Wajibu kwa Jirani
Pamoja na kuwajibika kutekeleza haki mbali mbali kwa wanafamilia tunawajibika vile vile kuwatendea wema majirani zetu wakiwa waislamu au katika dini nyingine. Qur-an inasisitiza:
"... Na wafanyieni ihsani wazazi wawili, jamaa, yatima, maskini najirani waliokaribu najirani walio mbali na rafiki walio ubavuni mwenu..." (4:36)
Mtume wa Allah (s.w) ametuusia juu ya suala Ia kuwafanyia ihsani jirani kwa uzito mkubwa kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:
"Anas(r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Allah amesema: "Yule ambayejirani yake hasalimiki kutokana na ukorofi wake, hataingia peponi." (Muslim)
Aysha na Ibn 'Umar (r. a) wameeleza kuwa Mtume wa Allah amesema: "Jibril hakuacha kunihimiza juu ya jirani mpaka nikahisi kuwa si muda mrefujirani atafanywa kuwa mrithi." (Bukhari na Muslim)
Katika hadith iliyosimuliwa na lbn Mas'ud (r.a) Mtume (s.a.w) amesikika akisisitiza:
"... Naapa kwa yule aliyeshikilia maisha yangu mkononi mwake, mtu hatakuwa Muislamu wa kweli mpaka moyo wake na ulimi wake viukiri Uislamu, na hatakuwa muumini wa kweli mapaka jirani yake asalimike na kero zake." (Ahmad)
Pia Mtume (s.a.w) anatufahamisha kuwa kipimo cha mtu kuwa ni mwema au ni mbaya ni jirani zake kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:
Ibn Mas 'ud (r.a) ameeleza kuwa mtu mmoja alimuuliza Mtume wa Allah: "Ee Mtume wa Allah! Nitatambuaje kuwa nimefanya mazuri na nitajuaje kuwa nimefanya mabaya?" Mtume (s.a.w) alimjibu: "Utakapowasikia majirani zako wakisema umefanya vizuri," basi umefanya vizuri na utakapowasikia wakisema - umefanya vibaya basi umefanya vibaya. Huu ndio ukweli kwa sababu majirani wako karibu sana na wewe na kwa hiyo wanaijua vema tabia yako.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Wajibu wa KufanyakaziUislamu siyo tu unawahimiza watu kufanya kazi na kutokuwa wavivu bali kufanya kazi ni Ibada.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza watu ambao ni halali kuwaoa na wale ambao ni haramu kuwaoa.
Soma Zaidi...Masharti ya Utoaji wa Zakat na Swadaqat Utoaji katika njia ya Allah (s.
Soma Zaidi...Post hii inakwenda kukufundisha maana ya neno talaka katika uislamu kisheria na kilugha.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuhusu zakat al fitiri, kiwango chake, watu wanaostahili kupewa na kutoa, pia umuhimu wake katika jamii.
Soma Zaidi...