Makala hii itakujulisha kazi kuu za vitamini C mwilini. Hapa pia utatambuwa ni kwa nini tunahitaji vitamini C na wapi tutavipata
Vitamini C ni katika vitamini muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Vitamini hivi vina sifa ya antioxidant. Antioxidant zenyewe ndani ya mwili ndizo ambazo husaidia kuupa mwili nguvu na kinga ya kupamba na na sumu, na vijidudu shambulizi. Vvitamini C ina pendelewa kuwepo ndani ya miili yetu kwa wingi muda wowote. Wapo wataalamu wa afya wanapendekeza kutumia vitamini C kwa ajili ya kupunguza uwezekeno wa kupata mafua na homa ya mafua mara lkwa mara. Katika makala hii nimekuandalia somo zima kuhusu vitamini C, kuanzia chanzo chake, maana yake, upungufu wake na kazi zake kwenye miili yetu.
YALIYOMO:
Maana na Historia ya vitamini C
Vitamini C kitaalamu pia hufahamika kama “ascobic acid” ama ascorbate. Vitamini C ni katika water soluble vitamini ambayo husaidia kukinga mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeyee au kitaalamu scurvy. Ni maradhi hatari sana yanayodhurua afya. Kwa maelezo zaidi ya maradhi haya enelea kusoma makala hii.
Vitamini C vimegunduliwa miaka ya 1920 na Mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Albert von Szent Györgyi. Pia itambulike kuwa hapo mwanzo mwanasayansi aliyejulikana kwa jina la Kazimierz Funk yeye alieleza kuwa kuna maradhi yanasababishwa na upungufu wa virutubisho mwilini. Katika maradhi hayo aliyoyataja ugonjwa uitwao scurvy yaani kisehehe aliupa virutubicho kwa herufi C.
Baada ya ugunduzi wa Albert von Szent na haworth wakaipa herufi C kemikali iitwayo ascobic acid. Na hii ndiyo vitamini C. hivyo herufi C kwenye vitamini C ina maana ascobic acid hii ni tindikali. Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa wanyama katu hawawezi kuishi bila ya vitamini C mwilini mwao.Vitamini C ndio vitamini vya kwanza kuweza kutengenezwa na binadamu kikemikali.
VYAKULA VYA VITAMINI C
Kwa kuwa tumeshajuwa sasa maana na historia ya vitamini C hapa nitakwenda kukueleza chanzo cha vitamini C na je ni katika vyakula vipi tunapata vitamini C. kwa ufupi wa somo ni kuwa vitamini C unaweza kuvipata kwenye matunda yenye ladha ya uchachu uchachu (citrus) na matunda vyenye rangi ya njano na kwenye mboga za majani
Vyakula vya vitamini c
Tofauti na mboga za majani na matunda ya uchachu na yenye rangi ya njano pia tunaweza kupata vitamini C kwa kula maini, maziwa na mayai. Pia unaweza kupata vitamini C kwa kumezaa vidonge vya vitamini C.
KAZI ZA VITAMINI C MWALINI
Kama tulivyowkisha kuona kuwa vitamini C hulunda mwili dhidi ya mashambulizi na sumu za vyakula. Pia basi vitamini C husaidia katika kulinda mwili dhidi ya magonjwa mbalimbali kma kiseyeye, magonjwa ya ngozi, mifupa na moyo. Katika kipengele hiki utakwenda kuona kwa undani zaidi kuhusu kazi hizi za vitamini c mwilini:
Kazi kuu tatuza vitamini C
Tishu hizi ndizo ambazo zilitupa umbo letu, kwa lugha nyepesi hizi nyama zinazoonekana kwenye miili yetu, zilizofunika mbavu, mifupa, magoti, kichwa na maeneo yote ya mwili. Tishu hizi pia zinapatikana kwenye viungio vya miili yetu. Mifupa laini ya kwenye viungio vyetu pia ni katika tishu hizi. Hivyo protini huhusika katika utengenezwaji wa hizi tishu.
