Udhaifu wa Hoja za Kudhibiti Uzazi:Hoja nyingi zinazotolewa kuunga mkono udhibiti wa uzazi zimejengwa juu ya hali na mazingira ya maisha yaliyoletwa na utamaduni na maendeleo ya nchi za Ulaya na Marekani.
Udhaifu wa Hoja za Kudhibiti Uzazi:
Hoja nyingi zinazotolewa kuunga mkono udhibiti wa uzazi zimejengwa juu ya hali na mazingira ya maisha yaliyoletwa na utamaduni na maendeleo ya nchi za Ulaya na Marekani. Wale wanaoiunga mkono kampeni hii wanaamini kuwa, mila na mwenendo wa jamii za Ulaya ndio kiigizo cha watu wengine wote duniani. Historia ya maendeleo ya binaadamu inatazamwa kana kwamba inafuata mstari ulionyooka. Watu wanatoka katika hali duni na kuelekea katika hali ya maendeleo. Na wanaoongoza maendeleo hayo ni watu wa Ulaya na Marekani. Kutokana na mwelekeo huo mtindo wa maisha wa huko Ulaya, mila za huko na taratibu za kiuchumi za huko zinaonekana kuwa hazitakiwi kubadilika.
Kinachotakiwa kubadilika ni mila na desturi zilizo kinyume na zile za Ulaya. Matokeo ya mwelekeo huu ni kuwa watu hutafuta ufumbuzi wa matatizo yao kwa kutazama Ulaya hata kama mila za Ulaya ndizo zilizo yaleta matatizo hayo. Kama nchi za Afrika hazitaamua kuchukua mwelekeo tofauti kabisa katika kukabiliana na matatizo, zitaendelea kuwa wafungwa wa Ulaya kila uchao. Hilo linalodhaniwa kuwa ni tatizo Ia ongezeko Ia watu ni zao Ia mfumo wa kiuchumi na kijamii wa nchi za Ulaya. Ufumbuzi hauwezi kupatikana kwa kampeni za kudhibiti uzazi wakati uchumi wa nchi hizo unadhibitiwa na watu wengine.
Watetezi wa kudhibiti uzazi (birth control) na kampeni za nyota ya kijani, hawataweza kuyaona makosa ya mwelekeo wao hadi watakapokuwa tayari kuitazama upya misingi ya udhibiti wa uzazi. Kinachohitajika siyo kukata matawi bali kung'oa mti mzima unaozalisha matunda haya machungu.
Hoja ya Uhaba wa Rasilimali za Kiuchumi
Hoja yao maarufu kuliko zote kama tulivyoona ni juu ya uchumi. Hudaiwa kuwa sehemu ya kuishi katika ardhi ma ukomo na kwamba rasilimali za kiuchumi pia zina ukomo. Lakini hudaiwa kwamba uwezo wa mwanaadamu wa kuzaliana ni mkubwa ambapo ardhi itajaa na chakula kitakosekana cha kuwatosheleza watu wote. Katika Encyclopaedia Britanica (1985) kwa mfano, inakadiriwa kuwa hadi mwisho wa karne hii ya ishirini idadi ya watu imekuwa ni zaidi ya bilioni sita (6,000,000,000). Hivyo, basi ili kujikinga na baa hilo watu hawana budi kudhibiti kizazi. Kwa mujibu wa Bwana Malthus na mwenzake Francis Place iwapo juhudi za kudhibiti uzazi (birth control) hazitatiliwa mkazo basi uwiano kati ya watu na mahitaji muhimu kama chakula utakuwa ni 4096:13 katika karne tatu na baada ya kame 20 uhusiano huo hautakuwapo kabisa. Yaani hakutakuwepo na uhai kabisa.
