Post hii fupi itakwenda kukujulisha utaratibu wa kula daku.
*NI UPI MUDA WA MWISHO KULE DAKU*?
Daku unaweza kula saa yote hadi inapoingia Alfajiri. Hii ni kutoka na kauli ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala):
((..وَكُلُواْ وَاشْرَبُواْ حَتَّى يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِ ثُمَّ أَتِمُّواْ الصِّيَامَ إِلَى الَّليْلِ...))
((…Na kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni Swawm mpaka usiku…)) [Al-Baqarah: 187]
Hivyo, unaruhusiwa kula daku hadi Alfajiri ndipo unapoanza kufunga. Na hata Muadhini akiadhini na kama una tonge au fundo la maji mdomoni usiliteme, kamilisha kulimeza kisha ndio uanze kufunga. Haya yamethibiti katika Sunnah kama inavyoonyesha Hadiyth ifuatayo:
عن ابن عمر رضي الله عنهما قال: كان لرسول الله صلى الله عليه وسلم مؤذنان: بلال وابن أم مكتوم .فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم ((إن بلال يؤذن بليل فكلوا واشربوا حتى يؤذن ابن أم مكتوم)) متق عليه
Kutoka kwa Ibn 'Umar (Radhiya Allaahu 'anhuma) ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) alikuwa na waadhini wawili; Bilaal na Ibn Ummi Maktuum. Akasema: ((Hakika Bilaal anaadhini usiku (adhana ya mwanzo), basi kuleni na mnywe hadi aadhini Ibn Ummi Maktuum)) [Al-Bukhaariy na Muslim]
Na Allaah Anajua zaidi
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Ugumba ni “ugonjwa wa mfumo wa uzazi unaofafanuliwa kwa kushindwa kupata ujauzito baada ya miezi 12 au zaidi ya kujamiiana bila kinga mara kwa mara. Utasa kutoweza kwa kiumbe hai kufanya uzazi wa ngono au kutoweza kupata mimba au kuchangia mimba.
Soma Zaidi...Post hii itakufundisha faida na umuhimu wa kijenga uchumi katika jamii ya kiislamu.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu: Shahada (EDK form 2:dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hapa utajifunza sera za kiuchumi katika uchumi wa kiislamu. Hapa utajifunza sera kuu tatu za uchumi wa kiislamu.
Soma Zaidi...Endapo mtu yupp katika orodha ya wanaotakiwa kutithi, anaweza kuzuiliwa kurithi kwa kuzingatia haya.
Soma Zaidi...