Fahamu kuhusu vitamini D na kazi zake mwilini
Hapa utajifunza kuusu vitamini D, kazi zake, upungufu wake na chanzo cha kupata vitamini D.

VITAMINI D NA FAIDA ZAKE MWILINI
Vitamini D ni vitamini inayosaidia miili yetu iweze kuvyonza madini ya calcium, magnesium na phosphate. Vitamini D hutengenezwa chini ya ngozi kwa kutumia mwanga wa jua. Vitamini D ipo katika makundi makuu mawili nayo ni vitamini D2 na vitamini D3. Vitamini vipo katiaka makundi mengi kuna vitamini A, B, C, D, E na K . katika makala hii tutakwenda kuona zaidi kuhusu vitamini D, namna ambavyo vitamini D hutengenezwa mwilini, Je ni zipi kazi za vitamini D, na upungufu wake unasababisha athari gani mwilini?.
YALIYOMO:
1.Maana ya vitamini D
2.Makundi ya vitamini D
3.Kazi za vitamini D
4.Chanzo cha votamini D
5.Upungufu wa vitamini D
Maana ya Vitamini D
Vitamini D ni matika fat soluble vitamin ambayo imetokana compound za cholesterol. Vitamini D vimegunduliwa mwaka 1922 na Mwanasayansi anayefahamika kwa jina Elmer McCollum. Historia ya uchunguzi huu wa vitamini D ulianzia toka mwaka 1914 wakati Elmer McCollum na Marguerite Davis walipogundua vitamini A
Vitamini hivi vimeitwa D kwa sababu ndio vitamini vya nne kugundulika toka A, B, C na sasa ni vitamini D. ugunduzi wa vitamini D ulianzia kwenye mbwa mgonjwa ambaye alikuwa ana matege. Baadaye ikajulikana kuwa mbwa aliweza kupona matege kwa sababu ya chembechembe amazo baadaye ndiyo zikaitwa vitamini D.
Makundi ya vitamini D
Kama ilivyokuwa vitamini K na vitamini B zina makundi mengi. Basi hata hivyo vitamini D vimegawanyika katika makundi kadhaa, makuu katika kundi hilo ni vitamini D2 na bitamini D3. makundi haya mawili kwa pamoja ndiyo hufahamka kama vitamini D.
Vitamini D1 na vitamini D2 kwa pamoja pia huitwa calciferol. Vitamini D2 vimeweza kupewa sifa yake kikemikali mwa ka 1931 na vitamini D3 vimeweza kupewa sifa yake kikemikali mwaka 1935.
Kazi za vitamini D
Katika miili yetu vitamini D ina kazi kuu ya kufanya metabolism ya madini ya calcium. Kwa lugha nyepesi ni kuhakikisha kuwa unyonzwaji wa madini ya chumvi ambayo ni calcium, magnesium na phosphate unafanyika vyema ndani ya utumbo mdogo.
Faida za vitamini D:
1.Husaidia kufyonza mwili kufuonza madini ya calcium
2.Husaidia kuboresha afya ya mifupa
3.Husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata saratani
4.Husaidia kuboresha mfumo wa faya
5.Kupunguza uzito na kitambi
Chanzo cha vitamini D
Chanzo kikuu cha vitamini D ni mwanga wa jua ambao husaidia katika utengenezwaji wa vitamini D chini ya ngozi. Kama mtu hataweza kupata mwangaza wa jua vyema kuna uwezekano wa kupata upungufu wa vitamini D.
Pia tunaweza kupata vitamini D kutoka katika vyakula na mboga, kama vile:-
1.Uyoga
2.Yai lililopikwa
3.Maini
4.Samaki
Upungufu wa vitamini D
Upungufu wa vitamini D unaweza kusababisha athari kubwa kwenye afya. Miongoni mwa athari hizo ni:-
1.Matege
2.Udhaifu wa mifupa
3.Mifupa kuvunjika kwa urahisi
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina 👉2 web hosting 👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w) 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 ai web app 👉6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Mbinu za kuponyesha majeraha
Posti hii inahusu zaidi mbinu ambazo hutumika kuponyesha majeraha kwa haraka zaidi,tunajua majereha utokana na kupona kwa vile vidonda au kupona kwa sehemu ambayo imekuwa na majeraha kwa hiyo ili kuponyesha majeraha hayo tunapaswa kufanya yafuatayo.
Soma Zaidi...Ratiba ya chanjo ya kifua kikuu
Posti hii inahusu zaidi ratiba ya chanjo ya kuzuia kifua kikuu, hiii ni ratiba ambayo chanjo hii utolewa na ushauri mbalimbali utolewa ili kuweza kufanikisha kazi ya chanjo hii
Soma Zaidi...Msaada kwa wenye tonsils
Posti hii inahusu zaidi msaada kwa wenye tonsils, kwa wale wenye tonsils wanapaswa kufanya yafuatayo ili kuweza kupambana na ugonjwa huu.
Soma Zaidi...Hatua za kufuata baada ya kuhisi kuwa umeambukizwa na virusi vya HIV
Posti hii inahusu zaidi hatua za kufuata unapohisi umeambukizwa na virus vya ukimwi. Kwa sababu watu wengi wanakuwa na kiwewe anapohisi ameambukizwa na virus vya ukimwi kwa hiyo wanapaswa kufanya yafuatayo.
Soma Zaidi...Dalili za fizi kuvuja damu
Posti hii inaelezea kuhusiana na Ugonjwa wa fizi ambapo fizi huweza kuwa na maumivu, kuambukizwa, kuvuja damu kwenye fizi na Vidonda.
Soma Zaidi...Matokeo ya maumivu makali.
Posti hii inahusu zaidi matokeo ya maumivu makali , kuna wakati mwingine mgonjwa anapata maumivu makali ya viungo na dawa mbalimbali uweza kutolewa kwa mgonjwa huyo lakini matokeo yake huwa ni kuendelea kwa maumivu kwa hiyo yafuatayo ni matokeo ya maumivu
Soma Zaidi...