Hoja hii ya kwamba binaadamu wanaongezeka sana, mara mbili kila baada ya robo karne, haina msingi kwa sababu si ya kweli. Lau madai hayo yangekuwa ya kweli basi leo kusingekuwa na binaadamu ardhini. Kwa mujibu wa utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa katika jarida liitwalo "National geographic" (Vol. 154 No.6) Ia huko Marekani, yamepatikana maandishi huko Syria yanayothibitisha kuwa miaka 3,000 kabla ya kuzaliwa kwa Nabii Issa (a.s) kulikuwa na dola nyingi sana zilizofikia kiwango kikubwa sana cha maendeleo. Dola hizo pia zilikuwa na watu wengi sana. Dola ya Ebla imetaja miji 5,000 waliyokuwa wakifanya nayo biashara. Mmoja kati ya miji hiyo ni Iram uliotajwa katika Qur-an 89:7. Na maandishi hayo yalikuwa katika makao ya Ikulu ya dola ya Ebla. Kama madai ya akina Malthus yangekuwa kweli basi hata Yesu asingezaliwa kwani zilikuwa zimekwishapita karne zaidi ya 30
Wazo kwamba mahitaji muhimu hayatatosha ni dhaifu kwa sababu rasilimali zote ambazo mwanaadamu anazihitaji zilikuwepo tokea dunia ilipoumbwa kwa ajili ya matumizi ya binaadamu wa zama zote. Rasilimali hizi zinafahamika kwa binaadamu kutokana na maendeleo ya kisayansi na teknolojia. Mfano watu wa zama za kale hawakuwa na habari kuhusu mafuta ya petroli yanavyoweza kuwa muhimu katika maendeleo ya binaadamu japo yalikuwepo na japo Wasumeria walifahamu juu ya kuwepo kwa mafuta hayo. Mifano ya ama hii ni mingi sana. Hii ma maana kuwa kutokana na upeo wa sasa wa Elimu watu wanaweza kudhani kuwa vizazi vijavyo havitaweza kuishi kwa sababu ya uhaba wa mahitaji muhimu. Ni muhimu kutambua kuwa watu wakiongezeka upeo wa binaadamu wa kuzalisha mali, vyakula n.k., nao pia huongezeka.
Historia ya hivi karibuni imeonesha kuwa kuongezeka kwa binadamu hakusababishi uhaba wa mahitaji muhimu. Mwaka 1880 idadi ya Wajerumani ilikuwa milioni 45 hivi. Wakati huo kulikuwa na uhaba wa chakula ukilinganisha na hivi sasa ambapo idadi yao ni zaidi ya milioni 68, na wanakula na kusaza. Uholanzi na Uingereza pia ni mifano mizuri katika kuelezea ukweli huu. Isitoshe zaidi ya binaadamu kuna viumbe wengi sana juu ya ardhi hii yenye nafasi yenye ukomo. Na kila kiumbe kinao uwezo mkubwa sana wa kuzaliana kiasi ambacho kama pasingekuwepo na kanuni za kimaumbile (natural laws) za kudhibiti uwezo huo, basi ama moja tu ya viumbe ingeweza kuijaza ardhi yote katika kipindi kifupi mno.
Kwa mfano, jamii ya aina fulani ya mti ijulikanayo kama Sysmbrium Sophia, ma uwezo wa kutoa mbegu kiasi cha robo tatu milioni. Inakadiriwa kuwa kama mbegu zote za mti mmoja tu zitaota, katika kipindi cha miaka mitatu tu mti huo utaijaza ardhi yote na pasiwe na nafasi ya kiumbe kingine chochote. Aina ya samaki ajulikanaye kama 'Star' fish hutaga mayai mia mbili milioni kwa mara moja. Kama yote yataaanguliwa basi baada ya vizazi vichache tu samaki huyo mmoja atazijaza bahari za dunia nzima na isiwepo hata nafasi ya tone moja Ia maji.
Hali kadhalika ukimwangalia binaadamu, manii anayotoa mara moja yanatosha kuwapa mimba wanawake milioni mia tatu hadi mia nne. Hivyo kama uwezo wa mwanamume mmoja ungeruhusiwa kufanyakazi yake basi ingehitajia miaka michache tu kwa mwan aume huyo kuijaza dunia yote kwa watoto wake tu na kusiwe na nafasi ya watu wengine achilia mbali viumbe wengine. Ni nani anayedhibiti na kuweka uwiano kwa viumbe wote hawa?
Tatizo halijawahi kuwa uhaba wa rasilimali za kuwakimu watu, bali kasoro za kibiashara, ugawaji na usambzaji wa rasilimali hizo. Kwa mfano inafahamika kuwa asilimia 10 tu ya rasilimali zinazotumiwa kutengeneza silaha ulimwenguni zinatosha kufutilia mbali njaa na maradhi dunia nzima. Tukizingatia uwiano kati ya idadi ya watu na chakula duniani, tutaona wazi kuwa tatizo siyo uwingi wa watu. Mfano kwa upande mmoja mwaka 1982 Uingereza ilikuwa na watu 583 kwa kila maui mraba lakini ilikuwa haina tishio Ia njaa. Kadhalika Uholanzi ilikuwa na watu 1,117 katika maili mraba, lakini vile vile haikuwa natishio Ia njaa. Ambapo Brazil iliyokuwa na watu 38 na Bolivia watu 12 kwa kila maili mraba, zote zilikuwa na tishio Ia njaa. Tatizo hapa ni suala zima Ia uzalishaji mali na sio idadi ya watu katika mji. Ni mara ngapi tumeshuhudia mamilioni ya tani za vyakula yakiunguzwa moto au kumwagwa baharini katika nchi tajiri kama vile Marekani na hapo hapo mamilioni ya watu wanakufa njaa katika nchi masikini?
