Vyakula vyenye protini kwa wingi


image


Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula vyenye protini kwa wingi


VYAKULA VYENYE PROTINI KWA WINGI

 

 

Tunaweza kupata protini kwenye mimea jamii ya mikunde kama kunde na maharagwe. Pia kiasi kikubwa cha protini tunaweza kukipata kwa kula mayai, nyama, samaki, dagaa na maziwa. Pia tunaweza kupata protini kwa kula nafaka kama mchele na nafaka zingine. Ulaji wa mboga za majani unaweza pia kutupatia protini kwa kiasi kidogo. Wadudu kama kukbikukbi, senene na wengineo pia wanaweza kutupatia protini.

 

Kwa kifupi vyakula vinavyotupatia protini ni pamoja na :-

 

1.Samaki; samaki ni chanzo kizuri cha protini. Samaki wenye mafuta kama salmon ni vyanzo vyema zaidi vya protini. Ulaji wa samaki umekuwa ni chanzo kizuri cha protini hasa kwa wakazi wa maeneo ya baharini na maeneo ya pwani ama mitoni, mabwawa na maziwa. Tunaposema samaki hapa wanaingia mpaka dagaa, kaa, kaji, kamongo, perege, mikunga, papa na samaki wengine. Pia ulaji wa samaki ni muhimu kwa afya ya ubongo, kukinga mwili dhidi ya maradhi mbalimbali, chanzo cha madini ya chumvi na fati

 

2.Mayai; mayai ni katika vyanzo vikubwa vya protini. Karibia watu wengi hujipatia protini kwa kula mayai. Unaweza kula yai likiwa limekaangwa, chemshwa ana la kuchoma. Pia unaweza kula yai bichi kama wafanyavyo baadhi ya watu. Ulaji wowote kati ya niliotaja unaweza kukupatia protini. Ila hakikisha kama umelikaanga ama kulichoma halikauki sana likawa kama chapati iliyokauka, upishi huu unaweza kuathiri virutubisho.

 

.3. Maziwa; maziwa ni katika vyanzo vikuu vya protini kwa binadamu na wanyama. Maziwa ya mama ni chanzo kipekee kilicho salama zaidi kwa mtoto mchanga kuliko hata ya ng’ombe. Tofauti na kutupatia protini maziwa pia ni chanzo cha vitamini na fati. Maziwa ni katika vyakula vilivyokusanya viinilishe vyote muhimu. Ni vyema kuyachemshha maziwa kabla ya kuyanywa ili kuepuka baaadhi ya matatizo ya kiafya.

 

4.Nyama; tunaweza kupata protini kwa kiasi kikubwa kwa kula nyama. Nyama ni katika vyanzo vizuri vya protini. Inaweza kuwa nyama nyekundu ama nyama nyeupe. Nyama nyeupe tunaweza kuzipata kwa kula kuku, baadhi ya samaki, kaa. Nyama nyekundu tunaweza kupata kwa kula mbuzi, kondoo na karibia wanyama wengi. Nyama pia ni chanzo kizuri cha fati mwilini. Ulaji wa nyama unaweza kuleta athari za protini kwa muda mchache sana.

 

5.Mimea aina ya kunde na nafaka; mimea jamii ya kunde hii ni mimea ambayo inatambaa kama kunnde na maharagwe na mimea jamii hii. Mimea hii inatambulika kuwa na kiasi kikubwa cha protini. Watu wenye kipato cha chini mimea hii ni chanzo chao cha msingi cha kupata protini. Maharagwe yapo katika aina nyingi yapo ya soya na aina mbalimbali. Ulaji wa aina zote hizi unaweza kutupatia protini.

 

6.Mboga za majani. Kwa kiwango kilicho kidogo tunaweza kupata protini kwa kula mboga za majani. Mboga za majani oekee hazitoshelezi kutupatia kiwango cha protini kinachohitajika. Kwa wale ambao hawali chama (vegetarian) wapo ambao hawali nyama lakini wanakula mayai na maziwa hawa wanaweza kujipati protini kwenye mayai na maziwa. Lakini kwa wale ambao hawali nyama, maziwa wala mayai watahitajika kupata vyamzo vingine mbadala vya protini yaani watumie protini za kutengeneza japo miongoni mwazo zipia mbazo zinatengenezwa kwa wanyama.

 

7.Vyanzo vingune: tofauti na vyanzo vya protini nilivyotaja hapo juu lakini pia kuna vyanzo vingine kama ulaji wa senene na kumbikumbi na wanaofanana. Kuna baadhi ya jamii zinakula senene hasa jamii zinazopatikana maeneo ya kagera. Kwao senen ni chanzo kizuri sana cha protini. Kumbikumbi nao hupatikana maeneo mengi na jamii nyingi zinatumia chakula hiki.



Sponsored Posts


  ðŸ‘‰    1 Maktaba ya vitabu       ðŸ‘‰    2 Madrasa kiganjani       ðŸ‘‰    3 Magonjwa na afya       ðŸ‘‰    4 Hadiythi za alif lela u lela       ðŸ‘‰    5 Mafunzo ya html kwa kiswahili       ðŸ‘‰    6 Jifunze fiqh    





Je una umaswali, maoni ama mapendekezo?
Download App yetu kuwasiliana nasi




Post Nyingine


image Vyakula vyenye madini kwa wingi
Somo hili linakwenda kukuletea baadhi ya vyakula vyenye madini kwa wingi Soma Zaidi...

image Hasara za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito
Posti hii inahusu zaidi hasara za kitunguu swaumu wakati wa ujauzito. Soma Zaidi...

image Vyakula salama kwa mwenye kisukari
Somo hili linakwenda kukuletea orodha ya vyakula salama kwa mwenye kisukari Soma Zaidi...

image Dalili za upungufu wa vitamini C mwilini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za upungufu wa vitamini C mwilini Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula maini
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula maini Soma Zaidi...

image Vyakula vinavyosaidia katika kusafisha ini
Post hii inahusu zaidi baadhi ya vyakula ambavyo vinaweza kutumika ili kuweza kuweka ini kwenye hali yake ya kawaida. Soma Zaidi...

image Fahamu vyakula vya nyuzinyuzi
Posti hii moja kwa moja inaenda kuelezea vyakula vya nyuzinyuzi zinazopatikana kwenye matunda na mboga mboga. Soma Zaidi...

image Faida za kitunguu maji/ onion
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu umuhimu wa kitunguu maji mwilini Soma Zaidi...

image Faida za kiafya za kula biringanya (eggplant)
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula biringanya eggplant) Soma Zaidi...

image Madhara ya chakula kutosagwa vizuri tumboni.
Posti hii inahusu zaidi madhara ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni, haya ni madhara ambayo utokea kwa sababu ya chakula kushindwa kumengenywa vizuri tumboni. Soma Zaidi...