8.
8. Tatizo la Riba
Riba ni kupata chochote kile cha ziada kutoka katika mkopo au mtaji bila kushiriki katika faida au hasara. Mwenyezi Mungu anatufahamisha katika Qurβan:
Wale wanaokula riba hawasimami ila kama anavyosimama yule ambaye shetani kamzuga kwa kumsawaa; haya ni kwa sababu wamesema, Biashara ni kama riba, hali Mwenyezi Mungu amehalalisha biashara na kuiharamisha riba.(2:275)
Mwenyezi Mungu huyafutia (baraka mali ya) riba; na kuyatia baraka (mali iliyotolewa) sadaka (2:2 76).
Madhara ya riba katika jamii
(i)Riba inachafua nafsi ya Tajiri na uchumi wake. Tajiri ambaye hayuko tayari kukukopesha mali yake pasi na riba, kamwe hawezi kutoa mali yake bure kuwasaidia wanyonge na wenye dhiki. Tajiri asiye tayari kutoa mali yake kuwasaidia wenziwe wenye dhiki na shida katika jamii huwa mchoyo, bahili, mpupiaji mali, asiyetosheka na utajiri alionao, mfujaji, muonevu na dhalimu. Tajiri mwenye moyo wa namna hii hata kama atajiita Muislamu hawezi kamwe kuchunga mipaka ya halali na haramu katika kuchuma!
(ii)Riba inamkandamiza Mnyonge mwenye dhiki. Wanyonge na wenye dhiki katika jamii inayoendesha uchumi wake katika misingi ya riba, hawapati msaada wowote wa bure kutoka kwa matajiri kwa kiasi ambacho wengi wa wale wasiojiweza kabisa kujitosheleza kwa mahitaji muhimu ya maisha yao kwa namna duni sana - wengi hujipatia chakula chao kutoka katika mapipa ya taka (watoto wa mtaani), wengi hujisitiri kwa masalio yaliyookotezwa hapa na pale na wengi makazi yao ni stesheni na sokoni. Hawa, kisaikolojia, hujiona ni watu duni wasio na maana yoyote katika jamii na huwaona matajiri na watu wenye uwezo kuwa ndio wenye maana. Na hapa ndipo inapojengeka chuki baina ya wasionacho kuwachukia walio nacho.
(iii) Riba inaharibu uchumi wa jamii na maendeleo yake. Riba na msingi wake wa unyonyaji imma ikitozwa na tajiri mmoja au kikundi cha matajiri, imefanywa msingi wa uchumi wa taifa au wa kimataifa. Kwa bahati mbaya kutokana na mazoea tuliyonayo juu ya vyombo vya uchumi vya kitaifa na kimataifa vinavyoendeshwa katika misingi ya Riba kama vile mabenki ya taifa na shirika la Bima la Kimataifa, baadhi ya watu wamediriki kuhalalisha Riba ya mabenki na Bima. Kuhalalisha huku kwa riba ya mabenki na Bima aidha kumetokana na uzoefu wa uchumi haramu katika jamii zetu au umetokana na kushindwa kuona ubaya wa riba kitaifa au kimataifa.
Waislamu hatuna budi kukumbuka kuwa alichokiharamisha Allah (s.w) kinakuwa ni haramu katika wingi wake na katika uchache wake. Tukichukua mfano wa pombe Mtume (s.a.w.) amesema:
Kinacholewesha kikiwa kingi ni haramu pia hata kikiwa kichache. (Tirmidh, Abu Daud, Ibn Majah). Kwa hiyo kilicho haramishwa kwa mtu binafsi, pia ni haramu kwa taifa na ni haramu kwa mataifa yote ulimwenguni. Kwa upande mwingine jambo la haramu litakapotendwa kitaifa litakuwa na athari mbaya zaidi kwa jamii kuliko likitendwa katika kiwango cha mtu binafsi, hali kadhalika jambo baya likitendwa kimataifa huwa na athari kubwa na mbaya zaidi kwa jamii ya mwanadamu kuliko likitendwa katika kiwango cha kitaifa.
(iv) Riba ni mali ya dhulma inayonyakuliwa na matajiri kutoka kwa wanyonge kwa njia moja au nyingine kiuchumi, pia riba inaukandamiza na kuudidimiza uchumi wa kitaifa au kimataifa. Mali ya riba kwa kuwa ni mali inayopatikana bila jasho na bila hata ya kushiriki katika mashaka ya uchumi, huwafanya matajiri na wenye uwezo wa kuendesha miradi mbali mbali ya kiuchumi wakae tu bila kazi wakingojea fedha zao zizae katika mabenki ambazo wana kila uhakika wa kuzipata hata itokee gharka ya namna gani. Kwa hiyo kutokana na riba, jamii huwakosa watu wenye uwezo mkubwa wa kuzalisha mali ambao wangaliweza kuendesha miradi mbali mbali ya kiuchumi ambayo ingaliinua uchumi wa taifa na wa kimataifa kwa ujumla.
Wataalam wa uchumi wanakiri kuwa riba inaporomosha uchumi. Wamegundua kuwa kadiri kiwango cha riba kinavyokuwa kikubwa ndivyo uchumi unavyozidi kushuka kwa sababu matajiri huona kuwa wanapata faida kubwa zaidi na kwa njia nyepesi isiyotoa jasho lolote wakiweka fedha zao benki kuliko kuziingiza katika miradi ya kiuchumi. Hivyo utaona kuwa riba hupunguza uzalishaji na huongeza gharama za uzalishaji.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1046
Sponsored links
π1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
π2 Kitabu cha Afya
π3 Simulizi za Hadithi Audio
π4 Madrasa kiganjani
π5 kitabu cha Simulizi
π6 Kitau cha Fiqh
Mambo yanayodhaniwa kuwa yanaharibu funga lakini hayaharibu
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Mambo ambayo hayafunguzi funga
Hii ni orodha ya mambo ambayo hayawezi kuharimu funga yako endapo utayafanya. Soma Zaidi...
Shahada nguzo ya kwanza ya uislamu, sifa zake na umuhimu wake.
Soma Zaidi...
Shart kuu nne za swala
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu masharti ya swala. Soma Zaidi...
ijuwe maawe maan ya kusimamisha swala
Soma Zaidi...
Tarstibu za kulipa swaumu ya Ramadhani
Hapa utajifunza namna ambayo utatakiwa kulipa funga ya Ramadhani kwa siku ambazo hukufunga Soma Zaidi...
Kuandama kwa Mwezi na Kufunga ama kufungua ramadhani, sheria na hukumu za kuangalia mwezi
Soma Zaidi...
Nguzo za swala.
Kipengele hiki kinaelezea nguzo mbalimbali za kuswali. Soma Zaidi...
Sunnah za funga ya ramadhan
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Nini maana ya najisi, na ni zipi Najisi katika uislamu na aina za najisi
Soma Zaidi...
Yajuwe mandalizi ya Ibada ya hija
Soma Zaidi...
Swala ya ijumaa, nguzo zake na suna zae, namna ya kuswali swala ya ijumaa
Soma Zaidi...