picha

Haki ya kumiliki mali katika uislamu

Haki ya kumiliki mali katika uislamu

Haki ya kumiliki mali



Kumiliki mali ni suala la kimaumbile na limeshikamana na silka ya kujihami (self presevation).Katika historia ya binaadamu suala la kumiliki mali limekuwa likiandamana na itikadi au falsafa inayotawala mahali.


Kwa mfano katika baadhi ya jamii za kitwaghuti umilikaji wa mali uko chini ya familia au huwa chini ya “watu wote” (mali ya umma) au huwa chini ya mtu au watu binafsi. Katika Uislamu kila kitu kipo chini ya miliki ya Mwenyezi Mungu:


“Sema Ee Mola uliyemiliki Ufalme wote! Humpa ufalme umtakaye na humuondolea ufalme umtakaye na humtukuza umtakaye na humdhalilisha umtakaye, kheri imo mikononi mwako. Bila shaka wewe ni Mwenye Uwezo juu ya kila kitu ”. (3:26).



Hivyo ni dhahiri kuwa Mwenyezi Mungu ndiye mmilikaji wa hakika wa vitu vyote. Binaadamu anamiliki mali kwa dhamana tu siyo kwa hakika na kwa sababu hiyo ataulizwa jinsi alivyotumia. Katika Qur-an Allah (s.w) ameruhusu watu binafsi au kwa vikundi kumiliki mali pale aliposema:


“Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe kwa ajili ya hizo (sadaka zao) na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaom bee dua. Hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu (watengenekewe); na Mwenyezi Mungu ndiye asikiaye na ajuaye.” (9:103)


Hivyo Uislamu unakubali na kuheshimu haki ya mtu au watu binafsi kumiliki mali.



Mipaka ya Umilikaji mali
(i)Mali hiyo iwe imechumwa kwa njia ya halali. Uislamu unaitambua haki ya kumiliki mali na haki ya kuilinda mali hiyo, lakini mali yenyewe iwe ya halali.



(ii)Mtu anaweza kuiuza au kuitumia mali yake apendavyo maadamu ana akili timamu. Iwapo hana akili timamu, itabidi apatikane mdhamini wa kuingalia mali hiyo kwa niaba na manufaa yake na manufaa ya jamii.



(iii)Maadamu mtu anayo mali basi anao pia wajibu wa kutekeleza majukumu yanayohusiana na mali aliyo nayo.



(iv)Uislamu unakataza ubakhili na israfu (ubadhirifu) katika matumizi. Mwenyezi Mungu anasema:


Wala usifanye mkono wako (kama) uliofungwa shingoni mwako, wala usikunjue ovyo ovyo, utakuwa ni mwenye kulaumiwa na kufilisika. (17:29).


Enyi wanaadamu! Chukueni mapambo yenu wakati wa kila sala; na kuleni (vizuri) na kunyw eni (vizuri). Lakini msipite kiasi tu. Hakika Yeye hawapendi wapitao kiasi. (7:3 1).


Ubadhilifu ni kufanya mojawapo ya mambo matatu
Kwanza,
kununua kitu usichokihitaji. Au kununua kitu unachokihitaji lakini kwa kiasi kingi kuliko unavyoweza kutumia. Kwa mfano kutengeneza chapati tano ilihali uwezo wako ni wa kula chapati mbili tu, halafu zile tatu ukazitupa jalalani.


Pili ni ubadhilifu kununua kitu chochote kile cha haramu, hata ikiwa kwa thamani ndogo namna gani. Kwa mfano hata kama masanduku laki moja ya bia yanauzwa kwa shilingi hamsini ukiitoa shilingi hamsini hiyo kununua pombe hiyo unaandikiwa madhambi ya ubadhilifu.


Tatu kutoa sadaka kwa ajili ya kujionesha kwa watu, badala ya kuandikiwa thawabu unaandikiwa madhambi ya israfu.



(v) Uislamu unakataza rasilimali zilizo katika jamii kuachwa bila kutumiwa Mtume (s.a.w) amesema mtu akiendeleza ardhi ana haki ya kuimiliki. Lakini akiiwacha kwa miaka mitatu bila kuitumia mtu mwingine ana haki ya kuiendeleza na kuimiliki.




                   


Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Fiqh Main: Dini File: Download PDF Views 1562

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 ai web app    👉2 Dua za Mitume na Manabii    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Bongolite - Game zone - Play free game    👉6 Madrasa kiganjani   

Post zinazofanana:

Mda wa mwisho wa kula daku mwezi wa ramadhani

Post hii fupi itakwenda kukujulisha utaratibu wa kula daku.

Soma Zaidi...
Kwanini funga imefaradhishwa mwezi wa ramadhani

Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Ufafanuzi kuhudu mgogoro wa mwezi ni muda gani mtu aanze kufunga.

Je inapoonekana sehemu moja tufunge duania nzima ama tufunge kwa kuangalia mwandamo katika maenro tunayoishi.

Soma Zaidi...
Riba na Madhara Yake Katika Jamii

- Riba ni kipato chochote kile cha ziada kutokana na mkopo au mtaji bila kushiriki katika faida au hasara.

Soma Zaidi...
Jinsi ya kuswali swala ya kuoatwa kwa juwa ama swala ya kuoatwa kwa mwezi.

Post hii itakufundisha kuhusu swala ya kupatwa yaani kupatwa kwa juwa na kupatwa kwa mwezi swalat kusuf na swalat khusuf

Soma Zaidi...