Menu



Mkojo mchafu na Rangi za mikojo na maana zake

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu Rangi za mkojo na maana zake na mkojo mchafu

MKOJO MCHAFU NA RANGI ZA MKOJO NA MAANA YKE KIAFYA

 

Mwili wa binadamu ukiuchunguza kwa umakini unamengi ya kushangaza. Unaweza kuijuwa afya ya mtu kwa kuangalia ishara kadhaa na ukajuwa hadi maradhi anayouguwa na aina gani ya vyakula anatumia. Kwa mfano kwa kuangalia rangi za kucha, ngozi, macho, mate na mkojo unaweza kuhuwa mengi sana. Uso na nywele zinaweza kukupa hali halisi ya afya ya mtu. UTI ni katika maradhi yanayoweza kuonekana kwa kupitia uwepo wa mkojo mchafu ama kwa rangi ya mkojo. Katika makala hii tutakwenda kuona mkojo unatueleza nini kuhusu afya. Mkojo ukiwa mchafu ama msafi sana nini humaanishwa hapa. Endelea na makala hii, na usisahau kutembelea tovuti hii mara kwa mara.

 

Rangi za mkojo mkojo na mkojo mchafu na dalili zake

Kabla ya kuendelea kwnza nataka nifahamishe kuhusu rangi za mkojo. Baada ya kuzijuwa rangi hizi tutaweza kuona sasa nini tunajifunza kuusu afya na tabia ya mtu kwa kupitia kuchunguza rangi hizi za mkojo. Mkojo unaweza kuwa na rangi kadhaa kulingana na vyakula, vinywaji na hali ya afya. Miongoni mwa rangi hizo ni:-

 

1.Mkojo wa rangi ya njano

2.Mkojo wa rangi ya hudhurungi

3.Mkojo wa rangi nyekundu

4.Mkojo wa rangi ya chungwa

5.Mkojo wa rangi nyeupe

6.Mkojo wa rangi buluu

7.Mkojo wa rangi ya kijani.

 

Katika hali ya kawaida rangi ya mkojo huanzia kwenye njano. Kuzidi kwa njano inamaana hunywi maji ya kutosha. Na kadiri unavyokunywa maji kwa wingi ndivyo rangi ya mkojo inavyoendelea kusafika. Sasa ikitokea rangi ya mkojo inakuwa tofauti na hivi huwa kuna shaka inaingia. Na endapo unaona damu kwenye mkojo wako hakikisha unafika kituo cha afya maramoja maana utakuwa na tatizo la kiafya linalohitaji msaad haraka iwezekanavyo.

 

1.Mkojo wa rangi Rangi nyekundu au waridi (pink)

Rangi hii katika mkojo wako sio jambo la kuhamaki saana na ukaanza kuoata hofu. Hata usiwe na hofu saana uonapo rangi njekundu au pink kwenye mkojo wako. Miongoni mwa sababu zinazoweza kupeleke rangi ya mkoj wako kuwa hivi ni:-

 

A.Damu. Rangi ya mkojo wako kuwa mwekundu inaweza kuwa kuna damu inaingia kwenye mkojo. Damu hii inaweza kuashiria vitu kadhaa ambavyo nu hatari sana kwa afya yako. Kwa mfano kama rangi ya mkojo wako ni nyekundua na pink na ikawa sababu yake ni kuchanganyikana na damu, basi hapa tunaweza kusema kuwa: huwenda mtu huyu ana kichocho, au UTI, korodani linashida, ana mauvimbe yanayosababishwa na saratani, ana shida kwenye figo,amekimbia kwa umbali mrefu na kwa muda mrefu,ana vijiwe kwenye figo ama kwenye kibofu. Kama mkojo una rangi nyekundu hivyo moja kati ya hizo huwenda ndio sababu.

 

B.Vyakula pia vipo vyakula mtu akila huweza kubadili rangi ya mokojo wake na kuwa mwekundu.

 

C.Matumizi ya madawa. Yapo baadhi ya madawa yanaweza kubadili rangi ya mkojo kuwa mwekundu ama pink. Kwa mfano dawa kama rifampin ambazo ni antibiotics za kutibu TB.