Kazi nyingine za vitamini C
Ugonjwa wa kiseyeye husababishwa na upungufu wa vitamini C na kutibiwa kwa kupata vitamini C aidha kwa kutumia vyakula ama vidonge vya vitamini C. dalili za ugonjwa huu huanza kutokea mwezi mmoja toka upungufu wa vitamini C uanze kutokea mwilini.
Dalili za ugonjwa wa kiseyeye:
Tafiti mbalimbali zilizofanya zinaonesha kuwa vitamini C inaweza kusaidia kupunguza nguvu za virusi waletao mafua na homa ya mafua. Baadhi ya tafiti zinadiriki kusema kuwa vitamini hivi kuponyesha mafua yaa kwa haraka, lakini ambalo halina shaka ni kuwa vitamini c vinaweza kupunguza kupata mafua ya mara kwa mara au kufanya mafua yaondoke kwa haraka.
Vitamini C ni muhimu sana katika mfumo wa kinga mwilini. Kwani vitamini C husaidia katika Antimicrobial yaani katika kuzuia vijidudu shambulizi mwilini kama bakteria na virusi, pia vitamini C husaidia katika Natural killer cell yaani katika kuuwa vijidudu shambulizi ama kuvizuia visiendelee kukua mwilini, pia vitamini C husaidia katika kuimarisha mfumo wa kinga kwa kuimarisha seli hai nyeupe ziitwazo lymphocyte hizi ndizo seli ambazo askari mkuu wa mwili dhidi ya vimelea vya maradhi kama virisi, fangasi, protozoa na bakteria.
Tafiti mbalimbali zimefanywa kuhusu aina ya saratani na zinavyohusiana na vitamini C kama saratani ya matiti na mapafu. Ijapokuwa tafiti hizi hazikuweza kuthibitisha moja kwa moja kuwa vitamini C vinasaidia kuondoa saratani hizi kalaki kuna mambo ambayo tafiti hizi yametufungua mawazo:
UPUNGUFU WA VITAMINI C
Endapo kutatokea upungufu wa vitamini C mwilini kuna athari kubwa itakayotokea mwilini ikiwemo:
ATHARI ZA KULA VITAMINI C KUPITILIZA
Kila kirutibisho kinahitajika ndani ya miili yetu kwa kiwango maalumu. Endapo kirutubisho kitakuwa kingi kupitiliza athari zinaweza kutokea katika afya ya mtu. Miongoni mwa athari za kuwa na vitamini C kupitiliza ni kama zifuatazo:-
Mwisho
Kwakuwa sasa unatambua umuhimu wa vitamini C ndani ya mwili wako. Hakikisha kula vyakula vyema ili kusaidia katika kuboresha afya yako. Endelea kuwa pamoja na si kwa makala nyingine za Afya.
MAKALA NYINGINE ZINAZOHUSU:
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za vyakula vya fati na mafuta
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mabadiliko kwa wavulana wakati wa kubarehe, ni kipindi ambacho ni kutoka utotoni kwendea ujana.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi malengo ya kusafisha vidonda, kwa sababu Kuna watu wengine huwa wanajiuliza kwa nini nisafishe kidonda hospitalini au kwenye kituo chochote Cha afya, yafuatayo ni majibu ya kwa Nini nisafishe kidonda.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mbinu za kuondoa sumu mwilini, ni njia mbalimbali ambazo uweza kutumika ili kuondoa sumu mwilini.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza kuusu vitamini D, kazi zake, upungufu wake na chanzo cha kupata vitamini D.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu namna ya kumsafisha mgonjwa kinywa,ni njia unazopaswa kufuata wakati unamsafisha mgonjwa kinywa hasa wale walio mahututi.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia ambazo maradhi huambukizwa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kuwepo kwa vidonda, kwa sababu tunaona vidonda vinashambulia sehemu mbalimbali za mwili ila tunakuwa hatuna sababu kwa hiyo zifuatazo ni sababu za kuwepo kwa vidonda.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna chanjo ya polio inavyotolewa na ratiba zake yaani kuanzia siku ya kwanza mpaka pale mtoto anapomaliza chanjo hii kwa hiyo tuone ratiba ya chanjo ya polio.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu kushiriki-ngono-na-mtu-aliye-na-vvu-na-ukimwi
Soma Zaidi...