ELIMU YA UJAUZITO, MIMBA NA KIZAZI

ELIMU YA UJAUZITO, MIMBA NA KIZAZI

UTANGULIZI:-
Ni ndoto ya kola mwanamke na mwanaume siku moja awe na mtoto na familia. Kufanya hivi watu wamekuwa wakitafuta ujauzito, wengine unakuwa na wengine unatoka. Kuna wengine hawabahatiki kabisa kupata ujauzito. Makala hii ni kwa ajili yako. Hapa utakwenda kupata utaratibi mzima wa mimba, kutoka kuingia kwake hadi kujifunguwa. Hapa nitakueleza mambo kadhaa kwa ajili ya kukupa Nukuu za juu juu muhimu hasa kwa wale ambao huu ni ujauzito wao wa kwanza.SIKU YA KUPATA UJAUZITO
Swala la kupata ujauzito limekuwa likikabiliwa na imani nyingia ambazo sio sahihi. Watu wengi wamekuwa wakipoteza muda na fedha kujaribu kutatua maswali yao. Leo nitakusaidia kutatua swali hili Je..! ni zipi dalili za mimba changa. Swali hili ni la msingi kwani kuna watu wengi wamekuwa wakichanganya dalili za ujauzito na shida nyingine za kiafya. Hapa nitajaribu kukufahamisha utofauti wa dalili hizi na nyingine ili upate kufahamu vyema.Imani potofu kuhusu dalili za ujauzito:-
1. Mimba inaingia siku yeyote ile. Hii sio sahihi kabisa mimba inasiku maalumu ambazo huweza kutungwa. Kitaalamu siku hizi zinafahamika kama fertile window
2. Siku yya 14 ndio siku ambayo mimba hingia. Hii pia sio sahihi, kwani wanawake sio wote wanaingia siku 28, kuna wengine ni kati ya 21 mpaka 35
3. Unaweza kupima mimba kwa ktumia sukari, chumvi, mafuta, sabuni, delto. Hizi zote sio sahihi kabisa.Ni siku gani mimba huingia.
Mimba huweza kuingia siku ambayo yai litakutana na mbegu ya kiume kwenye mirija ya falopia kwenye tumbo la uzazi la mama. Yai la mwanamke kuzalishwa kwenye ovari. Mwanamke ana ovari mbili, moja upande wa kulia na nyingine kushoto. Hizi mbili hupeana zamu ya kutoa mayai. Yaani kama mwezi huu limetoa hili na nyingine itatoa mwezi ujao.Tafiti zinaonyesha kuwa yai huweza kuanza kukomaa kuanzia siku ya 10 toka kupata hedhi mpaka siku ya 14. hii ni kwa wanawake wengi. Ila si wote. Kikawaida yai hutolewa (ovulation) kwa makadiria ya siku 12 mpaka 16 kabla ya kupata hedhi nyingine. Yaani unaweza kuhesabu kabla ya kuingia hedhi siku 12 nyuma, kisha toa siku 4 mnyuma ndani ya siku nne zizi ndizo yai hutolewa. siku hizi ndizo moja wapo yai hutolewa. Kwa mfano:--1.Mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21, sasa tunatoa siku 12 nyuma kabla ya kuingia hedhi (21 - 12 = 9) kisha toa nne nyuma (9-4=5) basi mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 5 na 9 katika siku zake.2.Mwanamke mwenye mzunguruko wa siku 32: tunaanza kutoa siku 12 nyuma kabla ya kupata hedhi yake (32-12=20) tonatoa siku nne tena nyuma (20-4=16) kwa hiyo mwanamke huyu anaweza kutoa yai kati ya siku ya 16 mpaka 20.4. Mwanamke mwenye siku 28: 28-12 = 16 kisha toa siku 4 nyuma 16 - 4 = 12. hivyo siiku ambazo yai hukomaa kwa mwenye siku 28 ni kati ya 12 mpaka 16.Sasa baada ya kuzijua siku hizi ambazo yai hukomaa, inabidi ufahamu kuwa yai la mwanamke huweza kuishi kati ya masaa 12 mpaka 24 toka kukomaa (ovulation). kwa upande mwingine mbegu za kiume huisho kati ya siku 3 mpaka 5. hivyo ujauzito unaweza kutungwa kwa mbegu ambayo ilikuwepo toka siku tatu zilizopita.
NI IPI HASA SIKU AMBAYO NITAFUTE UJAUZITO?