 

Hivyo basi kama rangi ya mkojo wako ni nywekundu ama ni pink huwenda moja katika sababu tatu za hapo juu huchangia huenda ni vyakula ama madawa ama mchanganyiko wa damu. Na kama mkojo umechanganyika na damu na kuwa mwekundu ni vyema kwenda kituo cha afya kupata vipimo.

 

2.Mkojo wa rangi ya chungwa.

Kama ilivyokuwa kwa rangi nyekundu hata rangi ya chungwa kwenye mkojo wako sio jambo la kukupa taabu sanaa. Rangi ya chungwa kwenye mkojo inaweza kuashiria shida za kiafya kulingana na sababu ya kuwepo kwa rangi hiyo. Kwa mfano mkojo wa rangi ya chungwa unaweza kusababishwa na moja kati ya yafuatayo:-

 

A.Matumizi ya madwa: madawa huweza kuchangia katika kubadili rangi ya mkojo wako kuwa wa njao. Kwa mfano madawa ya anti-nflammatory kama vile sulfasalazine (Azulfidine) phenazopyridine (phyridium) ama madawa aina za laxatives na baadhi ya madawa ya kufanyia chemotherapy. Madawa haya yanaweza kuchukuwa nafasi kubwa katika kuufanya mkojo wako kuwa wa rangi ya chungwa.

 

B.Mkojo unaweza kuwa narangi ya chungwa kutokana na sababu za kiafya. Yaani yapo matatizo ya kiafya ukiwa nayo mkojo wako unaweza kuwa ni wa rangi ya chungwa. Kwa mfano mkojo unaweza kuwa wa chungwa kama una shida kwenye ini ama mrija wa nyongo na hali hii huendana na kuwa na kinyesi cha rangi ya mpauko. Pia kama huna maji ya kutosha mwilili hii inaweza kusaabbisha mkojo wako kuwa na rangi ya chungwa.

 

3.Mkojo wa rangi ya buluu na kijani.

Si jambo la kawaida kuona mkojo wako una rani ya buluu ama kijani. Lakini pia usipatwe na presha kuona lamda unakaribia kufa. Hapana unaweza kuwa na mkojo wa rangi ya buluu ama kijani na usiwe na shida kubwa za kiafya. Kwani rangi hizi kwenye mkojo huweza kusababishwa na moja kati ya yafuatayo:-

 

A.Vyakula, hutokea mtu akila baadhi ya vyakula vikapelekea hali hii. Haswa na hivi ndivyo.

 

B.Matumizi ya madawa. Yapo madawa ukitumia yanakwenda kubadili rangi ya mkojo na kuwa ya buluu ama kijanai. Kwa mfano amitriptyline, indomethacin (Indocin, Tivorbex) na propofol (Diprivan)

 

C.Pia maradhi. Unaweza kuwa na maradhi yakapelekea rangi ya mkojo kuwa ya buluu ama kijani. Kwa mfamo maradhi yaitwayo hypercalcemia. Huu ni ugonjwa unaosababishwa na kuzidi kwa madini ya calcium mwilini. Ugonjwa huu unaweza kuathiri utendaji wa kazi wa kibofu, figo, moyo na ubongo. Pia rangi ya buluu ama kijani kwenye mkojo inaweza kusababishwa na maambukizi kwenye mfumo wa mkojo.

 

Huvyo basi punde uonapo rangi ya buluu ama kijani kwenye mkojo wako ni vyema kufika kituo cha afya kujuwa hali yako zaidi. Na ujuwe nini hasa chanzo cha rangi hiyo.

 

4.Mkojo wa rangi ya hudhurungi

Kama mkojo wako una rangi ya hudhurungi pia usipatwe na presha saana. Rangi ya hudhurungi ni kama rangi tulizotaja hapo juu. Kwenye mkojo rangi ya hudhurungi inaweza kusababishwa na mambo mengi ikiwemo:-

 

A.Vyakula. Kama ilivyo rangi nyengine kwenye mkojo, vyakula huchukuwa nafasi. Kwa mfano zipo aina flani za maharagwe ukitumia rangi ya mkojo wako inaweza kuwa ni ya hudhurungi.