Tatizo Ia Vifo na Maradhi
Watetezi wa kampeni ya kudhibiti uzazi (birth control) wanakiri kuwa maumbile (nature) hudhibiti kukua kwa idadi ya viumbe. Lakini wanasema maumbile hufanya kazi hii kwa njia ya vifo na maangamizi na hivyo kusababisha machungu na mateso ya kimwili na kisaikolojia. Kwa nini binaaadamu wasitafute njia nzuri zaidi ya kujipunguza wenyewe? Yaani wajipunguze kwa njia ya kudhibiti uzazi (birth control) badala ya kungojea majanga kama njaa au mafuriko yaje kupunguza idadi ya watu.
Hoja hii pia mao udhaifu mkubwa. Ukweli ni kuwa uhai na kifo havipo katika milki ya binaadamu. Hadhari yoyote utakayoichukua, kifo kinabakia kuwa ni tatizo lisilo na ufumbuzi. Swali ni je, ni hadhari gani ambayo binaadamu anaweza kuichukua dhidi ya tetemeko Ia ardhi, kimbunga (au tufani), mafuriko, maradhi mabaya n.k.? Je, binaadamu amefikia muafaka na Mwenyezi Mungu (au maumbile kama wanavyodai) kuwa njia nyingine zote za kuwafisha watu zitasimamishwa endapo taifa litazindua mpango wa kupunguza watu kwa njia ya kudhibiti uzazi? Je wametafakari juu ya msiba unaowasubiri endapo watasimamisha kuzaliana na wakati huo huo kifo kikaendelea kuchukua ushuru mkubwa wa roho za watu kwa kupitia mabalaa, kama mvua za elnino na mafuriko, tufani, matetemeko ya ardhi na volkeno, maradhi, vita, kuzama kwa meli, kupinduka kwa magari, treni, kuanguka kwa ndge n.k.? Na hii ni mbali na mwenendo wa kawaida wa kifo ambao hapana njia ya kuukwepa. Ni jambo Ia kushangaza kuwa wataalamu hao wanashindwa kufanya mahesabu rahisi kama haya! Kama kuna kupungua kwa watu daima pasipokuwa na njia mahsusi za kuleta ongezeko, ni athari gani zitafuata?
Katika nchi zilizoendelea vifo vinavyosababishwa na maradhi ya zinaa ni vingi kuliko vifo vinavyosababishwa na vita. Usisahau vimbunga vya AIDS, Ebola, TB, Tauni n.k. Je, huku ndiko kushinda au kuepuka kifo? Kama sivyo, je watu hawatakuwa wanaunguza mshumaa kutoka pande mbili - kwa upande mmoja idadi ya watu itapungua kutokana na sababu tusizoweza kuzizuia (natural causes) na kwa upande mwingine kupunguza watu kwa kudhibiti uzazi?
Ili mtu awe katika nafasi nzuri ya kudai udhibiti wa uzazi (birth control) lazima awe na Elimu juu ya mambo kadhaa:
- Ajue idadi ya viumbe wote duniani waliotakiwa kuishi hapa duniani na kati ya hao ni wangapi wamekwishaishi na wangapi bado.
- Ajue idadi hasa ya chakula kiasi gani na chakula hicho huongezeka au hupungua vipi?
- Ajue pia ni kiasi gani cha viumbe watakaokufa kwa njaa, mafuriko, maradhi, vita na kadhalika na watakufa lini ili aweze kulinganisha na kiasi cha chakula kitakachokuwepo na mahitaji mengine.
- Ajue pia namna ambavyo sera yake ya kudhibiti uzazi itakavyohakikisha kuwa kila siku idadi ya watu wanaokufa na kuzaliwa haizidi wala kupungua kulinganisha na rasilimali zilizopo.
Kujiingiza katika kampeni za kudhibiti kizazi (birthcontrol) na nyota ya kijani bila ya kuwa na takwimu sahihi juu ya mambo yote hayo ni kujiingiza katika mchezo wa pata-potea.
