image

Zijuwe nguzo 17 za swala.

Ili swala itimie utahitajika kutimiza nguzo zake na masharti yake. Hapa utajifunza nguzo 17 za swala.

Nguzo za Swala

Utekelezaji wa nguzo za swala ni hatua ya pili katika harakati za kusimamisha Swala. Baada ya kutekeleza kwa ukamilifu sharti za swala, Muislamu huwa tayari kumkabili Mola wake na kuzungumza naye katika swala.Vipi tuzungumze na Mola wetu katika swala, tumeonyeshwa kinadharia na matendo na Mtume Muhammad (s.a.w) ambaye ametuusia: “Swalini kama mlivyoniona mimi nikiswali”. Tunafahamu Mtume (s.a.w) aliswali vipi kwa kurejea Hadith zifuatazo:

 


Aysha (r.a) amesimulia kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akianza swala kwa takbira na kusoma Qur-an - Alhamdullilaahi Rabil-alamiina (Suratul Fatiha). Alipoinama (kurukuu) hakuwa anaweka kichwa chake juu wala hakuwa anakiinamisha sana bali alikuwa akikiweka katikati ya hali hizo mbili, na alipoinuka kutoka kwenye rukuu hakuwa anakwenda

 

kwenye sijda mpaka asimame kwanza wima na alipoinua kichwa chake kutoka kwenye sijda, hakusujudu mpaka baada ya kukaa wima; na alikuwa akisoma tahiyyatu kila baada ya rakaa mbili, na (katika hiyo tahiyyatu) alikuwa anakaa kwa kuulaza mguu wa kushoto na kuusimamisha wima mguu wa kulia. Alikataza kukaa mkao wa shetani (kunyoosha miguu) na kunyoosha mikono kama mnyama, na alikuwa akifunga (akimaliza) Swala kwa Salaam”. (Muslim)

 


Abu Humid Sayid(r.a) aliwaambia Masw ahaba wa Mtume (s.a.w) alitaka kuwakumbusha jinsi Mtume wa Mwenyezi alivyokuwa akisw ali. Alisema (Abu Humaid) kwamba wakati alipokuwa akisoma takbira Mtume alikuwa akiweka mikono yake mkabala na mabega yake na alipokuw a akirukuu, aliweka viganja vya mikono yake juu ya magoti na kuupinda mgongo wake; wakati alipoinua kichwa (alipoinuka) alijinyoosha (alinyoosha shingo yake) wima mpaka kila kiungo kinarudia nafasi yake; wakati alipokwenda Sijda (aliposujudu) mikono yake ilikuwa kati na kati (haikuwa mbali sana wala haikuwa pamoja), na vidole vyake (ncha za vidole vyake) vya miguu vilielekea (alivielekeza) Ka ’aba, alipokaa baada ya rakaa mbili alikuwa akiukalia mguu wake wa kushoto na kusimamisha mguu wa kulia. Wakati alipokaa katika rakaa ya mwisho aliutanguliza (hakuukalia) mguu w a kushoto na kuusimamisha w a kulia, alikaa kwa makalio. (Bukhari).

 


Abu Hamaid Sayid aliwaambia Maswahaba kumi wa Mtume(s.a.w), kwamba yeye anajua vizuri zaidi jinsi Mtume (s.a.w) alivyokuwa akiswali. Alisema (Abu Hamid) kwamba: Wakati Mtume (s.a.w) aliposimama kuswali, aliinua mikono yake juu mpaka ilipokuwa mkabala na mabega yake. Halafu alisoma takbira na baadaye alisoma Qur-an. Halafu alisoma takbira na kuinua tena mikono yake hadi kufikia mkabala na mabega yake.Halafu aliinama (alirukuu) akiweka viganja vya mikono yake juu ya magoti na kujiweka mwenyewe sawa sawa (bila ya kuinamisha kichwa wala kukiinua juu). Baadaye aliinua kichwa chake (aliinuka kutoka rukuu) na kusema: “Mwenyezi Mungu anamsikia (humsikia) yule anayemsifu ”. Halafu aliinua tena mikono yake hadi kufikia mkabala na mabega yake akiwa wima sawa sawa na kusema:“Mwenyezi Mungu ni mkubwa ”. Baadaye alikw enda (chini alikw enda sijda) akiw eka mikono yake mbali na usawa wake na mwili na kupinda vidole vyake vya miguu. Aliinua kichwa chake na aliukunja mguu wake wa kushoto na kuukalia. Alikaa sawasawa (wima) mpaka kila kiungo cha mwili kimerudia mahali pake, na alikwenda tena sijda na kusema:“Mwenyezi Mungu ni mkubwa ”. Aliinuka (alijiinua) kutoka Sijda na kukalia mguu wake wa kushoto. Alikaa sawa sawa mpaka kila kiungo cha mwili kikarudia nafasi yake (mahali pake). Baadaye alisimama juu (wima) na kufanya yote kama alivyofanya

