Navigation Menu



image

Haki na wajibu wa mke kwa mumewe na familia

Haki na wajibu wa mke kwa mumewe na familia

Wajibu wa Mke kwa Mumewe:



Wanawake nao wanawajibika kisheria kwa waume zao kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo:


"... Nao (wanawake) wanayo haki kwa sheria (kufanyiwa na waume zao) kama ile haki iliyo juu yao kuwafanyia waume zao. Na wanaume wana daraja zaidi kuliko wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu mwenye hi/dma ". (2:228). Ili nyumba iwe ya furaha na amani, mwanamke naye anatakiwa ajitahidi kwa kadri ya uwezo wake kumfanyia mumewe yafuatayo:


(i)Kumtii mumewe katika mambo yote mema atakayomuelekeza:



Ilivyo ni kwamba, Mwenyezi Mungu (s.w), kwa Hekima yake isiyo mipaka, ametuumba na kututofautisha katika maumbile na vipaji iii tuweze kutegemeana na kusaidiana katika kuliendea lengo Ia kuwepo kwetu hapa ulimwenguni. Wanaume kulingana na umbile lao na jukumu lao Ia kuiangalia familia na kukidhi mahitaji yote muhimu ya maisha wamepewa wadhifa wa kuwa walinzi wa familia kama tunavyofahamishwa katika Qur-an:


Wanaume ni walinzi wa wanawake, kwa sababu Mwenyezi Mungu amewafadhilisha baadhi yao kuliko wengine na kwa sababu ya mali zao wanazozitoa (katika kukidhi haja zao). Basi wanawake wema ni wale wenye kutii, wanaojihfadhi (hata) was ipokuwepo (waume zao), kwa kuwa Mwenyezi
Mungu amewaamrisha wajihfadhi... (4:34).



Mke kumtii mumewe katika mambo ya kheri, si kwa ajili ya kumfurahisha mumewe tu bali ni katika kumtii Mwenyezi Mungu (s.w). Pia msisitizo wa mke kumtii mumewe unabainika katika hadithi ifuatayo:



Abu Hurairah(r.a) ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu aliulizwa: Ni nani mbora kuliko wote katika wanawake? Alijibu: Yule anayempa (mumewe)furaha wakati anapomuangalia, anayemtii wakati anapomuelekeza afanye jambo) na ambaye hampingi kuhusu yeye mwenyewe na mali yake kwa kuchelea, kutomfurahisha (kumuudhi). (Nisai).



Pia tunafahamishwa katika hadithi aliyosimulia Abu Sayid al-Khudri (r.a) kuwa Mtume (s.a.w) amesema:


"... Hapana mwanamke atakayefunga (funga ya sunnah) bila ya ruhusa ya mumewe..." (Abu Daud, Ibn Majah).
Kwa ujumla mwanamke anatakiwa apate ruhusa ya mumewe ndio afanye Ibada za nafil (sunnah). Mwanamke aliyekasirikiwa na mumuewe kwa sababu ya kutomtii katika jambo Ia kheri, laana ya Mwenyezi Mungu inakuwa juu yake. Pamoja na msisitizo huu, mke hatamtii mumewe katika mambo ya haramu. Katika Hadithi aliyoisimulia Au (r.a) Mtume (s.a.w) amesema: Hapana ruhusa kumtii yeyote katika kumuasi Mwenyezi Mungu. Utii ni katika mambo ya kheri tu. (Bukhari, Muslim, Abu Daud, na Nisai).



