image

Kwa nini lengo la Hija halifikiwi?

Kwa nini lengo la Hija halifikiwi?

Yanayopelekea Lengo la Hijja Kutofikiwa



Tumeona namna Ibada ya Hijja inavyowatayarisha na kuwazoesha Waislamu kuwa Makhalifa wa Mwenyezi Mungu (s.w) hapa ulimwenguni. Kwa maana nyingine inatarajiwa kuwa Waislamu wakitekeleza ibada ya Hijja vilivyo kila mwaka, wataweza kuwa Makhalifa katika ulimwengu na kuisimamisha dini ya Mwenyezi Mungu (s.w) kuwa juu ya dini zote japo makafiri na washirikina watachukia. Mwenyezi Mungu (s.w) anaahidi katika aya mbali mbali za Qur-an kuwa Waislamu wakiamua kusimamisha Dini yake hapa ulimwenguni atawawezesha kuisimamisha. Hebu turejee aya chache zifuatazo:


Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na kufanya vitendo vizuri, kuwa atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyowafanya makhalifa wale waliokuwako kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia dini yao aliyow apendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wale watakaokufuru baada ya hayo, basi hao ndio wavunjao amri zetu. (24:55).


Wan ataka kuzim a nuru ya Mw enyezi Mungu (Uislam u) kw a vinyw a vyao,


na Mwenyezi Mungu atakamilisha Nuru yake ijapokuwa makafiri watachukia. Yeye ndiye aliyemtuma Mtume wake kwa uongofu na kwa dini ya Haki ili kuifanya ishinde dini zote, ijapokuwa watachukia Washirikina. (61:8-9)



Lakini pamoja na ahadi hii na pamoja Waislamu kumininika Makka kwa mamilioni kila mwaka kwa Ibada ya Hija, hatuoni Uislamu kusimama katika jamii ya waislamu ulimwenguni. Miongoni mwa sababu zinazofanya Hija zetu zisitufikishe kwenye lengo lililokusudiwa ni hizi zifu atazo:



(i) Kuhiji kwa Chumo la Haramu
Wengi wahijio wanahiji kwa fedha waliyoichuma kwa njia za haramu. Ilivyo ni kwamba ibada yoyote itakayofanywa kutokana na chumo haramu haitapokelewa mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w). Hili amelidhihirisha Mtume (s.a.w) kwa uwazi kama tunavyojifunza katika Hadithi zifuatazo:



Ibn Umar(r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) amesema:“Swala haikubaliw i bila ya Tahara w ala Sadaqat haikubaliw i kama imetokana na mali iliyochumwa kwa njia za haramu”. (Muslim).



Mtume (s.a.w) amesema: “Kama mtu atanunua nguo kwa dirham 10, na ikawa dirham moja katika hizo 10 zimepatikana kwa njia ya haramu haitakubaliwa swala yake yoyote ile pindi atakapokuw a anasw ali na nguo hiyo ”.



Hadithi hizi zatosha kutuhakikishia kuwa iwapo chumo letu linapatikana kwa njia za haramu, tusahau kabisa kuvuna matunda ya ibada ya Hijja yanayotarajiwa tuyapate.Je, uchumi wetu haukujengwa katika msingi ya riba? Je miongoni mwetu hatupokei rushwa na kuwa tayari kufisidi haki za wengine au kuhujumu uchumi wa Umma? Je, wengi wetu sio waajiriwa katika miradi ya kuzalisha riba kama vile mabenki na mashirika ya bima? Ni vipi sasa tunatarajia kupata matunda ya ibada zetu na ili hali kipato chetu kimetokana na njia hizi haramu? Bila shaka chumo haramu latosha kuwa sababu kubwa inayoifanya ibada ya Hijja inayotekelezwa kila mwaka na mamilioni ya Waislamu isiweze kuwafikisha Waislamu katika kuutawala ulimwengu kama Makhalifa wa Mwenyezi Mungu (s.w) na kuifanya Dini yake kuwa juu ya dini zote pamoja na mbinu na juhudi za Makafiri na Washirikina dhidi ya Uislamu.


Hivyo, ili Waislamu tuweze kupata matunda ya Ibada hii kuu ya Hijja pamoja na ibada nyingine zote, hatuna budi kuusafisha uchumi wa jamii. Lakini tukumbuke kuwa kuusafisha uchumi wa jamii si lele mama, bali inahitajia kuifuma jamii upya kwa kuwaelimisha ‘Waislamu kwausahihi juu ya uislamu kama mfumo kamili wa maisha.



(ii) Kutochunga Miiko ya Hijja



Hijja kama ibada nyingine ina miiko yake ambayo kama haitachungwa vilivyo, mafunzo yanayokusudiwa kutokana na Hijja hayapatikani. Masharti ya Hijja yametolewa kwa muhtasari na aya ifu atayo:


“... Na anayekusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu, wala asibishane ka tika h iy o Hija...” (2:197).
Tunalojifunza katika aya hii ni kwamba, mtu anayekusudia kuhiji ni lazima ajitahidi kuwa mcha-Mungu ambaye hujiepusha kwa moyo mkunjufu na yale yote aliyoyakataza Mwenyezi Mungu (s.w), ambaye hujitahidi kwa jitihada zake zote kufuata inavyostahiki na kwa unyenyekevu maamrisho yote ya Mwenyezi Mungu (s.w), ambaye anajitahidi kwa jitihada zake zote kuwafanyia wema wanaadamu wenzake na ambaye ametubia kwa Mola wake kwa makosa yake na anawaomba msamaha wanaadamu wenzake aliowakosea. Pia tunafahamishwa katika aya hii kuwa, Hajji au Hajjat anatakiwa abakie katika hali hii ya Ucha-Mungu katika safari yote ya Hijja ikiwa ni pamoja na kuchunga kwa ukamilifu miiko ya Ihram.



