Historia na asili ya kuzibiti uzazi na uzazi wa mpango
Historia ya Kampeni ya Kudhibiti Uzazi
Upo ushahidi wa kutosha kuwa watu binafsi katika zama zote wamekuwa wakijitahidi kuzaa watoto wanaopishana miaka iii kuhifadhi afya ya mama na mtoto. Juhudi za serikali huko nyuma (yaani kabla ya kame ya 20) zilikuwa ni kuwashawishi raia kuoana na kuzaana. Lakini kuanzia karne ya 20 serikali zimejiingiza katika kampeni za kuwataka raia wadhibiti kizazi.
Neno kudhibiti uzazi (birth control) ambalo lilibuniwa na Margaret Sanger, mpiganiaji haki za wanawake wa huko Marekani, mwaka 1913 - 1915 lina maana ya njia za kuzuia mimba kwa kumtumia mwanamume au mwanamke, na hivi sasa zinajumuisha njia zote za kuzuia kizazi, ikiwa ni pamoja na kutoa mimba (abortion) au kuviza kizazi (sterilization). Hata hivyo jina Ia kampeni hii limekuwa likibadilika badilika. Katika miaka ya 1930 jina lilikuwa mpango wa familia (family planning) na katika miaka ya 1940 jina likawa mpango wa uzazi (planned parenthood). Baadaye yakazuka majina mengine mengi kama vile kuzuia mimba (controceptive), uzazi wa hiari (voluntary parenthood), kupunguza familia (family limitation), vita dhidi ya mimba (anti conception) na kadhalika.
Kampeni hizo zilipokuja Afrika Mashariki zilipewa majina mbali mbali kama vile uzazi wa majira, mpango wa familia, uzazi na malezi bora, na sasa kampeni hii imepewa jina Ia Elimu ya ngono (sex education) na Tanzania Elimu ya ngono hufundishwa mashuleni kwa jina Ia Elimu ya Afya na Uzazi.
Kwa vile tumemtaja Margaret Sanger kama mwanzilishi wa harakati za "bith control", ni vyema tumzungumzie kwa ufupi ili tupate kuelewa vyema uzito wa neno alilolizua.
Margret Sanger alizaliwa 1879 na kuolewa na William Sanger akiwa na umri kati ya miaka 20 na 25. Alijenga na kuitekeleza kwa vitendo dhana ya "mtu kuwa huru" kutembea na mwanamume yeyote anayemtaka. Alizikuza tamaa zake juu ya ngono na hivyo akawa kahaba mkubwa wa zama zake japo alikuwa kaolewa.
Yaonesha kuwa bwana William, kinyume na tabia ya mkewe, alikuwa ni mtu na heshima zake. Katika hatma ya mambo hakuwa na Ia kufanya ila kumwacha Margaret. Kwani kila alipojaribu kumsema juu ya uzinifu wake, Margret alimshauri mumewe naye azini.
Ndoa yake ya pili iliangukia kwa mume ambaye naye aliikubali dhana angamizi ya mtu kufanya zinaa apendavyo hata akiwa ndani ya ndoa. Na bwana huyu ndiye aliyezipa nguvu harakati za Margret za kampeni za kudhibiti uzazi.
Kiu ya Margret isiyokatika, na ulafi uliopindukia wa ngono, ulimfanya azini na wanaume wanne tofauti wakati yupo katika fungate ya ndoa yake ya pili. Huyo ndiye mwanzilishi wa sera ya kudhibiti uzazi:
Kwa mujibu wa Encyclopedia Britannica (1985) mojawapo ya sababu zilizopelekea kuenea kwa kampeni hii ni manufaa ya faida ya kibiashara iliyotokana na kuuza madawa au vifaa vya kuzuia mimba. Makampuni yanayotengeneza madawa hayo yalijikuta yanaingiza mamilioni ya dola. Hivyo, yakazidi kuitangaza biashara yao. Katika kuzivutia nchi changa, madawa hayo yamekuwa yakitolewa bure. Lakini sasa, baada ya kunogewa na sera hii, inabidi wasake madawa ya kuzuia mimba na magonjwa ya zinaa kwa bei mbaya.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game 👉2 ai web app 👉3 Madrasa kiganjani 👉4 Kitabu cha Afya 👉5 kitabu cha Simulizi 👉6 Dua za Mitume na Manabii
Post zinazofanana:
Swala ya idil fitir na idil haji nanjinsi ya kuziswali
Hapa utajifunza jinsi ya kuswali swala ya idil haji na swala ya idil fitir
Soma Zaidi...Tofauti ya uchumi wa kiislamu na usio wa kiisalmu
Tofauti kati ya mfumo wa uchumi wa Kiislamu na ile ya Kitwaghuti (i) Dhana ya mafanikioKatika mtazamo wa uchumi wa Kiislamu mafanikio yanatazamwa kwa kuzingatia hatima ya ama mtu kupata radhi za Mwenyezi Mungu au kubeba laana ya Mwenyezi Mungu.
Soma Zaidi...Taratibu za eda ya kufiwa katika uislamu
Hapa utajifunza taratibu za kukaa eda kwa mwanamke ambaye amefiwa na mume.
Soma Zaidi...NI ZIPI SWALA ZA SUNNAH: (qabliya (kabliya) na baadiya, tahajudi, tarawehe, qiyamu layl, shukr, istikhara)
Sunnah za SwalaSunnah za Swala Vipengele vya sunnah katika swala ni vile ambavyo mwenye kuswali akivitenda husaidia sana kukuza daraja ya swala yake na kuipa nguvu na msukumo mkubwa wa kuiwezesha kufikia lengo lililokusudiwa kwa urahisi zaidi.
Soma Zaidi...Fadhila za usiku waalylat al qadir
Zijuwe fadhila za usiku wenye cheo kuliko nyusiku ya miezi 1000.
Soma Zaidi...JIFUNZE FIQH
Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka.
Soma Zaidi...