1.
1. Twahara
Maana ya Twahara:
βTwaharaβ ni neno la Kiarabu lenye maana ya usafi wa nje ulioambatana na usafi wa ndani ya mtu. Usafi wa nje unahusiana na usafi wa mwili na nguo na usafi wa ndani unahusiana na utakaso wa nafsi. Mwili na nguo hutwaharika kwa kusafisha kwa kufuata maelekezo
ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Ama nafsi hutwaharika kwa kumtii Allah na Mtume wake kwa kufuata maamrisho yao na kuacha maovu na machafu waliyotukataza. Watu waliotwaharika kwa mtazamo huu hupendeza mbele ya Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo:
β...Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wanaotubu na huwapenda wanaojitakasa (wanaojitwaharisha)β (2:222)
β...Humo wamo watu wanaopenda kujitakasa. Na Mwenyezi Mungu anawapenda wajitakasaoβ. (9:108)
Kwa ujumla tunaweza kusema twahara kwa mtazamo wa Qur-an ni usafi wa nguo zetu, miili yetu, hisia zetu, mawazo yetu na mwenendo na tabia zetu kwa mujibu wa maelekezo ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Pamoja na maana hii ya ujumla, Muislamu aliyetwaharika na kuwa tayari kusimama kwenye swala ni yule aliyeepukana na Najisi na Hadathi. Hivyo tunapojitwaharisha kwa ajili ya swala tunajishughulisha na kuondoa Najisi na Hadath.
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa nitakujulisha kuhusu swala ya kuomba mvia, na taratibu za kuiswali.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...(ii) Hatua za Kuzuia Uzinzi JamiiUislamu pamoja na kutoa mafunzo ya maadii yanayomuwezesha mtu binafsi ajiepushe kwa hiari yake na kitendo kibaya cha zinaa, umechukua hatua mbali mbali ambazo huifanya zinaa isiwe kitendo chepesi katika jamii.
Soma Zaidi...Unadhani mwanamke kupewa mahari kitendo hiki kinaweza kushusha hadhi yake?
Soma Zaidi...Masharti ya Utoaji wa Zakat na Swadaqat Utoaji katika njia ya Allah (s.
Soma Zaidi...