Kama ulipojifunza hapo juu kuwa zipo siku maalaumu ambazo yai hukomaa. Katika siku hizo mojawapo yai huletwa kwenye mirija ya falopia. Baada ya kukokotoa siku zako hapo juu sasa itakubidi kuongeza siku moja ama mbili nyuma. Hii ni kwa sababu makadirio ya siku hutofautiana. Na si lazima kkutafuta toto katika siku zote hizi. Unaweza kuruka kwa siku moja moja.Jitahidi kufanya tendo la ndoa hasa katika siku hizo nne ulizozipata baada ya kukokotoa. Katika siku hizo jitahidi kufanya tendo siku ambayo itakuwa na sifa zifuatazo:-1. Majimaji ya mwanamke ukeni yatakuwa ni mengi kuliko siku zilizopita. Mwanamke mwenyewe anaweza kujichunguza hali hii na kuigundua ila taabu. Anaweza kutumia kidole ama kitambaa safi kuchunguza uwepo wa majimaji haya katika ukeni kwake. Kumbuka hali hii isiambatane na shida nyingine za afya kama PID. Wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kuchunguza hasa kwa wale wanaotumia uzazi wa mpango hasa hasa kwa kutumia vidonge vya homoni.2. Joto la mwanamke litakuwa ni kubwa kuliko siku nyingine. Joto hili sio homa, na lisiambatane na sababu nyingine kama maumivu ya kichwa, ama kutokana na kulala sana, ama misongo ya mawazo. Kikawaida siku ambayo yai hutolewa joto la mwanamke linakuwa kubwa hivyo akishiriki siku hii ujauzito ni rahisi kuingia.3. Siku ambayo mwanamke atakuwa na hamu sana ya kushiriki tendo. Wakato ambapo yai hutolewa kuna homoni huzalishwa kwa wingi. Homoni hizi zinaweza kusababisha mwanamke kutamani sana kushiriki tendo zaidi ya siku nyingine.Pindi mwanamke atakapojigundua kuwa siku hii ameipata basi ni vyema kushiriki tendo ndani ya siku hii ama siku itakayofata haraka iwezekanavyo, maana yai la mwanamke linaweza kufa ndani ya muda mchach masaa 12 mpaka 24.DALILI ZA MIMBA CHANGA:
Baada ya kutambuwa sku sahihi ya kutafuta ujauzito sasa ninakwenda kukufahamisha kama mimba iliingia, kama harakati zako zilifahamika. Dalili nitakazokutajia unaweza kuzishuhudiandani ya wiki ya mwanza mpaka wiki ya nne. Hata hivyo kama utakuwa makini unaweza kugundua ndani ya siku chache tu kama sio siku moja ama mbili.Kabla ya kuendelea ningependa utambuwe kuwa mimba huleta mabadiliko makubwa sana kwenye mwili wa mwanamke. Hivyo ni lazima mabadiliko haya yaonyeshe dalili zozote punde tu inapoingia. Hivyo kwa mwanamke akiwa makini na mwii wake anaweza kugundua mabadiliko haya mapema sana. Kuna mwanamke mmoja alinieleza kuwa yeye anaweza kugundua ujauzito kama umetunga ndani ya masaa machache toka akutane kimwili. Nilistaajabu ila nilishindwa kumuuliza anatumia njia gani.Dalili za mimba changa ni pamoja na:-DALILI ZA MIMBA KATIKA WIKI YA KWANZA NA PILI (SIKU 7 MPAKA 14)
1. Kuendelea kwa joto la mwili. Kama ulikuwa makini na siku ambayo joto la mwili wako lilikuwa kubwa, kama ulishiriki tendo siku moja ama mbili kabla ama siku ile, basi endapo joto la mwili litakuwa endelevu hii huashiria huwenda ulibeba ujauzito. Kwa nini, ni kwa sababu joto la mwili hutokea baada ya mabadiliko ndani ya mwili hususani homoni mpya huzaliwa kwa ajili ya kuandaa ukuaji wa ujauzito. Mabadiliko haya ya joto yasifananishwe na joto la homa.2. Katika wiki hii ya kwanza unaweza kuona mabadiliko ya majimaji kwenye uke. Majimaji yaliyokuwa siku za nyuma kidongo yanaweza kuanza kuchukuwa sura ya mfanano wa majimaji meupe ya yai lililovunjwa. Halikadhalika matarajio ni kuwa uke unatakiwa urudi katika hali ya ukavu baada ya kupita siku hatari. Lakini kama ujauzito ulitungwa uke hautarudi katika hali yake ya kawaida ya ukavu hivyo huanza kuzalisha majimaji kwa wingi. Mabadiliko haya si rahisi kuyaona ila endapo utakuwa manini zaidi unaweza kugundua.3. Kutokwa na damu kidogo (implantation bleeding). damu hii inaweza kutokea mwishoni mwa wiki ya kwanza ama katikati ya wiki ya pili. Damu hii ni kidogo na inaweza kuwa ni matone kadhaa. Haifanani na damu ya hedhi na wala haitoki na maumivu. Damu hii si endelevu inaweza kutoka kwa muda mchache na kukata. Mwanamke anaweza kuona nguo yake ya ndani inamadoa ya damu. Kwa damu hii mwanamke hatahitai kuvaa pedi.4. Maumivu ya kichwa ama kichwa kuwa chepesi. Hali hii inaweza kuandamana na kizunguzungu. Hali hii si lazima kuipata, hata hivyo wanawake wengine wanaipata ila hawafikirii kuwa ni tatizo kwani hutokea na kuondoka bila ya kuathiri mwili kwa muda mrefu. Hapa anaweza kuona ni hali ya kawaida kama hatatilia maanani mabadiliko haya.Kumbuka dalili hizo tajwa hapo juu ni ngumu kuziona mpaka uwe makini sana kwani zinaweza kuathiriwa na hali nyingine za kiafya. Kwa mfano joto la mwili linaweza kusababishwa na mambo mengi kama maradhi, uchovu na stress. Majimaji ya ukeni yanaweza kuongezeka kwa sababu ya njia za uzazi wa mpango ama mabadiliko ya homoni.DALILI ZA MIMBA KATIKA MWEZI WA KWANZA (Ndani ya siku 30)
Dalili hizi huweza kuonekana kwa urahisi kuliko hizo ambazo zimetajwa hapo juu. Ijapokuwa dalili hizi zinatokea ndani ya mwezi mmoja lakini zinaweza pia kutokea nje ya mwezi mmoja, yaani mpaka miezi mitatu. Sasa hebu tuzione dlili hizo:-1. Kukosa hedthi.
Kama ujauzioto ulishika mwanamke hataweza kupata siku zake. Hii ni dalili ambayowanawake wengi wamekuwa wakiamini kama ndio dalili pekee. Yes hii ni katika dalili kubwa ambazo wanawake wengi wameitaja kuwa ndio dalili yao ya kwanza. Unajuwa ni kwa nini? Ni kwa sababu ndio ya pekee wanayoweza kuigundua. Ukweli ni kuwa kukosa hedhi pekee sio dalili ya ujauzito, hedhi inaweza kukosekana kwa sababu kadhaa kama zifuatazo:-A. Mabadiliko ya homoni
B. Ujauzito
C. Maradhi
D. PID
E. Vyakula
F. Stress na misongo ya mawazo
G. Matumizi ya madawa
H. Mabadiliko ya hali ya hewa.Nini mwanamke afanye baada ya kukosa hedhi?.
Yes hili ni swali zuri sana. Mwanamke aliyekosa hedhi kwanza aanze kufikiria kama alishiriki tendo la ndoa katika siku hatari ama laa. Kisha aangalie uwepo wa dalili nyingine kama nitakavyozitaja hapo chini. Kama hana dalili yeyote basui aangalie kama anapata maumivu sehemu yeyote, ama uwepo wa maradhi. Kama vyote hana ni vyema apime ujauzito. Kipimo cha mkojo kinaweza kuchelewa kutoa majibu, hivyo kama atapima wiki ya kwanz na asione kitu basi ni vyema akarudia tena wiki inayofata. Maelezo zaidi juu ya kutumia kipimo nitayataja hapo chini.2. Maumivu ya matiti na chuchu, kujaa kwa matiti na mabadiliko ya rangi za chuchu.
