Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyoka
HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYOKA
Nyoka wapo katka makundi makuu mawili, kuna wenye sumu na wasio na sumu. Ni vigumu kuwatofautisha wenye sumu na wasio na sumu kwani wakati mwengine wanafanana sifa. Wataalamu wameweka njia kadhaa za kuweza kuwajuwa weenye sumu. Nyoka mwenye sumu ana sifa zifuatazo
1.kichwa chake kipo katika pembe tatu
2.Rangi zake zinameremeta sana
3.Mboni ya Macho yao yamefanana na macho ya paka
4.Wanapoogelea kwenye maji miili yao inaelea juu
Tmbua kuwa sifa hizi hata nyoka wasio na sumu wamaweza kuwa nazo. Kuwa makini na kaa mbali na nyoka wa aina yeyote kama huna ujuzi na utambuzi huu. Mtu aliyengatwa na nyka mwenye sumu ataonyesha dalili zifuatazo:-
1.Uchovu
2.Kizunguzungu
3.Anaweza kuzimia
4.Kichefuchefu
5.Kuharisha
6.Kutapika
7.Mapigo ya moyo kuongezeka kwa kasi
8.Misuli kukosa uweze wa kutanuka na kusinyaa
9.Kuvimba eneo alipong’atwa.
Ukiona mtu ameng’atwa na nyoka na akaonyesha dalili hizi, wahi kuomba msaada ili awahishwe ituo cha afya kwa haraka. Hakikisha unampatia huduma ya kwanza ili kupunguza athari za kusambaa kwa sumu mwilini. Huduma ya kwanza kwa mtu aliyeng’atwa na nyoka inaweza kuwa kwa nama zifuata zo:-
1.mtulize mgonjwa nafsi yake, mpe maneno matamu na ya kutuliza. Hii itasaidia moyo kupunguza kazi ya kusambaza damu mwilini, hivyo sumu haita sambaa kwa kasi.
2.Muweke mgonjwa chini, na katu usimtembeze, mlaze chini kwa namna ambayo sehemu alipong’atwa itakuwa chini. Kwa mfano kama ameng’atwa mguuni, unaweza kumuwekea kitu kichwani akaegemea kwa mto ili sehemu ya mguuni iwe chini.
3.Ondoa mengo ya nyoka kwa uangalifu na katu usimishe eneo alilongatwa na nyoka.
4.Kama mgonjwa ana kizunguzungu, ama baridi mfunike kwa nguo ili kumuongezea joto
5.Chukuwa maelezo kuhusu aina ya nyoka, hii itasaidia wataalamu wa afya kujuwa tiba sahihi.
6.Osha eneo kwa kupitishia maji kwa juu na katu usisugue ama kuminya jeraha.
Usifanye vitu hivi:
1.Usinyonye sumu kwa mdomo wako
2.Usimpe mgonjwa chakula wala maji
3.Usimtembeze mgojwa
4.Usitumie barafu sehemu yenye jeraha
5.Usifunge kwenye jeraha eti kuzuia mzunguo wa damu
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za mdomo kuwa mchungu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu njia na namna ya kumhudumia aliyeingiwa na nyoka. Nyoka ni kiumbe ambacho Kina sumu kali na mtu akifinywa na nyoka asipohudumiwa anaweza kupata ulemavu au kupoteza maisha
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Aina mbalimbali za vidonda kwenye mwili wa binadamu, ni vidonda ambavyo utokea kwenye mwili wa binadamu kwa Aina tofauti.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za kuzuia damu isiendelee kuvuja, ni njia ambazo utumika ikiwa kuna damu inavuja kwenye sehemu yoyote ya mwili,kwa hiyo tunaweza kutumia njia hizi ili kuepuka kuendelea kuvuja kwa damu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kupoteza fahamu, ni sababu ambazo umfanya mtu kupoteza fahamu kwa sababu mbalimbali kama ifuayavyo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi sababu za michubuko kwa watoto wanaozaliwa,ni sababu ambazo uweza kuchangia kuwepo kwa michubuko kwa watoto wanaozaliwa.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi ugonjwa wa kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria kwa kitaalamu huitwa vibrio cholera.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni, haya ni madhara ambayo utokea kwa sababu ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi madhara ya kutotibu homa ya uti wa mgongo, kwa kuwa ugonjwa huu mara nyingi uathiri sehemu za kwenye ubongo kuna madhara ambayo yanaweza kutokea endapo Ugonjwa huu haujatibiwa mapema.
Soma Zaidi...