Vituo vya kunuia hijjah au umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
- Vituo vya Kunuia Hijja au Umrah.
- Miiqaat, ni vituo vya kunuia Hijjah na Umrah.
- Vituo vitano alivyoviweka Mtume (s.a.w) ni;
- Zul-Hulaifa (Bir-‘Ali).
- Ni cha watu watokao Madinah, kiko kilometa 450 kutoka Makkah.
- Juhfah (Rabigh).
- Ni cha watu watokao Misri na Syria, kiko kilometa 187 kaskazini-magharibi ya Makkah.
- Qurnul-Manaazil (Sail).
- Ni kituo cha watu watokao Najd, kiko kilometa 94 mashariki ya Makkah.
- Makkah.
- Ni kituo cha wakazi wa Makkah na wale wanao nuia Hija mwezi 8, Dhul-Hijah.
- Yalamlam.
- Ni kituo cha watu watokao Yemen, Afrika Mashaiki na Afrika Kusini, kiko kilometa 54 kusini-magharibi ya Makkah.
- Dhaaru-Iraq.
- Ni kituo cha watu kutoka Iraq, Iran, n.k., alichokiweka Khalifah Umar Ibn Khatwaab (r.a) wakati wa ukhalifah wake.
- Kiko kilometa 94 kaskazini –mashariki ya Makkah.
- Jiddah.
- Ni kituo cha wasafiri wa ndege, kiko kilometa 72 kusini ya Makkah.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 ai web app 👉4 Kitau cha Fiqh 👉5 web hosting 👉6 Bongolite - Game zone - Play free game
Post zinazofanana:
haki ya kutaliki: kuacha na kuachwa katika ndoa ya kiislamu
Haki ya KutalikiKatika jamii nyingi za kjahili haki ya kutoa talaka iko kwa mwanamume tu na mwanamke hana haki yoyote ya kumtaliki mumee.
Soma Zaidi...Dhamana ya Kuchunga Ahadi Katika Uislamu
Kuchunga au kutekeleza ahadi ni miongoni mwa vipengele muhimu vya tabia ya muumini wa kweli.
Soma Zaidi...Ufumbuzi wa tatizo la riba.
Uislamu ndio dini pekee ambayo inatoa ufumbuzi juu ya suala la riba.
Soma Zaidi...Sanda ya mtoto
Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...