Dalili hii huwapata wanawake wengi, hata hivyo wapo ambao hawaipati kabisa. Hebu tuanze kuona kwa ufupi dalili hii. Mabadiliko ya rangi ya chuchu na eneo la kuzunguka chuchu. Hii ipoje ni kuwa mwanamke aliyebeba ujauzoto chuchu zake zinaweza kubadilika na kuweka ukiza na weusi. Inaweza kuwa chuchu pekee na na eneo la chini kuzunguka chuchu.Kwa baadhi ya wanawake wao matiti yanauma na yanakuwa kama yamejawa na kaugumu flani. Wakati mwimgine inaweza kuwa titi moja ama yanaweza kuwa yote ama yakapeana zamu. Ila maumivu haya ni maumivu ambayo yanavumilia si makali kiasi cha kushindwa kufanya shughuli za kawaida. Kwa wanawake wengine maumivu haya hutokea pale anapoyaminya matiti yake.Hata hivyo maumivu ya matiti pekee sio dalili ya moja kwa moja kuthibitisha ujauzito. Maumivu ya matiti yanaweza pia kusababishwa na maumivu ya kifua, shida katika homoni ama maradhi mengine. Hivyo bado itahitajika kupuma kupata uhakika.3. Kukojoa mara kwa mara.
Wiki kadhaa zimepita toka kuingia, homoni mbalimbali zimezalishwa ndani ya mwili,kwa ajili ya kuhakikisha usalama wa mama na mtoto. Homoni hizi zinapelekea mabadiliko mbalimbali ndani ya mwili wa mama, hivyo kusababisha mapigo ya moyo kuongezeka, mchujo wa damu kuwa mkubwa na uzalishwaji wa mkojo kuongezeka. Hapa mama mjamzito ataanza kuhisi mabadiliko katika kukojoa kojoa. Dalili hii kwa baadhi yao inachelewa kuonekana hadi miezi ya mbele.
4. Mapigo ya moyo kuongezeka.
Hapa mwanamke anaweza kujihisi moyo kwenda mbio. Ukweli nikuwa kuna ongezeko la mapigo ya moyo kwa ajili ya kuhakikisha maendeleo ya mtoto aliyetumboni hayaathiriki. Dalili hii pia inaweza kuchelewa kuonekana ndani ya mwezi wa kwanza. Kwa baadhi ya wanawake watajihisi lamda ana presha lakini ukweli ni kuwa hii sio presa ni ongezeko tu la mapigo ya moyo.5. Maumivu ya tumbo.
Dalili hii inaweza kutokea hata katika wiki kadhaa za mwanzo. Ila mara nyingi hutokea ndani ya mwezi wa kwanza na ni endelevu. Yaani dalili hii inaweza kuendeea mpaka mtoto atakapozaliwa. Mwanamke awe makini sana na maumivu haya. Maana yanaweza kusababishwa pia na mambo mengine ikiwemo maradhi. Maumivu haya hayawezi kuwa makali kiasi cja kushindwa kufanya kazi za kawaida. Yanaweza kufanana na ya hedhi ama kuwa na uafadhali kidogo.DALILI NYINGINE ZA UJAUZITO
1. Uchovu wa mara kwa mara
2. Maumivu ya tumbo mara kwa mara
3. Kichefuchefu
4. Tumbo kukuwa.
5. Mtotockucheza
6. Kuongezeka kwa uzito
7. Kupata kiungulia mara kwa mara
8. Kukosa choo
9. Maumivu ya mgongo
10. Hasira za mara kwa mara
11. Maumivu maeneo ya nyonga
12. Kuharisha
CHANGAMOTO ZA UAJAUZITO NA DALILI ZENYE KUENDELEA:
Ni vyema sana kutambuwa hili, kwani itakusaidia katika klujuwa changamioto za ujauzito. Katika dalili hizi za ujauzito zipo ambazo nio zenye kuendelea. Na katika kuendelea hko wengi katika wajawazito wanapatwa na changamoto kadhaa. Hapa nitakueleza nini cha kufanya.1. Kichefuchefu
Kichefuchefu kinaweza huweza kuchelewa kujitokeza lakioni kinaweza kuwa ni chenye kuendelea. Kwa baadhi ya wanawake kinaweza kwenda mpka miezi kadhaa mbele, ila kwa wengi kinaweza kukata kufikia wiki ya 28. Hii ni changamoto kwakweli kwa wajawazito. Maana kichefuchefu kinaweza lumkoseshea amani wakati mwingine.hali ya kutema mate, kuhisi kutapika ama kichefuchefu kwa ujumla huwasumbua wajawazito. Wataalamu wanaeleza kuwa hasa chanzo cha kichefuchefu ni mabadiliko ya homoni mwilini. Na huwenda pia kuna sababu nyingine.Kama utakuwa unasumbuliwa na hali hii fanya hivi. Epuka kukaa maeneo yenye joto sana. Epuka kunywa maji wakati unakula. Tumia tangawizi, kwenye chai ama tafuna. Unaweza kuiweka kama unga ama vipande vidogovidogo. Unaweza kutumia bigjii maalumu kwa ajili ya wajawazito.2. Maumivu ya tumbo:
Kwa wajawazito maumivu ya tumbo mara kwa mara ni hali ya kawaida na yenye kuendelea. Maumivu haya yanaweza kuchukuwa muda mchache na kuondoka. Pia ni yenye kuvumilika yaani mwanamke anaweza kuendelea kufanya shughuli zake. Ila endapo yatakuwa ni makali sana kutovumilika inaweza kuashiria kuna shida kwenye afya ya mwanamke huyu. Ni vyema kufika kituo cha afya kupata ufafanuzi wa hali.Katika hali ya maumiovu haya ya tumbo mwanamke anaweza kutumia dawa za kupunguza maumivu. Pia zipo tiba mbadala kupunguza maumivu. Ila mwanamke awe makini sana maana anaweza kuingia katika hatari endapo atatumia dawa kiholela.3. Kutokwa na damu:
Kama ilivyo dalili nyingine huendelea basi si jambo ;la kushangaza kwa mwanamke mjamzito kujikuta nguo yake ya ndani kuwa na vitone vya damu. Damu hii si yenye kuchuruzika ama yenye kutoka kwa wingi kama damu ya hedhi. Endapo mjamzito atakuwa anatokwa na damu nyingi eidha iambatane na maumivu makali ya tumbo ama isiambatane ni vyema awahi kituo cha afya kupata uthibitisho juu ya mabadiliko hayo. Maana wakati mwingimne damu inaweza kuashiria shida katika ujauzito.4. Mabadiliko katika hisia, matakwa na matamanio katika vyakula na vitu vingine.
