Kuungua kupo kwa aina nyingi.
Kuungua kupo kwa aina nyingi. Mtu anaweza kuungua kwa umeme, moto wa kuni, moto wa gesi ama mvuke unaotoka kwenye mashine kama bomba la pikipiki. Pia mtu anaweza kuungua kutokana na miripuko kama baruti. Pia mtu anaweza kuunguwa kwa kemikali. Namna zote hizi zina utoaji huduma wake. Hapa nitaelezea kwa ufupi kuungua kwa moto.
Mtu anapoungua na moto angalia kwanza ni kwa kiasi gani ameungua. Kama ameungua sana ama eneo kubwa ni vyema kuwahi kutoa taarifa kituo cha afya kilicho karibu, ama kumuwahisha mgonjwa. Pia kuwa makini sana kama ameungua usoni, kwenye makalio ama miguu ama mikono au sehemu za siri.
Kama ameungua kawaida unaweza kumpatia huduma ya kwanza kisha uaendelea kumuangalia mgonjwa kama itahitajika kumpeleka kituo cha afya. Mtu aliyeungua unaweza kumpatia huduma ya kwanza kwa njia zifuatazo:
1.mwagilizia maji kwa muendelezo kwenye jeraha kwa muda wa dakika 15. ikishindikana kufanya hivi
2.Pepea sehemu yenye jeraha, ila usitumie barafu kwani linaweza kusababisha athari zaidi.
3.Unaweza kumpa mgonjwa dawa za maumivu kupunguza maumivu
4.Safisha jeraha kwa kimiminika cha iodine, ama aloevera gel. Na katu usimpake mafuta ya aina yeyote.
5.Unaweza kumpaka asali kwenye jeraha
6.ili kulinda jeraha dhidi ya kuvamiwa na bakteria mpake mmgonjwa kimiminika cha antibiotic
7.Lizibe jeraha kwa kulifunga na bendeji ama kitambaa kilicho safi na hakikisha hukazi sana wakati wa kufunga.
8.Angalia hali ya mgonjwa kisha umpeleke kituo cha afya kilicho karibu kwa uangalizi zaidi
Umeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyekazwa na misuli
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi faida za seli. Seli ni chembechembe hai za mwili ambazo hufanya kazi mbalimbali katika mwili wa binadamu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu mambo yanayosaidia kuboresha afya
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi umuhimu wa mate mdomoni, mate ni majimaji ambayo hukaa mdomoni na husaidia katika kazi mbalimbali mdomoni.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Aina ya choo kisichokuwa cha kawaida, ni dalili za choo ambacho siyo Cha kawaida, Ina maana ukiona dalili za choo Cha Aina hii ni vizuri kwenda hospitalini Ili kupata matibabu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mabadiliko katika umri wa kubarehe kwa wsichana, ni kipindi ambacho watoto huelekea ujana, utokea Kati ya miaka kuanzia Kumi na kuendelea.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia maambukizi kwenye milija na ovari, ni njia ambazo usaidia kuzuia maambukizi kwenye milija na ovari
Soma Zaidi...Kungโatwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mambo yanayochangia Ili dawa iingie vizuri kwenye damu, na mambo yanayoweza kusababisha dawa kuingia au kutoingia vizuri kwenye damu.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za upungufu wa vitamini C mwilini
Soma Zaidi...