(ii)Kumfurahisha Mumewe na Kumliwaza:



Mke hana budi kuifanya nyumba yake mahali pa furaha na utulivu wa mawazo kwa mumewe. Inatakiwa mwanamume anapotingwa na mambo magumu katika harakati za kutafuta maisha na kusimamisha Dini ya Mwenyezi Mungu (s.w), apate maliwazo kutoka kwa mkewe arejeapo nyumbani. Kazi nzuri na ya kuigwa aliyoifanya Bibi Khadija katika kumliwaza na kumpa moyo Mtume (s.a.w) katika mwanzo wa utume wake, haitasahauliwa katika historia. Khadija ni mkewe Mtume (s.a.w) wa kwanza ambaye ndiye mtu wa kwanza kumuamini Mtume.Alipokaribia kupewa utume, Mtume Muhammad (s.a.w) alihamia pangoni katika mlima Hiraa iii kupata utulivu na wasaa kufikiri juu ya namna ya kuyaondoa maovu yaliyo kithiri katika jamii yake kwa msaada wa Allah (s.w). Kweli Allah (s.w) alimuwezesha kuikomboa jamii yake kwa kumpa utume na mwongozo kama tunavyojifunza katika Suratidh-Dhuha na Nashraka:


Soma kwa jina la Mola wako Aliyeumba. Amemuumba mwanaadamu kwa pande la damu. Soma, na Mola wako ni Karimu sana ". (96:1-3).



"Basi ukishamaliza (kulingania) shughulika (kwa ibada). "(94:7).
Mzigo uliovunja mgongo wa Mtume (s.a.w), si jengine bali ni yale maovu yaliyokithiri katika jamii yake, ambayo alipania kuyaondoa lakini hakuweza. Ndipo Allah (s.w) akamuwezesha kuyaondoa kwa kumpa utume na mwongozo kama tunavyojifunza katika aya hizo.



Khadija hakumkataza Mtume kuhamia pangoni wala hakulalamika. Badala yake alimtengenezea masurufu na kumpelekea Mtume Muhammad (s.a.w) alikaa pangoni takribani kwa muda wa miaka miwili.



Khadija hakumkataza wala hakulalamika.Badala yake alimtengenezea masurufu na kumpelekea, kumpeleka Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa pangoni takriban kwa muda wa miaka miwili. Alipojiwa na Jibril na kumpa wahyi wa kwanza Mtume (s.a.w) aliogopa sana na akarejea nyumbani na kumueleza mkewe juu ya tukio hilo, na kumwambia kuwa alihofia kuwa amejiwa na pepo mbaya. Khadija alimfariji sana, akamwambia: "Hilo haliwezi kuwa Mwenyezi Mungu (s.w) hatakuacha udhurike. Kwani wewe u mwema kwa ndugu zako, unawasaidia wale waliodhaifu, unawapa sadaqa wenye shida, unasema kweli, umkarimu kwa wageni wako na unafariji wale wenye dhiki". Yaani kwa tabia yako hii njema Allah hatakuacha udhurike.



Hebu fikiria hofu, wasi wasi na msukosuko mkubwa aliokuwa nao Mtume (s.a.w) na halafu fikiria utulivu alioupata baada ya kufarijiwa hivyo na mkewe. Hapana shaka faraja hiyo ilimpa nguvu za kusubiri na kuhimili misukosuko iliyofuatia. Bibi Khadija (r.a) alishiriki kikamilifu katika misukosuko yote aliyoipata Mtume (s.a.w). Mtume (s.a.w) alibughudhiwa sana na makafiri wa Makka. Lakini kila aliporejea nyumbani alifarijika kutokana na moyo wa mapenzi na huruma na maneno ya faraja kutoka kwa bibi Khadija. Hivyo Bibi Khadija(r.a) alitimiza jukumu muhimu sana katika kipindi hicho kigumu.


Mtume naye alimpenda sana mkewe, na alikumbuka huduma na maliwazo yake katika maisha yake yote. Kila mara alikuwa akimkumbuka na kumsifia sana Khadija,mpaka akamfanya bibi Aysha kuwa na wivu na kumuuliza: "Huishi kumtaja huyu bibi Kizee Khadija, je Mwenyezi Mungu hajakupa badala yake mke bora kuliko yeye?" (Akimaanisha yeye mwenyewe, Aysha). Mtume (s.a.w) alichukia na akasema: "La! Hajanipa badala yake mke bora kuliko yeye. Khadija aliukiri Uislamu wakati watu wengine waliukanusha, alinikiri wakati watu wengine walinikanusha, aliniunga mkono kwa mali yake na akaiweka mali yake chini yangu na chini ya 'Waislamu wakati watu wengine walikataa kutusaidia".