Haswa mwanamke anaweza kujishangaa mwenyewe inakuweje hali hii. Mwanamke anaweza kuona kuwa nachukia vitui ama kuna watu anawachukia ghafla. Wakati huo huo anaweza kupenda mtu flani sana. Pia kuna wakati atakuwa anachukia baadhi ya vyakula na vitu vingine. Yaani kwa ufupi ni mabadiliko tu katika saikolojia yake. Huu si ugonjwa hivyo hali hii isimpe mawazo saana mwanamke. Watu walio karibu na wajawazito wawe makini pia maana wanaweza kufanya makosa makubwa kama kumpiga na vinginevyo.5. Kuvimba ama kujaa kwa uso na miguu.
Yes hii ni changamoto kwa kweli. Hii haiwapati wenye mimba ya miezi ya mwanzo, hali hii hutokea wakati mimba imesha komaa miezi ya mbeleni. Kuvimba ama kujaa kwa uso na miguu kwa wajawazito sio jambao la ajabu. Hali huweza kukaa sawa atakapojifungua. Kama mwanamke anasumbuliwa na hali hii, ahakikishe anapumzika katika maeneo yenye utulivu na yaliyopa yaani aepuke kukaa maeneo yenye joto. Pia aepuke kubvaa nguo za kabana. Aepuke kukaa chini katika mkao mmoja kwa muda mrefu.6. Kuenda haja ndogo mara kwa mara.
Hii ji changanmoto hasa kwa wale ambao ndio ujauzito wao wa kwanza.Hapa pia kuna wajawazito wanajitahidi kujizuia eti wapunguze kuenda haja ndigo. Hii sio sawa kabisa. Mjamzito anatakiwa anaposikia haja kakaitoe wala asihofu kitu huu si ugonjwa na ni kawaida kabisa. Kwa kuwa moyo wake umeongeza utendaji wa kazi hivyo uchujwaji wa damu ni mkubwa. Kwa maendeleo mema ya afya yake na afya ya ujauzito wake, mjamzito asihofu kitu, aende tu haja.JE NITAHAKIKISHA VIPI KAMA NINA UJAUZITO?
Hili ni swali la msingi kabisa, maana unaweza kuwa na dalii za ujauzitio lakini si ujauzito, ama unaweza kuwa ujauzito lakini ukipima huoni kitu. Sasa nini tufanye. Njia pekee ya kuhakiki kama ni ujauzito ama sio ni kupima. Unaweza kutumia kipimo cha mkojo ukiwa nyumbani ama kwenda kupima hospitali.Kama utatumia kipimo cha mkojo fika duka la dawa na hakikisha unapewa kipimo kilichokuwa hakiku expire. Pata maelekezo kutoka kwa uuzaji kama ni mara yako ya kwanza. Pia maelekezo utaweza kuyakuta kwenye hiko kipimo ila lugha inaweza usielewe. Kipimo hili kinafanya kazi kwa kuangalia uwepo wa kemikali ambazo huzaliwa wakati wa ujauzito. Endapo zitakuwepo kipimo kitaonyesha kuwa ni mjamzito.Sasa ni muda gani unafaha kupima?
Ni vyema kupia wiki mbili baada ya kukosa hedhi. Endapo utapima wiki moja baada ya kukosa hedhi ama utapima mapema zaidi kuna uwezekano kuwa hutapata majibu kama ni mjamzito. Hivyo inashauriwa sana kusubiri baada ya wiki mbili toka kukosa hedhi ndipo upime. Kama utakwenda kupima hospitali haina shida hata ukiwahi maana zipo njia nyingi wanaweza kutumia.Nina dalili za uajauzito lakini nikipima sina?
Hili ni katika maswali ambayo wanawake wengi wamekuwa wakiuliza. Inatokea anazo dalili zote za ujauzito lakini akipima hakuna kitu. Kuna sababu nyingi juu ya swala hili. Kabla ya kuendelea na somo hili zaidi, wacha nikufahamishe kuwa, yafuatayo yanaweza kusababisha usione ujauzito kwenye kipimo:-1. Kama umepima mapema kabisa
2. Kama kipimo ni kibovu
3. Kama umekosea namna ya kupima
4. Kama huna ujauzito
5. Homoni za ujauzito hazipo za kutosha kwenye mkojo.Hizi ni katika sababu tu zinazotokea hasa wakati wa kupima. Sasa wacha tuingie katika somo hili kitaalamu zaidi. Ni kwa nini unaweza kupata dalili za uajauzitio zilizotaja hapo juu lakini ukipima huna hata ujauzito?. nitaangalia hoja kuu tano za kutokea kwa hali hizi kama ifuatavyo:-1. Kukosa Hedhi
Kukosa hedhi ni dalili ya ujauzito, lakini haimaanishi kuwa ni lazima utakuwa mjamzito. Kwani mwanamke anaweza kukosa hedhi kwa moja ya sababu zifuatazo:-
A. Uwiyano usiosawa wa homoni (hormene imbalance)
B. Madawa
C. Maradhi katika ovari
D. Magonjwa kama ya PID
E. Misongo ya mawazo
F. Vyakula
G. Njia za uzazi wa mpango2. Kuuma kujaa na kuvimba kwa matiti. Hii inaweza kuwa ni dalili ya ujauzito.akini pia hali hii inaweza kusababishwa na mambo kadhaa ambayo yanaweza yakakufanya uhisi ni mjamzito.kwa mfano:-