Hoja ya Ugumu wa Malezi
Hoja hutolewa kuwa wazazi walio na kipato kidogo watashindwa kulea watoto wengi. Watashindwa kuwapa Elimu nzuri, kuwalea katika hali nzuri ya kimaisha na kuwapa msingi wa kutosha wa kuanzia maisha. Isitoshe wanaweza kupata utapiamlo (malnutrition) na hata kufa wakati wa utoto wao.
Hoja hii yaweza kuwavutia watu wengi lakini nayo pia ni dhaifu. Kwanza, "Elimu bora", "hali ya maisha" n.k. ni misemo tata (vague) isiyokuwa na tafsiri moja maalum. Kila mtu anayo namna yake ya kuyaangalia mambo. Lipo kosa linalofanyika Ia mtu kuacha kutazama hali yake na mazingira yake na kuangalia hali ya maisha ya mahali pengine na hivyo kuanza jitihada za kujaribu kuwakuta waliotangulia. Raia wa nchi za Kiafrika kwa mfano, wanahimizwa wakimbie kwa dhana kuwa wale waliombele wanatembea. Kinachosahauliwa ni kwamba utaratibu mbaya wa uchumi na biashara uliopo leo duniani ndio unaodumisha utajiri wakupindukia wa nchi zilizoendelea na ufakiri wa kupindukia kwa nchi maskini. Hivyo chini ya utaratibu huu jitihada za kuiga 'maisha mazuri' kwa kiigizo cha Ulaya na Marekani ni ndoto. Na watu wenye fikra hizo huepa kulea japo mtoto mmoja kwa kuhofia kuwa atakosa kupata maisha bora. Msimamo huu huwafanya watu wawanie kupata starehe za hali ya juu. Huishia kuleta ufisadi katika ardhi au kujinyonga wakishindwa kufikia lengo hilo.
Fikra kuwa watu wasizae watoto hadi wahakikishe kuwa watoto hao hawatapata matatizo yoyote kwakuwa kila kitu kitakuwa kimeandaliwa pia ni mwelekeo potofu. Ni hatari kwa ustawi wa taifa ikiwa kizazi chao kitalelewa katika starehe na anasa ya mali wasioichuma na iwapo hawatakabiliwa na matatizo na misukosuko ya maisha. Hali hiyo itawafanya wasione haja ya kujitahidi na kupambana na matatizo.
Matatizo ni tanuri linalomfunza na kumpevua mtu ajue namna ya kukabiliana na hali mbali mbali za maisha. Hivyo uvumilivu, subira, ukakamavu, na ujasiri ni mambo yatakayoijenga tabia yake na kumfanya awe mtu mwenye manufaa katika jamii. Hakuna shule au chuo kinachoweza kutoa mafunzo haya, wala mtoto hawezi kupata mafunzo hayo kwa kuishi katika fahari na anasa tu. Misukosuko ni kiwanda kinachotenganisha nafaka na makapi. Mtu anakutana na misiba ili akabiliane nayo kiume, matatizo huja ili yamchochee kufanya jitihada zaidi ili ayatatue. Mambo magumu husafisha udhaifu wa binaadamu na kuamsha vipawa vyake na kuvistawisha na hivyo kuleta maendeleo. Wale wanaoweza kupita katika tanuri hilo kwa ujasiri ndio wanaoweza kutegemewa katika jamii. Katika historia ya binaaadamu karibu asilimia 90 ya watu mashahuri waliozisaidia jamii zao walizaliwa katika familia maskini na mazingira magumu.
Hivyo fikra ya kutaka watoto wazaliwe chambilecho Waingereza wamesema na "vijiko vya fedha midomoni mwao"; wasome shule bora kabisa, walale katika majumba ya fahari wakati wanasoma na wanapoanza maisha wawe wameandaliwa kila kitu ni ya hatari. Itatuletea kizazi cha watu wapendao anasa na ambao wataona taabu kujitoa muhanga kwa lolote, na wataepuka kubeba dhamana nzito. Moto utakuwa umezaa jivu.
Hoja ya Ubora na siyo Uwingi wa Watu
Yasemekana kilicho muhimu siyo uwingi bali ubora wa watu. Hali hii imesimama juu ya dhana kuwa kama watazaliwa watoto wawili au mmoja basi watakuwa na akili nzuri, afya na uwezomkubwa wa kuzalisha. Lakini kama watazaliwa watoto wengi watakuwa dhaifu, wagonjwa, wajinga na wasiofaa kwa lolote.