Wengi wetu wanaohiji hawachungi miiko ya Hijja. Tabia za wengi wanaokwenda kuhiji haina tofauti kabisa na tabia za makafiri na washirikina. Ni mara ngapi tunawaona watu wanaojiita waislamu na wanaokusudia kuhiji lakini hawasimamishi swala, hawatoi Zakat na hawawahurumii Waislamu wenzao hata wale waliokaribu nao na walio majirani zao?Je, hatujaona Waislamu wanaojiandaa kuhiji na huku wanadhulumu haki za watu, wanashirikiana na makafiri na Washirikina katika kuupiga vita Uislamu, wanagombanisha na kuwafitinisha watu na hata waislamu wenzao na wanashiriki katika maovu mbali mbali ikiwa ni pamoja na uchumi haramu. Kama tunashuhudia kuwa huu ndio mwenendo wa wengi wanaohiji na kurudi na majina ya Al-Hajj, vipi tunaitarajia Hijja iwafanye watu hawa Makhalifa wa Mwenyezi Mungu (s.w) hapa ulimwenguni?


Ili Hija zetu zituzalie matunda yanayotarajiwa, hatuna budi kuchunga miiko ya Hijja kwa kujipamba na mwenendo wa Kiislamu tangu katika maandalizi ya Ibada ya Hijja mpaka mwisho wake.



(iii)Kutotekeleza Nguzo za Hija Vilivyo


Ibada ya Hija kama ibada nyingine imejengwa na nguzo zinazoipa sura yake halisi. Endapo nguzo moja katika nguzo za Hijja haitatekelezwa vilivyo, ima kwa kukusudia au kwa kutojua, ibada ya Hijja haitasihi. Kutosihi au kutokubaliwa Ibada ya Hijja mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w) ni sababu tosha ya kufanya ibada ya Hija isiweze kumtayarisha mja kuwa Khalifa wa Mwenyezi Mungu (s.w) hapa ulimwenguni.



Ukweli ni kwamba, wengi wanaokwenda kuhiji kila mwaka hawajui masharti na nguzo za ibada ya Hijja kwa kiasi kwamba wanaitekeleza ibada hiyo visivyo na wanavunja miiko ya Ihram bila ya kujitambua. Wengi wa wanaohiji hutosheka tu na kupata tikiti ya usafiri na gharama nyingine za safari. Kujielimisha juu ya namna ya utekelezaji wa Ibada ya Hijja haimo kabisa katika ratiba ya matayarisho ya safari ya Hija. Je, kama wengi wetu tunaitekeleza ibada ya Hijja ovyo ovyo kwa kutokuwa na ujuzi unaostahiki juu ya ibada hiyo, tunatarajiaje kupata matunda ya Hijja sawa na wale walioitekeleza vilivyo? Si kwa ibadah ya Hijja tu, bali ibada yoyote itakayofanywa kwa ujinga,hatuna budi kufahamu vema kuwa haitampatiamfanyaji matunda yaliyoku sudiwa. Hivyo ili Waislamu wapate matunda ya Hijja zao, hawana budi kujitahidi kujielimisha juu ya ibada ya Hijja kama wanavyojitahidi kutafuta gharama za safari ya Hijja.



(iv)Kutojulikana kwa Lengo la Hijja



Kwa muhtasari tumeona kuwa lengo la Hija ni kuwatayarisha na kuwazoesha Waislamu kuwa Makhalifa wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni kwa kusimamisha na kuipigania Dini ya mwenyezi Mungu (s.w) bega kwa bega mpaka iwe juu ya dini zote japo watachukia makafiri na washirikina.
Je, ni wangapi wanaohiji wakiwa na lengo hili akilini mwao? Ukweli ni kwamba wengi wanaohiji hawana habari hata juu ya lengo la ujumla la maisha yao hapa ulimwenguni.




                   






           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1066


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Simulizi za Hadithi Audio     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    

Post zifazofanana:-

Wanaostahiki kupewa zakat
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

MAFUNZO YA SWALA: NGUZO ZA SWALA, SHARTI ZA SWASL, FADHILA ZA SWALA, HUKUMU YA MWENYE KUACHA SWALA
Soma Zaidi...

Hadhi na Haki za Mwanamke Katika Jamii
Soma Zaidi...

Haki ya kumiliki mali katika uislamu
Soma Zaidi...

Maana ya uadilifu na usawa na tofauti zao
Posti hii itakwenda kukufunza utofauti kati ya uadilifu na usawa Soma Zaidi...

Kuenea kwa dhana ya udhibiti uzazi na uzazi wa mpango
Kustawi kwa Kampeni ya Kudhibiti UzaziMiongoni mwa sababu zilizosaidia kustawi kwa kampeni hii ni matokeo ya mapinduzi ya viwanda (Industrial revolution) ya huko Ulaya. Soma Zaidi...

Madhara ya riba kwenye jamii
Haya ni madhara ya riba katika jamii. Ni kwa namna gani jamii inadhurika kutokana na riba? Soma Zaidi...

haki za mwanamke za kisiasa katika uislamu
Haki ya Kushiriki Katika Siasa. Soma Zaidi...

Funga za kafara, aina zake na sababu za funga hizi za kafara na hukumu zake
Soma Zaidi...

Jinsi ambavyo msafiri anatakiwa aswali akiwa safarini
Postvhiibinakwenda kukufundisha kuhusu swala ya msafiri na jinsi ya kuiswali. Soma Zaidi...

Maswali juu ya haki na uadilifu katika uislamu
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:Dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Funga za suna na funga za kafara na nadhiri: Masharti yake, nguzo zake na wakati wa kutekeleza
Funga za Sunnah. Soma Zaidi...