A. Kuwepo kwa uvimbe kwa ndani (breast sore)
B. Kuwepo kwa shida katika tishu za matiti (fibrocystic breast tissue)
C. Kwa wakati mwingine mazoezi makali yanaweza kusababisha hali hii.
D. Uvutaji wa sigara
E. Pia uwiyano mbaya wa homoni (hormone imbalany)3. Maumivu ya kichwa na kichefuchefu yanaweza kusababishwa pia na sababu nyingine. Ijapokuwa inakadiriwa kuwa asilimia 70 ya kichefuchefu ni ujauzito. Mengine yanayoweza kusababisha ni misongo ya mawazo, vyakula, maradhi na vidonda vya tumbo, sumu katika vyakula na mengineyo.4. Maumivu ya tumbo na kutokwa na damu kidongo (cramping and spotting). dalili hizi zinawezakufana na sana na mwanzoni mwa hedhi, dalili hizi hazimaanishi moja kwa moja utakuwa na ujauzito. Kwani huwenda pia zikasababishwa na uwiyano mbaya wa homoni (hormone imbalance), matumizi ya baathi ya njia za uzazi wa mpango, matumizi ya madawa, misongo ya mawzo, mashambulizi ya bakteria mwilini (PID) na maradhi yanayojulikana kama uterine fibrinoid.5. Uchovu, nadhani hapa sina haja ya kuzungumza sana maana kila mtu anafahamu kuwa uchovu unaweza kusbabishwa na mambo mengi sana kama mazoezi, kazi, maradhi mengine.Hivyo kama unapata dalili za ujauzito na kila ukipima hakuna kitu vyema kufika kituo cha afya kwenda kucheki vyema huwenda kuna kitu haki[o sawa.JE NAWEZA UPIMA UJAUZITO KWA KUTUMIA CHUMVI NA SUKARI?
Haswa hili ni swali zuri, wanawake wengi wamekuwa wakitafuta makala hizi na wanazipata. Namna ya kupima ujauzito kwa kutumia sukari ama chumvi. Ila nikwambie kitu si sukari na chumvi tu balli zipo njia nyingine kama:-Njia nyingine za kupima ujauzito ukiwa nymbani:-
1. Sukari
2. Chumvi
3. Sabuni
4. Mafuta
5. Delto
6. Shampoo
7. Dawa ya mswaki na yingine.Nini kinafanyika. Unachanganya kiasi cha mkojo vyema ukawa wa asubuhi. Unaandaa chombo na kuweka moja kati ya hizo zilizotajwa juu. Unaweza kutumia kijiko kimoja kcha mkojo ama kikombe. Uwiyano wa vilivyotaja juu uwe zawa na mkojo, ama mkojo uziti kidogo. Kisha subiria kwa dakika 5 hadi 10. kama utaona mabadiliko yeyote ya rangi yametokea ama utaona kuna mapovu yanachemka basi takuwa ni mjamzito.Je nji hizi ni sahihi?
Kwa ufupi njia hizi si sahihi kabisa. Haziwezi kukupa majibu ya kweli. Waandishi wengi wameandika lakini ukweli ni kuwa huu ni uwongo. Njia sahihi ni kwenda kupima kwa kipimo maalumu, vinginevyo utapoteza muda bure. Yes wakati mwingine unaweza kupima ukaona mabadiliko na ukawa ni mjamzito kweli. Lakini mabadiliko hayohayo utakayoyaona anaweza kuyaona hata asiye mjamzito.Je watu wa zamani walikuwa wanapimaje ujauzito?NJIA ZA KIASILI WALIZOTUMIA ZAMANI KUPIMA UJAUZITO:1. Kukojoa kwenye nafaka (mbegu za ngano na shayiri)
Tafiti zilizofnywa na wavumbuzi wa mabo ya kale (archeologist) wamegunduwa kuwa yapata miaka 1350 KK kabla ya kuzaliwa Yesu kuwa wanawake wa Misri (Egypt) walikuwa wanapotaka kujuwa kama wamebeba ujauzito walikuwa wakichukuwa viroba vya ngano na shayiri (barley) kisha wanakojolea kiroba chote. Kama ngano itaota basi mwanamke ana ujauziti tena wa mtoto wa kike. Na kama shayiri itaota atakuwa na ujauzito wa mtoto wa kiume. Na kama nafaka hizi hazitaota basi mwanamke hana ujauzito.Ni kuwa katika mwanamke mjamzito kwenye mojo wake kuna homoni ambazo zinachochea ukuwaji wa mbegu. Baada ya kukojolea pishori lile mbegu hazifukiwi, hivyo ztaota mulemule kwenye kiroba kile bila ya kufukiwa kwenye udogo. Miaka ya 1960 wanasayanzi wa leo walifanya tafiti wakagunduwa kuwa njia hii ni sahihi ya asilimoa 70%.2. Kitunguu.
Njia hii ilifanywa na wagiriki mikaa ya zamani sana. Matabibu wa kigiriki walikuwa wanapotaka kujuwa kama mwanmke ana ujauzito walikuwa wakiinguiza kwenye uke wa mwanamke kitunguu na kukiacha humo kwa usiku mzima. Na kama ikifika asubuhi mwanamke akawa anatowa harufu ya kitunguu kwenye mdomo wake basi ana ujauzito. Wagiriki waliamini kuwa mwanamke akiwa na ujauzito uke wake unauwezo mkubwa wa kufyonza vitu. Tafiti hii haikuweza kuthibitishwa na sayansi hili leo.3. Kwa kutumia funguo ama kitasa.
