kwa nini riba ni haramu?

kwa nini riba ni haramu?

Uharamu wa Riba katika Uislamu


Kwanza, Uislamu umeharamisha riba kwa sababu ni dhulma (unyonyaji).Ukichukua mkopo wa riba uliochukuliwa kwa madhumuni ya kukidhi haja ya matumizi ya lazima ya nyumbani, utozaji wa riba unakiuka lengo la Allah la kuumba (kuleta) mali kwa wanadamu. Utaratibu aliouweka Allah ni kwamba kwa kuwa mali ameileta kwa wanaadamu wote:


'Yeye (Allah) Ndiye aliyekuumbieni vyote vilivyomo katika ardhi...' (2:29).
Ni lazima matajiri (wenye mali) wawapatie wanyonge na wenye dhiki mahitaji yao muhimu ya maisha.Pili, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababu inahamisha mali kutoka kwa maskini au wanyonge na kuipeleka kwa tajiri ambayo huzidi kuondoa usawa katika mgawanyo wa mali. Hii ni kinyume na mahitaji ya jamii. Uislamu unataka kila mtu apate mahitaji muhimu ya maisha. Hivyo wale walio na ziada ya mahitaji muhimu ya maisha wanatakiwa wawape wasionacho kabisa au wale waliopungukiwa kwa upendo na udugu. Riba inakanusha kabisa msimamo huu.Tatu, riba imeharamishwa katika Uislamu kwa sababu hufanya kundi la watu katika jamii liishi kivivu bila ya kufanya shughuli yoyote ya uzalishaji, likitegemea kuishi kwa riba kutokana na mali zao walizozikusanya katika mabenki, bima, na vyombo vingine vya riba. Jamii inakosa mchango wa watu hawa katika uzalishaji na si hivyo tu, bali watu hawa wanakuwa mzigo na bughudha katika jamii. Ufasiki (uharibifu) wa aina zote katika ardhi hufanywa na kundi hili.
                   
Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 179


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Kiwango cha mahari katika uislamu
Kiasi gani Kinachojuzu kutolewa Mahari? Soma Zaidi...

Kibri cha Ibilis na Uadui Wake Dhidi ya Binadamu
Ibilis ni katika jamii ya majini aliyekuwa pamoja na Malaika wakati amri ya kumsujudia Adam inatolewa. Soma Zaidi...

NAMNA YA KUSWALI SEHEMU YA KWANZA
Mtume (s. Soma Zaidi...

Tamko la suluhu baada ya vita vya Siffin
Soma Zaidi...

Historia ya Dhana ya Kudhibiti Uzazi
Soma Zaidi...

DUA YA 1 - 10
1. Soma Zaidi...

HISTORIA NA MAISHA YA NABII ISMAIL(A.S)
Ismail(a. Soma Zaidi...

Hadhi na haki za mwanamke katika uislamu
4. Soma Zaidi...

kwa nini riba ni haramu?
Soma Zaidi...

Nini maana ya Kushahadia nguzo ya kwanza ya uislamu
Soma Zaidi...

Maana ya Swaumu na Lengo la kufunga
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Mbegu za maboga
Soma Zaidi...