Posti hii inahusu zaidi huduma ambazo wagonjwa wanaoishi na maambukizi ya virus vya ukimwi wanaweza kupata, huduma hii utolewa hasa kwa wale ambao wamejitokeza kupima afya zao na kujua wazi hali zao na kwa wale wanaofatilia huduma hii wanaweza kuishi vizu
1. Huduma ya kwanza ni kuwapa ushauri na kupima mara kwa mara afya zao Ili kuona wadudu wamafikia hatua gani na kuweza kutoa ushauri na elimu kuhusu namna ya matumizi ya dawa. Kwa sababu kwa wale wanaotumia dawa kila siku na kufuata mashart maendeleo yao ni mazuri mno na idadi ya virus upungua ingawa hawawezi kuisha Bali ufubaa.
2. Kuhakikisha wamekingwa na magonjwa nyemelezi, yaani magonjwa ambayo utokea pale kinga ya mwili inaposhuka , magonjwa hayo ni pamoja na kifua kikuuu ambapo dawa za kifua kikuuu utolewa kwa wagonjwa wetu na pia kuwapatia watoto vyakula mbalimbali Ili kuweza kuhakikisha kuwa wanakuwa na lishe ya kutosha yaani vyakula vya lishe utolewa kwa watoto wenye chini ya miaka mitano Ili kuepuka tatizo la kuwa na utapia mlo.
3. Kuzuia maamikimbi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto wakati Mama akiwa Mjamzito.
Akina Mama wote wanapokwenda clinic au kwenye mahudhulio ni lazima kwanza kabisa kupima ukimwi Ili kuweza kugundua kama Mama ana maambukizi kama anayo ushauri utolewa Ili kuweza kuepuka maambukizi kutoka kwa Mama kwenda kwa mtoto wakati akiwa Mjamzito, wakati wa kujifungua na wakati mtoto ananyonya kwa kipindi chote Mama anakuwa karibu na wahudumu wa afya Ili kuhakikisha mtoto hasipate maambukizi.
4. Kutoa elimu kwa watu ni kuwaahamasisha kupima virus vya ukimwi.
Kuna vikundi mbalimbali ambavyo vimeandaliwa Ili kuweza kutoa elimu kwa jamii Ili kuhakikisha watu wapime pia na kutumia kinga Ili kuweza kupunguza kuendelea kuwepo kwa ugonjwa wa ukimwi na pia kuwaanzishia dawa wale wote waliopata maambukizi ya ukimwi,kwa kufanya hivyo jamii itaweza kuishi kwa matumaini .
5. Pamoja na kuwepo kwa ugonjwa huu hatari watu wanapaswa kujua kuwa matumizi ya dawa ni muhimu na kwa kufuata mashart kwa sababu Kuna watu wengi wameugua ugonjwa huu lakini bado wanaoishi na wanaendelea vizuri kwa hiyo tusiwakatishe tamaaa wagonjwa tuwajali na tusiwatenge kwa sababu na wenyewe Wana haki ya kuishi kama watu wengine.
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Umeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza nywele za mgonjwa hasa kwa wagonjwa mahututi na wale wasiojiweza tunafanya hivyo ili tuweze kuwatoa kwenye hali ya usafi.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hasara za magonjwa ya ngono, ni magonjwa yanayoambukizwa kwa kujamiiana bila kutumia kinga.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili za kuwepo kwa kizungu Zungu,ni Dalili ambazo Uweza kujionyesha kwa mtu ambaye ameshawahi kupatwa na tatizo la kizungu Zungu au hajawahi kupata dalili zenyewe ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ambayo yanaweza kutokea kwa mtu mwenye uzito mkubwa,kwa kawaida ili mtu aweze kuwa na uzito wa kawaida ni vizuri na kiafya kupima urefu ukilinganisha na uzito wa mtu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia au kujikinga na kifua kikuu, hizi ni njia ambazo utumika ili kujikinga na kifua kikuu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kumsafisha mgonjwa kinywa, Mgonjwa akiwa anaumwa na pia anakula chakula ni lazima asafishwe kinywa Ili kuweza kuepuka madhara mengine yanayoweza kujitokeza kwa sababu ya kuwepo kwa uchafu kinywani.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria kwa kitaalamu huitwa vibrio cholera.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hatua za kufuata unapohisi umeambukizwa na virus vya ukimwi. Kwa sababu watu wengi wanakuwa na kiwewe anapohisi ameambukizwa na virus vya ukimwi kwa hiyo wanapaswa kufanya yafuatayo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi mbinu za kuondoa sumu mwilini, ni njia mbalimbali ambazo uweza kutumika ili kuondoa sumu mwilini.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi namna ya kutoa huduma ya kwanza kwa watu waliopata ajali. Ajali ni tukio lisilotarajiwa ambalo kinaweza kumkuta mtu yeyote, tunapotoa huduma ya kwanza tnazingatia rangi ambazo huwakilisha jinsi watu walivyoumia.
Soma Zaidi...