda kujifunz ajinsi ya kutumia batani na kuweka maumbo mbalimbali ya batani. Soma Zaidi...

FLUTTER somo la 2: Jinsi ya kutengeneza App ya flutter
Katika somo hili utajifunza jinsi ya kutengeneza App yako ya kwanza ya Flutter hatuwa kwa hatuwa. Soma Zaidi...

Flutter somo la 8: Jinsi ya kutumia widget ya column
Katika somo hili utakweda kujifunza kuhsu widget ya column. Widget hii ni moja katika widget zilizo muhimu sana kuzifaham. Soma Zaidi...

Flutter somo la 14: Jinsi ya kuweka picha
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu widget ya Image ambayo hutumika kuonyesha picha kwenye App. Soma Zaidi...

Flutter somo la 6: Scaffold widget, kazi zake na property zake
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu scaffold widget. Hapa tutakwend kuona properties zake na baadhi ya mifano. Soma Zaidi...

Flutter somo la 12: widget ya padding
Katika somo hili utakweda kujifunza jinsi ya kutumia widget ya padding kwenye App yako. Soma Zaidi...

Flutter: Somo la 3: Mambo muhimu kuhusu App ya flutter
Katika somo hili tutakwend akuyaona baadhi ya maeneo muhimu ya kuanzia kuyajuwa kwa ajili ya course ya flutter kwneye android studio. Soma Zaidi...

Flutter somo la 9: Jinsi ya kutumia widget ya Row
Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu row widget. Hii ni widget ambayo ina utofauti na column widget kwa kuwa hii yenyewe inapangilia maudhui kwa safu za mlalo, tofauti na iliyopita inapangilia kwa safu za wima. Soma Zaidi...

Flutter somo la 11: Matumizi ya text widget
Katika Flutter, Text Widget ni kipengele kinachotumiwa kuonyesha maandishi kwenye programu. Kwa kawaida, hutumiwa kama sehemu ya muundo wa UI ya programu za Flutter. Soma Zaidi...

Flutter somo la 10: Jinsi ya kutumia widget ya container
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu widget ya container pia tutajifunza jinsi widget hii inavyoweza kutumika na widget nyingine. Soma Zaidi...