Khadija ni miongoni mwa maswahaba waliobashiriwa pepo na Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Imepokelewa kutoka kwa Abu Hurairah kuwa amesema: "Jibril alimjia Mtume (s.a.w) akamwambia, 'Ewe Mjumbe wa Allah, anakuja Khadj/a na chombo ambacho ndani yake kuna chakula na kunywaji, atakapokuja mpe salamu kutoka kwa Bwana wake (Allah (s.w)) na kutoka kwangu (Jibril) halafu mbashirie nyumba peponi ilyojengwa kwa lulu, ambayo hamna kelele ndani yake wala uchovu" (Bukhari).



(iii)Kuhifadhi Nyumba na Mali ya Mume:
Mwanamke ni malkia wa nyumbani mwenye jukumu Ia kuhakikisha kuwa usalama na unadhifu unakuwepo nyumbani. Mwanamke hana haki ya kumkaribisha yeyote nyumbani kwake pasi na idhini ya mumewe. Kwa maana nyingine, mwanamke haruhusiwi katika sheria ya Kiislamu, kumkaribisha mtu yeyote ambaye mumewe hataki akaribishwe nyumbani kwake, awe wa kike au wa kiume. Mtume (s.a.w) katika Hadith iliyosimuliwa na Amr bin Al-As (r.a) amewausia waislamu kama ifuatavyo:
Jueni kuwa nyinyi mna haki juu ya wake zenu, na wao wana haki juu yenu. Miongoni mwa haki zenu juu ya wake zenu ni kuwa wasimuweke juu ya matandiko (viti yenu msiyemtaka, wala wasimkaribishe katika ma] umba yenu msiyemtaka. ('Tirmidh,)


Mwanamke pia, ni wajibu wake kutunza mali ya mumewe na asitoe kumpa yeyote pasina ruhusa yake kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Abu Umamah ameeleza: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu akisema katika khutuba yake katika Hi/a ya kuaga: "Hapana mwanamke yeyote atakayetumia kitu chochote kutoka kwenye nyumba ya mumewe, bila ya ruhusa yake. Aliulizwa: Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu! Wala chakula? Al/ibu: Hicho ndicho kitu chetu kilicho bora kuliko vyote. (Tirmidh)



Hadithi hii inasisitiza kuwa mke hatatoa mali ya mumewe kinyume na ridhaa yake. Lakini kama mke, kwa kumfahamu mumewe kuwa hatakuwa na neno, anaweza kutoa sadaqa pasina idhini yake lakini atapata nusu ya malipo atakayopata mumewe, kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:



Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: Mwanamke akitumia (akitoa) kitu cha mumewe bila ya ruhusa yake, atapata nusu ya malpo ya mumewe. (Bukhari na Muslim)



Katika kutunza mali ya mume ni pamoja na kujizuia kufanya israfu. Ni jukumu Ia mke kuhakikisha kuwa hapana ubadhirifu wa chakula, nguo n.k. na kila kitu katika nyumba kinatunzwa vizuri. Mwenyezi Mungu (s.w) hawapendi wenye kufanya ubadhirifu wala ubakhili bali katika waja wake anaowapenda ni pamoja Na wale ambao wanapotumia hawatumii kwa fujo (hawafanyi ubadhirfu) wala hawafanyi ubakhili, bali wanakuwa katikati baina ya hayo. (25:67).