 

B.Madawa: kuna madawa mengi sana yanayoweza kupelekea rangi ya mkojo wako kuwa ya ahawiya. Kwa mfano madawa ya kutibu malaria (antimalarial drugs) kam vile chloroquine na primaquine, pia madawa ya aina za antibiotics metronidazole (Flagyl) na nitrofurantoin (Furadantin), laxatives containing cascara au senna, na methocarbamol — a muscle relaxant hizi zote huweza kusababisha rangi ya mkojo wako kuwa wa hudhurungi.

 

C.Pia maradhi, kwa mfano rangi ya mkojo inaweza kuwa ya hudhurungi kama una shida kwenye ini ama figo. Pia maambukizi kwenye njia ya mkojo yanaweza kusababisha hali hii.

 

D.Kufanya mazoezi makali kwa muda mrefu.

 

5.Mkojo wa rangi ya mawingu.

Maambukizi ya njia ya mkojo na mawe ya figo yanaweza kusababisha mkojo kuonekana kuwa wa mawingu.

 

6.Mkojo mweupe. Kama mkojo wako ni mweupe hongera sana. Inamaana umekunywa maji ya kutosha. Maji uhai, na viungo vyote vinahitaji majiili kufanya kazi vyema. Endapo mwili umepata upungufu wa maji unawez kupata shida za kiafya mwilini.

 

 

Kama rangi ya mkojo wako haisababishwi na vyakula basi huwenda ni kwa sababu ya madawa ama mardhi. Hivyo ni wakati sasa wa kujichunguza vyema. Kama umependa makala hii usiwachekutembelea kwenye tofuti hii wakati mwingine upate makala nzuri zaidi ya kiafya.

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea

Ndio     Hapana     Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Huduma Main: Post File: Download PDF Views 2962

Share On:

Facebook WhatsApp

Post zinazofanana:

Haya hayawezi kuambukiza UKIMWI

Somo hili linakwenda kukuletea mambo ambayo hayawezi kuambukiza UKIMWI

Soma Zaidi...
Mambo yanayoathiri Uponyaji was jeraha.

Posti hii inazungumzia kuhusiana na Mambo yanayoweza kuadhiri Uponyaji wa jeraha.jeraha huleta maumivu makali sana, vilevile Uvimbe, kutoa usaha. Pia jeraha hutofautiana katika kupona kwa mtu mzima na Mtoto.

Soma Zaidi...
Zijue sababu za kupoteza fahamu.

Posti hii inahusu zaidi sababu za kupoteza fahamu, ni sababu ambazo umfanya mtu kupoteza fahamu kwa sababu mbalimbali kama ifuayavyo.

Soma Zaidi...
Mkojo usio wa kawaida huwa na vitu vifuatavyo.

Posti hii inahusu zaidi Aina ya mkojo usiokuwaa wa kawaida uwa na vitu vifuatavyo, ukiona dalili kama hizo wahi mapema hospitalini Ili upatiwe huduma.

Soma Zaidi...
Dalili za shambulio la hofu

Shambulio la hofu ni tukio la ghafla la hofu kali ambayo husababisha athari kali za kimwili wakati hakuna hatari halisi au sababu inayoonekana. Mashambulizi ya hofu yanaweza kuwa ya kutisha sana. Mashambulizi ya hofu yanapotokea, unaweza kufikiri kwamba

Soma Zaidi...
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPANDWA NA PRESHA

Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg.

Soma Zaidi...
Fahamu kuhusu kazi za ini.

Posti hii inahusu zaidi kazi za ini, kwa kawaida tunafahamu kwamba ini ni sehemu muhimu kwenye mwili wa binadamu kwa sababu ni.likikosa kufanya kazi yake maisha ya binadamu yanakuwa hatarini kwa sababu mbalimbali.

Soma Zaidi...
Uvutaji wa sigara

Somo Hili linakwenda me kuhusu madhara ya uvutaji wa sigara

Soma Zaidi...
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPANDWA NA PRESHA

Presha ya kupanda hutokea pale kipimo kinaposoma zaidi ya 120/80mm Hg.

Soma Zaidi...
Huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na joto kubwa mwilini

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyepatwa na joto kubwa mwilini

Soma Zaidi...