Umuhimu wa kupima virus vya ukimwi kwa wajawazito na wanaonyonyesha
Post hii inahusu umuhimu wa kupima virus vya ukimwi kwa mama wajawazito na wanaonyonyesha. Ni hatua ya kupima Mama akiwa mjamzito na wakati wa kunyonyesha ili kuepuka hatari ya kumwambikiza mtoto
Umuhimu wa kupima virus vya ukimwi kwa mama mjamzito na wakati anaponyonyesha.
1. Tunajua wazi Mama akiwa mjamzito pale anapogundua kubwa ana mimba tu anapaswa kuja kliniki kupima maambukizi pamoja na mme wake, pengine Mama anaweza kuja kupima kwa Mara ya kwanza hasikutwe na virusi na akija kupimwa mara ya pili kabla ya kujifungua hasikutwe navyo lakini anaweza kuwa navyo kwa sababu ya kuwepo kwa hali mbalimbali vinaweza visionekane kwa hiyo anapaswa kupima tena akiwa ananyonyesha kwa sababu anaweza kupata ndani ya mda huo lengo ni kumzuia mtoto hasipatwe na Maambukizi.
2. Kwa kufanya vipimo vya marudio kwa mara tatu na wengine wanapima zaidi wakati wa ujauzito na kunyonyesha huweza kutambua hali ya Wazazi kwa ujumla na ikiwa Maambukizi yakiwepo ni rahisi kuanza Dawa mapema ili kuweza kufuvaza makali ya virusi vya Ukimwi kwa ajili kuimarisha afya ya mzazi na kumkinga mtoto dhidi ya Maambukizi, lakini Mama hasipoanza dawa mapema anaweza kumwambikiza mtoto na mtoto akazaliwa na Maambukizi.
3.Pia kwa kutumia dawa hizi umsaidie kuzuia magonjwa nyemelezi kwa Mama na mtoto pia kama vile ugonjwa wa kifua kikuu, Malaria, Magonjwa ya ngozi kupungukiwa na kinga ambapo upelekea Mama kubwa na mkanda wa jeshi na magonjwa mengine mengi uweza kutokea kwa sababu ya kuwepo kwa kinga ndogo ya mwili kwa hiyo Mama kama hajapima ugonjwa wa VVU na kuona magonjwa Mengi anapaswa kwenda kupima ili kujua afya yake na mtoto wake.
4. Kwa upande wa mtoto pale ikitokea Mama amejifungua mtoto huku mama ana Maambukizi mtoto anapaswa kuchukuliwa vipimo kama ifuatavyo, mtoto apimwe pale anapozaliwa, mtoto akiwa na umri wa miezi sita, pia akiwa na umri wa miezi tisa, miezi mitatu baada ya kuacha kunyonya na baada ya miezi kumi na minane, kutokana na vipimo vyote hivyo kama Mtoto hajagundulika na Maambukizi tunaweza kusema kuwa mtoto ni salama.
5. Kwa hiyo elimu inapaswa kutolewa kwa jamii nzima ili kujua umuhimu wa kupima maambukizi ya HIV ili kuepuka kuambukiza watoto hambao hawana hatia na wakati wa kwenda kliniki kwa Mara ya kwanza wazazi wanapaswa kwenda wote kupima maambukizi ili kuepuka kumwambukiza mtoto.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 Dua za Mitume na Manabii 👉2 Simulizi za Hadithi Audio 👉3 Kitabu cha Afya 👉4 kitabu cha Simulizi 👉5 web hosting 👉6 Madrasa kiganjani
Post zinazofanana:
Sababu za zinazosababisha kuwepo kwa vidonda
Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa vidonda, kwa sababu tunaona vidonda vinashambulia sehemu mbalimbali za mwili ila tunakuwa hatuna sababu kwa hiyo zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa vidonda.
Soma Zaidi...HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYEPATWA NA KWIKWI
Kwikwi sio hatari sana kwa afya, lakini inaweza kuwa hatari zaidi kwa mu aliyefanyiwa upasuaji kwenye tumbo.
Soma Zaidi...Njia za kukabiliana na presha ya kushuka
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kukabiliana na presha ya kushuka
Soma Zaidi...Faida za chanjo
Posti hii inahusu zaidi faida ya chanjo, tunajua wazi kuwa chanjo Ina faida kubwa kwenye mwili wa binadamu na vile vile kwenye jamii kama tutakavyoona hapo chini.
Soma Zaidi...Jinsi moyo unavyosukuma damu
Post hii inahusu zaidi jinsi moyo unavyosukuma damu, moyo ni ogani ambayo usukuma damu kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
Soma Zaidi...Haya hayawezi kuambukiza UKIMWI
Somo hili linakwenda kukuletea Mambo ambayo hayawezi kuambukiza UKIMWI
Soma Zaidi...