Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kubadili app icon kwenye app ya Android na iphone kwenye flutter.
App icon ni moja katika sehemu muhimu sana katika kuvutia mtumiaji. App ikiwa na icon nzuri ndipo inavutia zaidi. App icon ni ile picha ndogo ambayo inaonekana kwenye kifaa chaka endapo app ipo installed. Mtumiaji akibofya icon hiyo ndipo ataweza kuifunguwa App hiyo.
Default App icon
Flutter wanakupa icon yao by default, ila unatakiwa uibadilishe wakati app yako unataka kuiweka kwenye app store. Hapo chini nimekuletea default app icon
Wapi app icon inapatikana.
Ili uweze kubadili icon itakuwa vyema kwanza ujuwe iyo icon inakaa wapi kwenye App ya flutter. Location ya icon inatofautiana kulingana na aina ya App.
Kwa App ya android
Kwa app ya Android icon inapatikana kwenye folder linaloitwa res. Folder hili utalipata kwenye kwenye Andrid -> src -> main -> res ndani ya folder la res utakutana na mafolder kama:-
Mipmap-hdpi
Mipmap-mdpi
Mipmap-xhdpi
Mipmap-xxhdpi
Mipmap-xxxhdpi
Ndani ya mafolder hayo ndip utakuta hizo icon. Icon zina ukubwa tofauti kulingana na device. Ukiangalia humo utaona kutoka mipmap-hdpi picha ni ndogo ila huongezeka kila unapokwenda chini.
B. Kwa watumiaji wa ios
Ama unatengeneza App kwa ajili ya iOS basi icon utazikuta kwenye folder linaloitwa AppIcon.appiconset hili linapatikana kwenye ios -> Runner -> Assets.xcassets -> AppIcon.appiconset hapo utakutana na orodha ya icon kwa kkukubwa tofauti tofauti.
Kutengeneza icon:
Sasa kwakuwa tumeshajuwa icon zinapokaa sasa tutatakiwa kujifunza kutengeneza icon kwa ajili ya app yetu. Kuna mitandao mingi (website) inayotoa huduma hii ya kutengeneza icon free. Katika mafunzo haya tutatumia website inayoitwa appicon. Ingia kwenye browser yako kisha andika www.appicon.co kisha fuata hatuwa hizo hapo chin:-
Kwenye menu ya website hakikisha upo kwenye App Icon. chini yake utaona kuna palipoandikwa click or drag image file. Bofya hapo hapo, utapelekwa kwenye kuchaguwa faili la picha la ku upload.
...
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu widget ya container pia tutajifunza jinsi widget hii inavyoweza kutumika na widget nyingine.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza jinsi ya kutengeneza faili la apk kwa ajili ya ku share app yako, na faili la aab kwa ajili ya ku publih app yako.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu row widget. Hii ni widget ambayo ina utofauti na column widget kwa kuwa hii yenyewe inapangilia maudhui kwa safu za mlalo, tofauti na iliyopita inapangilia kwa safu za wima.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza jinsi ya kutumia icon yaani kuweka icon kwenye App ya flutter.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakweda kujifunza kuhsu widget ya column. Widget hii ni moja katika widget zilizo muhimu sana kuzifaham.
Soma Zaidi...Katika somo hili uatwkeda kujifunza zaidi kuhusu widget, maana yake, aia zake na kazi zake kwneye flutter.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu widget ya Image ambayo hutumika kuonyesha picha kwenye App.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakwend akujifunza kuhusu scaffold widget. Hapa tutakwend kuona properties zake na baadhi ya mifano.
Soma Zaidi...Katika somo hili utakweda kujifunza jinsi ya kutumia widget ya padding kwenye App yako.
Soma Zaidi...Katika somo hili tutakwend akuyaona baadhi ya maeneo muhimu ya kuanzia kuyajuwa kwa ajili ya course ya flutter kwneye android studio.
Soma Zaidi...