(iv)Kuwa na Subira juu ya Mumewe:



Mume na mke wote wanawajibika kuvumiliana na kusubiriana. Hakuna mwanaadamu aliyekamilika. Kama walivyo na udhaifu wanawake, vile vile wanaume wana udhaifu wao. Takriban kila mtu hakosi udhaifu ambao si wenye kumpendezesha mwenziwe. Kama wanaume walivyosisitizwa kuwavumilia wake zao kwa udhaifu kama huu, na wanawake pia hawana budi kuwavumilia waume zao endapo watakuwa na udhaifu usiopendeza. Kufanyiana subira ni jambo linalopendeza mno mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) na lina malipo makubwa kama tunavyojifunza katika aya mbali mbali za Qur-an:


Enyi mlioamini! Jisaidieni (katika mambo yenu) kwa kusubiri na kuswali. Bila shaka Mwenyezi Munguyupamoja na wanaosubiri. (2:153).



(v)Kutosheka na kile anachopewa na Mumewe:



Mwanamke hana budi kujizuilia na kumtaka mumewe ampatie matumizi ambayo hana uwezo nayo. Kwa upande wa mume, kama tulivyoona hana budi kwa kadiri ya uwezo wake kukidhi mahitaji muhimu ya mkewe na familia yake kwa ujumla. Pia ni vyema, kama mume ana uwezo mkubwa, ampe mkewe ziada ya mahitaji muhimu na amzawadie mara kwa mara. Katika Qur-an tunajifunza kuwa:


Mwenye wasaa agharimu kwa kadri ya wasaa wake; na yule ambaye amepungukiwa riziki yake, atoe katika idle alichopewa na Mwenyezi Mungu; Mwenyezi Mungu hamkalflshi mtu yeyote ila kwa kadiri alichompa. Atajaalia Mwenyezi Mungu baada ya dhikifaraja. (65:7).



Endapo mke atamdai mumewe hiki na kile na hali anaona kuwa uwezo wake ni mdogo, kwa vyovyote vile atamfanya mumewe aishi kwa wasi wasi. Atamuona mkewe kuwa hamtakii jema na hiyo itakuwa ni sababu tosha ya kuondoa mapenzi na huruma katika unyumba na kuvuruga amani katika familia.


Wanawake wa Kiislamu wanatakiwa wawasaidie waume zao kwa kila hali na wawaonee huruma na kuwatuliza na kuwaliwaza badala ya kuwakamua na kuwataka watoe hata kile wasicho na uwezo nacho. Katika historia tunajifunza kuwa wakeze Mtume (s.a.w) , kibinaadamu walighafihika na kumtaka Mtume (s.a.w) awape matumizi yaliyokiuka uwezo wake. labia hii ilimuudhi sana Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Kutokana na tabia yao hii Mtume (s.a.w) aliwahama kwa kipindi cha mwezi mmoja (siku 29) kama tunavyojifunza katika hadithi ndefu iliyosimuliwa na Jabir (r.a) na kukusanywa na Imam Muslim. Baada ya kipindi hiki, Mwenyezi Mungu (s.w) alimshushia Mtume wake wahyi, ufuatao:


Ewe Mtume! Waambie wake zako: Ikiwa mnapenda maisha ya hii dunia na uzuri wake (mimi sinayo, na mimi siwezi kukulazimisheni kukaa na mimi katika hali ya ufakiri) njooni, nitakupeni kitoka nyumba, na kukuacheni muwachano mzuri. Na kama mnataka Mwenyezi Mungu na Mtume wake na nyumba ya Akhera, basi Mwenyezi Mungu amewaandalia wafanyao mema hayo, miongoni mwenu, malipo makubwa. (33:28-2 9)



Aya hizi hazikuwahusu wakeze Mtume (s.a.w) tu, bali zinawahusu wanawake wote wa Kiislamu kuwa watosheke na kile kidogo wanachowapa waume zao kulingana na uwezo wao, Mwenyezi Mungu (s.w) atakuwa radhi nao, na kuwapa furaha hapa ulimwenguni na ujira mkubwa huko akhera.