Hoja hii haina msingi wowote na haiwezi kuthibitishwa kwa uzoefu wala majaribio. Mtu aweza kuzaa mtoto mmoja tu na akawa juha au mwenye afya dhaifu sana. Tuchukuwe mfano wa mabwana wawili. Mmoja amejaaliwa kuzaa watoto wawili tu, alijitahidi kuwalea watoto hawa kama yai. Aliwahangaikia kwa kila kitu mpaka wakawa watu Wazima. Matarajio ya bwana huyu kwa vijana wake ni kwamba kutokana na malezi ya starehe aliyowapa, watakapokuwa watu Wazima watatoa mchango wao kuwasaidia wazazi wao, familia zao na jamii kwa ujumla.
Kinyume na matarajio haya vijana hawa waliishi kwenye ulevi, ukahaba, na kila ama ya anasa yenye kumwangamiza mwanaadamu! Bwana huyu akabakia katika hali ya ukiwa na kukata tamaa huku uzee unamuandama. Bwana wa pili amejaaliwa kuzaa watoto kumi. Hakuwa na kipato kikubwa kiuchumi hivyo alihangaika sana katika kuwalea watoto wake. Alimfanya kila mtoto atoe mchango wake kwa kadri ya umri wake kuongeza kipato cha familia yao. Vijana wawili kati ya vijana wake waliangukia kutokuwa na manufaa yoyote kwa wao wenyewe na kwa jamii kwa ujumla kama wale wa bwana wa mwanzo.
Vijana wake wanane waliobakia, walibakia kuwa watu wa maana kama walivyolelewa, wakawa ni wenye manufaa kwa wazazi wao na familia zao na wakawa ni wenye kutoa mchango mkubwa katika kuiendeleza jamii. Kutokana na mfano huu, huoni hatari ya kudhibiti uzazi? Utahakikishaje kuwa hao wachache watakaozaliwa kuwa ndio watakaokuwa bora? Tusiufikirie ubora wa mwanaadamu kama ule wa ng'ombe anayenenepeshwa kwa ajili ya nyama, au kutoa maziwa mengi! Ubora wa binaadamu uko katika utu wake. Kumlea mtoto katika starehe, hakuna uthibitisho wowote wa kuukuza utu wake, bali kuna uwezekano mkubwa wa kuudunisha. Hatuna budi kukumbuka kuwa msingi wa maendeleo ya jamii sio vitu bali ni utu.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 472
Sponsored links
๐1 kitabu cha Simulizi
๐2 Kitabu cha Afya
๐3 Kitau cha Fiqh
๐4 Simulizi za Hadithi Audio
๐5 Madrasa kiganjani
๐6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Maana ya sadaqat
Nguzo za imani, maana ya sadaqat
(EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...
Nguzo za uislamu
Katika kipengele hiki tutajifunza nguzo za uislamu.aina tano za nguzo za uislamu,dhana ya nguzo za uislamu,lengo na umuhimu wa nguzo za uislamu Soma Zaidi...
Nguzo za kufunga ramadhani
Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
Mgawanyo wa mirathi kutoka kwenye Quran
Quran imegawanya mirathi katika haki. Mgawanyo huu ndio unaotakiwa utumike na si vinhinevyo. Soma Zaidi...
Ni yapi masharti ya Udhu na kujitwaharisha
Soma Zaidi...
Maneno mazuri mbele ya mwenyezi Mungu
kuna adhkari nyingi sana ambazo Mtume wa Allah ametutaka tuwe tunadumu nazo. lajkini kuna adhkari ambayo imekusanya maneno matukufu na yanayopendwa sana na Allah. Soma Zaidi...
Maana ya swala
Maana ya Swala Maana ya Swala kilugha(a) Kilugha Katika lugha ya Kiarabu neno ยSwalaatย lina maana ya ยombi au ยdua. Soma Zaidi...
Haki na wajibu wa mke kwa mumewe na familia
Soma Zaidi...
MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA ELIMU
Maana ya elimuElimu ni ujuzi ulioambatanishwa na utendaji. Soma Zaidi...
Swala ya jamaa na taratibu zake
Post hii inakwenda kukufundisha kuhusu swala ya jamaa na taratibu zake. Soma Zaidi...
NAMNA YA KUSWALI
13. Soma Zaidi...
Maana ya Funga ya ramadhani kisheria na Aina za funga
Amesema mtume (s.a.w) kuwa Allah (s.w) amesema: kila amali ya mwanaadamu ni kwa ajili yake isipokuwa funga. Soma Zaidi...