Njia hii ilifanya kwa namna hii, endapo mwanamke anajihisi ni mjamzito alikuwa anachukuwa fnguo ama kitasa kisha anaweka kwenye bakuli kisha anakojowa kiasi cha mkojo kuzamisha funguo ama kitasa kisha anaacha hivyo kwa muda wa masaa matatu. Kama akitowa hakuna mabadiliko ya michubuko ama rangi ana chochote basi mwanamke ni mjamzito. Njia hii [ia haikuweza kuthibitishwa hivi leo.4. Kwa kuangalia rangi ya macho.
Moja katika matabibu wa zamani sana wa kifaransa aliyetambulika kama Jacques Guillemeau yeye aliamini kuwa macho ndio kioo cha mwili, hivyo unaweza kujuwa maradhi na hali ya mwili wa kutumia macho. Aliamini kuwa mwanamke mjamzito macho yake yameingia ndani kidogo, mboni ya macho yake imesinyaa kidogo na mishipa ya neva ilajitokeza pembezoni mwa macho. Wanasayansi wa leo pia wameshindwa kuthibitisha usahihi wa njia hii, ijapokuwa ni kweli mabadiliko yanaweza kutokea kwenye macho ila si kwa kipindi cha mwanzo.5. Njia uliyojulikana kama Piss Prophets
Njia hii ilitumiaka miaka ya 1600, matabibu hawa walikuwa wakipima ujauzito kwa kutumia kuangalia mkojo. Hawa waliamini kuwa mkojo wa mjamzito unakuwa ni msafi naani hauna uchafu, una rangi ya limao bivu lililopauka lakini unakuwa na ukungu kwa mbali juu yake. Pia matabibu hawa hawakuishia hapa walikuwa wakiangalia uwepo wa maradhi engine kwa kuangalia mkojo. Wanasayansi wa leo pia wameshindwa kuthibitisha usahihi wa njia hii.6. Kwa kutumia riboni:
Njia hii ilikuwa na mzunguruko kidogo, nikuwa mwanamke anapojihisi ni mjamzito anakwenda kwa tabibu. Tabibu atamwambia akojoe kwenye beseni, kisha tabibu atachukuwa riboni na kuitia kwenye beseni lenye mkojo. Baada ya muda ataitoa na kuikausha, kisha ataichoma mbele karibu na mwanamke. Kama harufu ya riboni itamfanya mwanamke ahisi kichefuchefu basi atakuwa ana ujauzito. Wanasayansi waleo pia hawakuweza kuthibitisha njia hii.7. Kwa kutimia Sungura ama wanyama wadogo wadogo kama panya.
Njia hii iligunduliwa miaka ya 1900 na matabibu waliojulikana kwa majina ya Bernhard Zondek na Selmar Aschheim. Hawa miaka ya 1940 waliamini kuwa mkojo wa mjamzito ukiingizwa kwenye mwili wa vijinyama vidogo basi ovari zao huwa kubwa. Baadaye jaribio hili lilijikita sana kwa kutumia sungura. Wanasayansi wa leo walionyesha kuwa njia hii ilikuwa na ukweli kiasi japo sio njia nzuri maana ilihitajika kumuuwa sungura ili kuchunguza kama ovari zimekuwa kubwa.8. Kwa kutumia chura.
Njia hii ilianza kutumika Afrika ya Kusini. Wao walikuwa wakutumia chura wa kike. Waliamini kuwa endapo chura wa kieke akichomwa sindano yenye mkojo wa mwanamke mjamzito, basi chura huyo atataga mayai ndani ya masaa 12.Njia nyingine:
9. Kuangalia mwendo, yaani jinsi anavyotembea mjamzito ni tofauti na mwanamke asiye mjamzito.
10. Kwa kuaangalia ongezeko la mapigo ya moyo. Kama mapigo ya moyo yameongezeka basi mwanamke ana ujauzito.Njia zilizotajwa hapo juu zilikuwa zukitumika katika nyakati zake na zilionekana kusaidia kwa wakati ule. Ni kweli njia hizo zina madhaifu makubwa lakini si kila wakati zilikuwa zikikosea. Wakati mwingine zilikuwa zikipatia, ni kwa sababu mwanamke alikuwa ni mjamzito kweli. Hata hivyo ilibidi pia kuangalia dalili nyingine za ujauziti ndipo tabubu alikuwa akitoa jibu.HATUA KUU TATU ZA UKUAJI WA MIMBA.
Ujauzito umegawanyika katika hatua kuu tatu, au vipindi vikuu vitatu ambavyoni:-
1. trimester ya kwanza (first trimester)
Hiki ni kipindi katia ya wiki 1 mpaka 12 yaani ndani ya miezi mitatu ya kwanza. Kipindi hiki mjamzito awe makini sana kwani ni kipindi ambacho kutoka kwa ujauzito ni rahisi sana. Kipindi hiki ndicho ambacho mtoto anaanza kukuwa ubongo, uti wa mgongo na viungo vingine ama moyo na masikio. Tafiti zinaonyesha kuwa takribani asilimia 85 ya mimba zinazotoka huwa zinatoka katika kipindi hiki. Hata hivyo wanaotowa mimba pia hutoa katika kipindi hiki.Mabadiliko ya mwili katika kipindi hiki