(vi) Kuwausia na kuwakumbusha kumcha-Allah (s.w).
Wanawake kama Waislamu wengine wana wajibika kuwaokoa waume zao na wapenzi wao wengine na moto kama anavyo usia Allah (s.w): Enyi mlioamini! Jiokoeni nafsi zenu na watu wenu, na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe. Wanausimamia malaika wakali, wenye nguvu, hawamuasi Mwenyezi Mungu kwa amri zake; na wanatenda wanayoamrishwa (yote)" (66:6)



Ni nani anayependa mpenzi wake ahiliki motoni? Kama mke anavyompenda na kumhurumia mumewe kwa kumfanyia mambo kadhaa yanayompendeza na kumfurahisha katika maisha haya mafupi ya dunia, basi anapaswa atoe kipaumbele katika kumuusia na kumkumbusha mumewe kumcha Allah (s.w) ili kwa rehma za Allah (s.w), waendelee kuwa pamoja katika starehe za kudumu milele huko peponi. Tunafahamishwa katika Quran kuwa watu walioshirikiana katika kumcha Allah (s.w) watakuwa pamoja.



"Na wale walioamini na wakafuatwa na wazee wao na watoto wao katika imani, Tutawakutanisha nao hao jamaa zao, wala Hatutawapunja kitu katika (thawabu za) vitendo vyao; kila mtu atalipwa kwa idle alichokichuma ".



"Na tutawapa (Idla namna ya (Matunda na (kila namna za) nyama, kama vile watakavyopenda ". "Watapeana humo gilasi (zilizojaa vinywaji) visivyoleta maneno ya upuuzi wala ya dhambi". "Iwe wanawapitia watumishi wao (wanaopendeza) kama kwamba ni lulu zilizomo ndani ya chaza (shaza) ndio kwanza zimepasuliwa.



"Wataelekeana wao kwa wao wanaulizana, (wanazungumza) •1 Waseme: "Tulikuwa zamanipamoja na watu wetu tukimuogopa (Mwenyezi Mungu) ". "Basi Mwenyezi Mungu amefutanyia ihsani, (ametutia Peponi) na ametuokoa na adhabu ya pepo za Moto". "Hakika sisi zamani tulikuwa tukimuabudu Yeye (tu Mwenyezi Mungu): Hakika Yeye ndiye Mwema, Mwenye rehema".(52:21-28).



Pamoja na jitihada hizi za mke kumuusia mumewe na watoto kucmha-Allah (s.w), hanabudi naye kuomba msaada wa Allah kwa kuleta mara kwa mara dua aliyotufunza Allah (s.w). Na wale wanaosema: "Mola wetu! Tupe katika wake zetu na watoto wetu yaburudishayo macho (yetu) (nyoyo zetu), na Utujaalie kuwa waongozi kwa wamchao (Mungu) ". (25:74).




                   







           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1732


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉5 Simulizi za Hadithi Audio     👉6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Ni mambo gani yanaharibu na kutengua udhu?
Soma Zaidi...

Jinsi ambavyo msafiri anatakiwa aswali akiwa safarini
Postvhiibinakwenda kukufundisha kuhusu swala ya msafiri na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Swala ya ijumaa, nguzo zake na suna zae, namna ya kuswali swala ya ijumaa
Soma Zaidi...

Taratibu za eda ya kufiwa katika uislamu
Hapa utajifunza taratibu za kukaa eda kwa mwanamke ambaye amefiwa na mume. Soma Zaidi...

Njia haramu za uchumi
Soma Zaidi...

Hijja na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sharti za kusihi kwa funga
Soma Zaidi...

Tofauti kati ya zakat na sadaqat
Nguzo za Imani, tofauti kati ya sadaqat na zakat (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Kusimamisha Swala na kuamrisha mema
Swala iliyosimamishwa vilivyo ndiyo nyenzo kuu ya kumtakasa Muislamu na kumpa sifa zinazomuwezesha kustahiki kufanya kazi takatifu ya kusimamisha Uislamu katika jamii. Soma Zaidi...

Maswali juu ya Mambo anayopaswa kufanyiwa maiti ya muislamu
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sunnah za funga ya ramadhan
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

ijuwe maawe maan ya kusimamisha swala
Soma Zaidi...