 

katika rakaa ya kwanza. Mw is ho wa rakaa hizi mbili alisimama na kusoma takbira.ya kwanza na aliinua mikono yake hadi ikawa mkabala na mabega yake kama alivyosoma takbira ya kufungulia swala na baadaye alifanya hivyo hivyo katika sehemu ya swala iliyobakia mpaka kufikia Sijda ambamo mlikuwa na (Taslimu). Aliondoa mguu wake wa kushoto (hakuukalia). Alikaa kwa makalio zaidi upande wa kushoto (alikalia mfupa wa kalio la upande wa kushoto) baadaye alitoa Salaam (Taslim). Maswahaba wote `walikubali kuwa Abu Hamid amesema ukweli. (Abu Daud).

 


Hadithi hizi zinatufahamisha kuwa swala ya Mtume(s.a.w) ambaye ametuamrisha tumuigize ina vipengele vilivyogawanyika katika mafungu makubwa mawili. Nguzo za Swala na Sunnah za Swala.

 


Nguzo za Swala

 


Nguzo za swala ni vile vipengele vya swala ambavyo lazima mtu avitekeleze ndio swala yake iweze kukamilika. Nguzo moja tu ikikosekana swala haisihi (haikamiliki). Hivyo ili mwenye kuswali awe na matarajio ya kupata matunda ya Swala hana budi kutekeleza nguzo zake zote kwa ukamilifu. Zifuatazo ni nguzo za Swala:

 


1. Nia - dhamira moyoni.
2. Takbira ya kuhirimia (au Takbira ya kufungulia Swala).
3. Kusoma suratul-Fatiha.
4.Kurukuu.
5.Kujituliza katika rukuu.
6.Kuitidali (kusimama kutoka katika rukuu).
7.Kujituliza katika itidali.
8.Kusujudu.
9.Kujituliza katika sijda.
10.Kukaa kati ya sijda mbili.
11.Kujituliza katika kikao cha kati ya sijda mbili.
12Kusujudu mara ya pili.
13.Kujituliza katika sijda ya pili.
14.Kukaa Tahiyyatu.
15.Kusoma Tahiyyatu.
16.Kumswalia na kumtakia rehema Mtume (s.a.w) na Waislamu.
17.Kutoa Salaam.
18.Kuswali kwa kufuata utaratibu huu (1 - 17).

 


hizi za swala tunaweza kuzigawanya kwenye makundi
(a)Nia.
(b)Nguzo za matamshi (visomo)
(c)Nguzo za vitendo.
(d)Kufuata utaratibu.

 


Katika nguzo 18, nguzo za matamshi ni hizi tano zifuatazo:
(i)Takbira ya kuhirimia swala.
(ii)Ku soma suratul-Fatiha (Al-hamdu).
(iii)Kusoma Tahiyyatu.
(iv)Kumswalia Mtume.
(v)Kutoa Salaam.

 


Nguzo zote zilizobakia, ukiacha nia na kufuata utaratibu ni nguzo za vitendo.

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1446


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Maana ya mirathi katika uislamu
Post hii itakufundishabkuhusu mirathi ya kiislamu, maana yake. Soma Zaidi...

nini maana ya hadathi na ni zipi aina za hadathi na uchafu katika uislamu
Soma Zaidi...

Kujitwaharisha najisi kubwa najisi ya mbwa na Nguriwe
Soma Zaidi...

Aina ya talaka zisizo rejewa
2. Soma Zaidi...

Jinsi ya kuoga josho la kiislamu ( janaba, hedhi na nifasi)
Post hii inakwenda kukufundisha jinsi ya kuoga josho kisheria. Soma Zaidi...

Maana ya zakat
Nguzo za uislamu,kutoa zakat na sadaqat (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Sifa za kuwa maamuma kwenye swala na namna ya kumfuata imamu
Post hii inakwenda kukuelezea sifa za kuwa maamuma na taratibu za kumfuata imamu. Soma Zaidi...

Aina za hijjah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

Yaliyo haramu kwa mwenye hadathi kubwa.
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu mambo ya haramu kwa mwenye hadathi kubwa Soma Zaidi...

Namna lengo la zakat linavyofikiwa
Nguzo za uislamu (EDK form 3:dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...

namna ya kuswali swala ya vitani
Soma Zaidi...

Taratibi za malezi ya watoto wadogo baada ya talaka katika uislamu
Endapo mke na mume wameachana na hali ya kuwa mke ana watoto wachanga. Je uislamu unasemaje kuhusu taratibu za malezi? Soma Zaidi...