A. Uchovu
B. Kukosa haja kubwa
C. Kichefuchefu
D. Maumivu ya kichwaNini hakitakiwi kufanyika katika kipindi hiki?
A. Wacha kuvuta sigara
B. Wacha kunywa pombe
C. Wacha kutumia dawa kiholela bila ya ushauri wa daktari
D. Kuwa makini sana kwani kosaadogo ujauzito upo hatarini
E. Punguza kuchwa chai kupitiliza
F. Punguza kula samaki kwenye magobeta jaamii ya tondo
2. Trimester ya pili (second trimester)
Kipindi hiki ni kati ya wiki 13 mpaka 27 yaani kuanzia mwezi wa 3 mpaka wa 6 kwenda wa saba. Katika kipindi hiki mwanamke atafanyiwa vipimo vya utrasound kuangalia mkao wa mtoto na kama yupo katika afya njema. Katika kipindi hiki hata jinsia ya mtoto itaweza uonekana kwa ambaye anataka kuiona kwenye kipimo cha utrasound. Hapa mtoto anaweza kuishi nje ya mwili wa mama yake kuanzia wiki ya 23. na endapo mtoto atazaliwa hapa atakuwa njiti hivyo vifaa maalumu vitahitajika kumlea kabla ya kuanza kuishi huru. Katika kipindi hiki mama mjamzito atasikia vurugu za mtoto tumboni, kupiga mateke, kugeuka na nyinginezo.Katika kipindi hiki karibia dalili zote za ujauzito za mwanzo hupotea. Nguvu itarudi vyema na utawza kulala usingizi mnono usiku. Katika kipindi hki tumbo litaanza kuonekana kukuwa. Katika kipindi hiki jiepushe sana yafuatayo:-
A. Kuvaa nguo za kubana
B. Kuwa na hasira mara kwamara. Yaani jitahidi kkutafuta furaha, kaa na maafiki cheka na furahia.
C. Usikibane tumbo hata likiwa kubwa vipi.Katika kipindi hiki unawezakuhisi kuingulia mra kwa mara, na maumivu ya miguu. Hamu ya kula inawea kuongezeka, na uzito pia kuongezeka katika kipindi hiki. Katika kipindi hiki mwanamke anaweza kupatwa na maumivu ya mgongo. Hata hivyo anaweza kujihisi kama ana mafua ama pua zimeziba ila akifina hakuna kitu. Pia anaweza kuiona mishipa inatokeza kwa nje hasa kwenye miguu.Katika kipindi hiki mama mjamzito ataanza kusikia mijongeo ya mtoto. Hata hivyo mtoto ataweza kuitambuwa sauti ya mama yake na watu wa karibu sana na mama yake. Baadhi ya viungo vinavyoweza kuonekana kwenye utrasound katika kipindi hiki ni kama figo, mapafu, moyo na ubongo na jinsia. Katika kipindi hiki mama mjamzito anaweza kupimwa kisukari cha mimba kuanzia wiki ya 26 mpaka 28.3. Trimester ya tatu (third trimester)
Kipindi hiki huanzia wiki ya 28 mpaka 40, yaani kuanzia miezi 7 kwa makadirio. Katika kipindi hiki mara kwa mara utahitajika kumuona daktari kwa vipimo zaidi. Daktari atakuwa anakuangalia maendeleo yako kwa jumla na afya ya ujauzito wako. Atakuwa anakucheki:-
A. Anapima mkojo kuangalia protini
B. Atakuwa analkuangalia shinikizo la damu (presha)
C. Atasikiliza mapigo ya moyo wa mtoto
D. Atakuwa akipima njia ya uzaziatakuwa acheki miguu na mikono kama itakuwa inavimba.Pia daktari anaweza kukupima uwepo wa bakteria wanaoitwa Group B streptococcus (GBS) kwenye uke. Uwepo wa bakteria hawa unaweza kuhatarisha afya ya mtoto anayezaliwa. Katika kipindi hiki ni vyema kuanza kufuatilia habari za kujifungua, mazoezi ya kujifungua na namna ya kujiandaa.

KUTOKA KWA UJAUZITO, DALILI ZAKE NA SABABU ZAKE.
Kutoka kwa ujauzito mara nyimgi hutokea katika hiki kipindi cha kwanza yaani ndani ya wiki 12 za mwanzo. Inakadiriwa kuwa robo ya mimba hutoka. Mwanamke anaweza akatokwa na mimba kwa kujuwa ana bila ya kujuwa. Inaweza kutokea pia mwanamke akabeba ujauzito na ukatoka bila kuwa na habari yeyote kama alikuwa na miba na imetoka. Ni kuwa mimba inaweza kutoka bila ya kuwa na dalili za wazi kama kutoka na damu.Dalili za kutoka kwa mimba:
A. Maumivu ya mgongo
B. Kuharisha
C. Kichefuchefu
D. Maumivu ya maeneo ya nyonga na kiuno kama unahisi unataka kuingia kwenye siku zako
E. Maumivu makali ya tumbo
F. Kutokwa na majimaji kwenye uke.
G. Kutokwa na vitu kama vijioande vya nyama vijidogo kwenye uke
H. Uchovu mkali sana usio na sababu
I. Kupotea kwa dalili nyingine za ujauzito
J. Kutokwa na damu mabonge manonge ama damu nyingiKumbuka hizi ni dalili tu, unaweza kuwa nazo na ujauzito ukawa salama kabisa. Ukiona unahisi dalili hizo muone daktari atathibitisha vyema kwa vipimo ikiwemo utrasound ama kuangalia kiwango cha homoni ya ujjauzito kwneye damu yako.Ni zipi sababu za kutoka kwa mimba?
Mara nyingi kutoka kwa ujauzito kunaweza kusababishwa na chromosomal abnormalities. Hili ni tatizo la kigenetics. Hapa seli za mtoto zinashindwa kugawanyika vyema na kukuza mtoto. Sababu nyingine za kutoka ujauzito ni:-
A. Matatizo katika homoni kuwa nyingi sana ama kidogo sana
B. Kama mama mjamzito ana kisukari na hafuati masharti vyema
C. Mazingira yanaweza kuchangia kama kuna mionzi hatari kama ya madini ya uranium
D. Maambukizi na mashambulizi ya vijidudu kama bakteria kwenye via vya uzazi.
E. Shida katika mlango wa uzazi (cevix)
F. Kutumia madawa kiholela ama kutumia madawa kusudi kwa lengo la kutoa ujauzito
G. Ugonjwa wa endometriosis (kuvimba kwa kuta za mji wa mimba "uterus")
H. Magonjwa ya ngono kama gonoriaSababu nyingine za kutoka kwa mimba
A. Utapia mlo
B. Kuwa na kitambi
C. Matumizi ya vilevi na sigara
D. Maradhi ya tezi ya thyroid
E. Shinikizo la damu la juu sana
NITAZUIAJE MIMBA KUTOKA?
