Aina za swala..
Nguzo za uislamu,aina za swala (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
- Aina za Swala za Sunnah.
Rejea Kitabu cha 1, EDK, Shule za Sekondari, Uk. 150-165.
Swala za Sunnah ni nyingi, tutaangalia baadhi tu kama ifuatavyo:
- Swala ya Maamkizi ya Msikiti.
- Huswaliwa rakaa mbili muda wowote mara tu muislamu aingiapo msikitini kabla ya kukaa.
- Swala za Qabiliyyah na Ba’adiyyah.
- Hizi huswaliwa kabla (Qabiliyyah) na Baada (Ba’adiyyah) ya swala za Faradh.
- Ziko aina mbili; ‘Mu’akkadah’ (zilizokokotezwa) na ‘Ghairu Mu’akkadah’ (Hazikukokotezwa).
Rejea Kitabu cha 1, EDK, Shule za Sekondari, Uk. 152.
- Swala ya Witiri.
- Huswaliwa rakaa kwa idadi ya witiri; 1, 3, 5, 7, 9 na 11 katika theluthi ya mwisho wa usiku au mara tu baada ya swala ya Ishaa.
- Witiri imekokotezwa mwisho wa usiku zaidi na huambatanishwa kwa dua ya Qunuti katika rakaa ya mwisho.
- Swala ya Tahajjud (Qiyaamul-layl).
- Huswaliwa rakaa 8 usiku wa manane kwa rakaa mbili mbili na kumalia 3 za witiri na kutimia rakaa 11.
- Huswaliwa kwa kisimamo na kisomo kirefu cha Qur’an.
Rejea Qur’an (17:79), (25:64), (39:9) na (73:1-4).
- Swala ya Tarawehe (Qiyaamu Ramadhan).
- Ni swala ya kisimamo na Kisomo kirefu cha Qur’an, Juzuu 1 kila siku inayoswaliwa mwezi wa Ramadhani tu baada ya Ishaa au kabla ya swala ya Alfajir.
- Kuna hitilafu kwa idadi ya rakaa, kauli zinasema ni rakaa 8, 11, 20, 36, n.k.lakini yenye nguvu ni rakaa 8 na 3 za witiri na kuwa jumla rakaa 11.
- Swala ya Idil-Fitr na Al-Udhuhaa.
- Zote huswaliwa rakaa mbili, Idil-Fitr huswaliwa mwezi 1 Shawwal baada ya kumalizika funga ya mwezi wa Ramadhani.
- Idil-Al-Udhuhaa huswaliwa mwezi 10 Dhul-Hija baada ya kukamilika ibada ya Hija kila mwaka.
- Swalatudh-Dhuhaa.
- Huswaliwa kila siku baada ya Jua kupanda kiasi cha mita tatu kutoka kuchomoza kwake.
- Huswaliwa rakaa mbili mbili hadi kutimia nane, lakini kwa uchache huswaliwa rakaa mbili.
- Swalatul-Istikharah.
- Ni swala inayoswaliwa muda wowote kwa ajili ya kuomba msaada na mwongozo kwa Allah juu ya uamuzi au utatuzi wa jambo lolote zuri.
- Swala ya Kukidhi Haja.
- Ni swala inayoswaliwa muda wowote kwa ajili ya kuomba msaada au utatuzi wa tatizo lililotokea au unalohitajia.
- Swalatut – Tawbah.
- Huswaliwa rakaa mbili muda wowote kwa ajili ya kutubia baada ya muislamu kufanya kosa.
Rejea Qur’an (3:135-136).
- Swala ya Kupatwa kwa Jua na Mwezi.
- Huswaliwa kwa jamaa, rakaa mbili, rukuu mbili kwa kila rakaa moja. Huswaliwa kwa kisimamo na kisomo kirefu mpaka Kupatwa kuondoke.
- Swala ya Kuomba (Swalatul-Istisqaa).
- Ni swala ya rakaa mbili kwa ajili ya kuomba mvua baada ya kuzidi dhiki na ukame, kwa jamaa na uwanjani.
- Swala hii ina khutuba mbili na takbira kama inavyoswaliwa swala za Idi.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉3 Kitau cha Fiqh 👉4 Dua za Mitume na Manabii 👉5 web hosting 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Hadathi ya kati na kati
Posti hiibinakwenda kukufundisha kuhusu hadathi ya kati na kati.
Soma Zaidi...Tofauti kati ya hijjah na umrah
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Maswali juu ya haki na uadilifu katika uislamu
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...