Menu



Namna ya kutekeleza swala ya maiti hatua kwa hatua

Mambo ya faradh kwa maiti ya muislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Utaratibu wa kusimamisha swala ya maiti ni kama ifuatavyo;

  1. Maiti iwekwe mbele.
  2. Imamu asimame katikati ya mwili wa maiti ikiwa maiti ni ya kike, na usawa wa mabega kama maiti ni ya kiume.
  3. Maamuma watasimama kwenye mistari (safu) kwa idadi ya witiri; 1, 3, 5, n.k.
  4. Baada ya hapo swala itaanza na kuendelea kama ifuatavyo:
    1. Nia - ambayo ni kukusudia moyoni.
    2. Kuleta takbira ya kwanza; kwa kusema, “Allaah Akbar”
    3. Imamu na maamuma watasoma suratul-Faatiha – kimya kimya.
    4. Imamu ataleta Takbira ya Pili kisha maamuma – kimya kimya kwa maamuma na si lazima kuinua mikono wao. 
    5. Kumswalia Mtume (s.a.w) kama ilivyo katika Tahiyyatu, wote – kimya kimya.
    6. Imamu ataleta takbira ya Tatu kisha maamuma- kama walivyofanya awali.
    7. Wote kumuombea maiti dua kimya kimya, ikiwemo: 

“Allaahumma ghfir lihayyinaa wamaayyitinaa washaahidinaa waghaaibinaa waswaaghirinaa wakaabirinaa wadhakirnaa waunthaanaa. Allaahumma man ahyaytahuu minnaa faahyi ‘alal Islaam. Waman tawaffaytahuu minnaa tawaffahuu ‘alal Imaani. Allaahumma laa tahirimnaa ajirahuu walaa taftinaa ba’adahuu”

    Tafsiri:

“Ewe Allah tusamehe sisi, na maiti wetu, na mashahidi, na wasiokuwepo miongoni wetu, vijana wadogo miongoni mwetu na wakubwa miongoni mwetu, wanamume wetu, na wanawake wetu. Ewe Allah, yeyote yule miongoni mwetu utakayemewezesha kuishi, mjaalie aishi katika Kiislamu na yeyote miongoni mwetu utakayemfisha, mfishe katika Imani (ya Kiislamu). Ewe Allah, usitukatishe ujira kutoka kwake na wala usitufitinishe baada yake.” 

 

            -   Au kwa kifupi tuweza kumuombea maiti kama ifuatavyo;

                “Allaahumma ghfir lahuu warhamhuu wa-afihii wa-afu-anhu”

            Tafsiri:

                “Ewe Allah, Mghufirilie na Umrehemu”.

 

  1. Imamu ataleta Takbira ya nne na maamuma kufuatihia kama awali.
  2. Wote watawaombea waislamu dua – (pia si lazima kuleta dua hii).

Rejea Qur’an (59:10).

 

  1. Imamu kutoa salaam na maamuma kufuatishia bila kutoa sauti kama ilivyo kwenye swala ya kawaida kwa kusema; 

        “Assalaamu ‘alaykum Warahmatullaah (Wabarakaatuh)”

    Tafsiri:

        “Amani iwe juu yenu na Rehema za Allah na Baraka zake”.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Fiqh Main: Post File: Download PDF Views 1171

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

Kwa nini imefaradhishwa kufunga mwezi wa Ramadhani

Unaweza kijiuliza ni kwa nini hasa kimepelekea kufaradhishwa kufunga mwezi wa Ramadhani.

Soma Zaidi...
Kiasi cha mahari kilicho bora kinachofaaa katika uislamu

Uislamu haukuwekabkiwango maalumu cha mahari. Mwanamke anaweza tajabkiasi atakacho. Ila vyema kuzingatia haya wakayi wa kutamka mahari yako.

Soma Zaidi...