Mimba nyingi zinazotoka husababishwa na genetics ama mambo ya kiafya ambayo si rahisi kuzuilika. Hivyo kwa mimba hizi ni ngumu sana kuzuia kutoka kwake. Hata hivypo kitu ambacho unaweza kukifanya ni kuhakikisha kuwa unabakia katika afya salama kabla na baada ya kubeba ujauzito. Fafya mabo yafuatayo yatasaidia katika kuboresha afya yako na kuzuia kiutoka kwa ujauzito:-A. Kula mlo kamili wenye virutubisho (balanced diet)
B. Fanya mazoezi mara kwa mara. Si lazima eti mazoezi ya kukutoa mijasho, unaweza kufanya mazoezi ya viungo pia hata ukiwa kitandani.
C. Wacha ama punguza kutumia pombe, sigara ama dawa za kulevya.
D. Punguza unywaji wa chai kama unakunywa kwa wingi kupitiliza. Hapa ninazungumzia chai ya majani ya chai ambayo ina caffein.
E. Fanya uchunguzi wa afya yako mara kwa mara.
F. Wacha kutumia dawa kiholela
G. Jiepushe na mambo ambayo yataweza kuwa ni hatari kwa ujauzito kama kupigana ama miereka.
H. Fuata maelekezo vyema kutoka kwa wahudumu wa afya.MAJIMAJI YANAYOTOKA UKENI WAKATI WA UJAUZITO
Majimaji yanayotoka ukeni wakati wa ujauzito (Damu na uteute)
Ni kawaida kwa mjamzito kushuhudia kwenye uke wake kutokwa na kama uteute na huongezeka kila mimba inapoendelea kukomaa. Wakatiflani anaweza kuona nguo zake zina madoa ya damu, ama akashuhudia matone kadhaa ya damu. Wapo pia wanaingia hedhi kwa damu chache. Sasa hebu tuangalie kwa ufupi hali hizi:-1. Baada ya kutoka hedhi uke wa mwanamke unakuwa mkavu bila ya kuwa na utelezi telezi. Hiki ni kipindi ambacho mwanamke hawezi kubeba ujauzito. Katika kipindi hiki hata akitia kidole hakitoki na utelezitelezi. Kipindi hiki kinaweza kuchukuwa takribani siki tano hadi 10 inategemea na mzunguruko wa mwanamke. Huu ni kuda mzuri wa kushiriki tendo kwa wale ambao hawahitaji kulea ujauzito.2. Zitakapoanza kuingia siku hatari mwanamke ataanza kuhisi uwepo wa uteute kwenye uke wake anapotia kidole kwa ndani. Siku hizi pia zinatofautiana kulingana na idadi ya mzunguruko. Ila zinaweza kuazia siku ya 11 hadi 14 inaweza pia kuwa chini ya papo lwa baadhi ya wanawake ama juu ya hapo.3. Siku moja kabla ya kukomaa kwa yai na kuwa tayari kwenye mirija ya falopian tayari kutungisha mimba, uteute huu huongezeka zaidi. Sifa za uteute huu ni kuwa ni wenye kuteleza sana ila sio mzito na wenye kunatanata ama kuvutikana. Kwa wanaotumia njia za uzazi wa mpango hasa zile za homoni uteute wao upo muda wowote kwa hiyo ni ngumu sana kwao kuiona hali hii.4. Siku ya hatario zaidi mwanamke atapata mabadiliko ya hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa. Yaani hamu itaongezeka zaidi siku hii kuliko siku iliyotangulia. Hapa kwa wale ambao hawataki ujauzito sio siku salama kwao kushiriki tendo landoa.5. Uteute huu katika siku hizi kuandaliwa kwa ajili ya kusaidia mbegu za kiume ziweze kusafiri vyema, kuogelea vyema na kulifikia yai. Pia kuhakikisha kuwa mbegu za kiume haziathiriwi na asidi ya tumboni kwa mama kwa kiasi kikubwa. Hivyo uteute huu katika kipindi hiki ni muhimu sana.6. Kali hii inaweza kudumu kwa masiku kadhaa toka 14 hadi 17 kwa makadirio inaweza kupungua ama kuongezeka kulingana na mzunguruko wa mwanamke. Baada ya hapo kama mwanamke alibeba ujauzito majimaji haya yanaongezeka uzito saa na kuwa yenye kunata na kufanana na utelezi wa yai pindi unapolibanja. Baada ya mimba majimaji haya yataendelea kutoka na kuongezeka na kuwa mazito zaidi hadi atakapojifungua.Katika ujauzito majimaji haya yanakazi ya kulinda njia ya kuingilia kwenye mji wa mimba dhidi ya mashambulizi na aambukizi ya bakteria. Yaani kuhakikisha kuwa hakuba bakteria ama fangasi atakayeweza kuingia na kumzuru mtoto tumboni.7. Kama hakuna ujauzito uliobebwa majimaji yataanza kurudi kutoka hali yake ya kawaida na kuwa safi, yenye harufu kwa mbali ila si harufu ya kukera, pia yanaweza kuwa na rangi ya maziwa hivi.Majimaji haya pia nayaweza kuashiria shida kwenye afya endapo yatakuwa na sifa hizi:-
A. Yana rangi ya njao, kijani ama buluu
B. Yana harufu kali mbaya
C. Yanakusababishia muwasho kwenye uke na mashavu ya uke
D. Yanakusababishia kuvimba kwa uke na mashavu ya uke8. Ama kuhusu kutokwa na damu, ikiwa chache ni kawaida. Ikiwa unaambatana na maumivu makali ya tumbo, ama maumivi makali ya kichwa na homa, basi vyema kumuona daktari kwa ushauri zaidi. Kama nilivtotangulia kusema kuna wanawake wanapata hedhi wakiwa wajawazito. Wenyewe wanaita kupunguzia, kwa ufupi hii si hedhi na pia haiashirii kama kuna tatizo. Ila kama inatoka nyingi na kuambatana na maumivu yasiyo ya kawaida ni vyema kumuona daktari.UTIJe! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 713


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-