Faida za kula Pilipili

Faida za kula Pilipili

Usiogope kuwashwa, kula pilipili ni nzuri kwa afya yako ia virutubisho vingi sana

Faida za kula Pilipili

14.Pilipili kali. Watu wengi wamekuwa wakiacha kutumia pilipili etu kwa sababu ya ukali wake. Ila itambulike kuwa ijapokuwa ni kali lakini ila faida nyingi sana kwa afya ya mtu. Pilipili pia ina vitamini c ndani yake kwa kiasi. Vitamini hivi ni muhimu sana katika mfumo mzima wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa na wadudu shambulizi.

Pilipili zote zina vitamin A, C na K lakini pilipili nyekundu zimezidi wenzie. Wataalamu wa afya wanazungumza kuwa antioxidant, vitamin A na C vilivyomo kwenye pilipili husaidia katika kuzuia maradhi ya saratani na baadhi ya maradhi yanayohusiana na kuzeheka, na pia husaidia katka kuboresha mfumo wa kinga. Pia vitamin K husaidia katika kuganda kwa damu, kuimarisha mifupa pia husaidia katika kulinda seli.

Pilipili nyekundu ni chanzo kizuri cha carotenoid ambayo hutambulika kama lycopene, hii ni mujarabu sana katika kuzuia mwili kupata maradhi ya saratani ya kibofu, njia ya uzazi kwa kinamama na saratani ya kongosho.pia kuna carotenoid inayotambulika kama cryptoxanthin hii nayo hujulikana kwa uwezo wake wa kupambana na kuzuia mwili kupata saratani ya mapafu inayohusiana na uvutaji wa sigara.

Wataalamu wa afya wanatueleza kuwa pilipili husaidia katika kurekebisha mapigo ya moyo na kuongeza joto la mwili kwa muda wa dakika 20 baada ya kuila. Hii inaonesha kuwa mwili utakuwa na uwezo wa kuunguza mafuta na cholesteral za ziada kwa muda huo. Pia tafiti nyingine zinaonesha kuwa pilipili husaidia katka kupunguza athari za vidonda vya tumbo kwani husaidia katika kuuwa bakteria ndani ya tumbo.

Ndani ya pilipili kuna antioxidant iitwayo piperine. Wataalamu wa afya wanadai kuwa ulaji wa antioxidant husaidia katika kuimarisha afya ya mtu. Piperine inatambulika kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kudhibiti na kulinda uharibifu wa seli. Pia ulaji wa pilipili husaidia katika kuimarisha afya ya ubongo.

Kwa ufupi pilipili husaidia sana kwa afya ya mlaji. Pia pilipili husaidia katika kuulinda mwili dhidi ya maradhi ya kisukari, saratani na maradhi ya moyo. Afya ya ubongo, kuimarisha mapigo ya moyo pamoja na kupunguza mgando wa mafuta kwenye mirija ya damu. Pilipili husaidia katika kuufanya mwili uweze kunyonya virutubisho muhimu kutoka kwenye chakula.


                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF Views: 3990

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Dua za Mitume na Manabii     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 ai web app     👉6 Bongolite - Game zone - Play free game    

Post zinazofanana:

je ni vipi vyakula vyenye protini kwa wingi?

Makala hii iatakuletea aina kuu tano za vywkula vyenye protini nyingi zaidi. Kama ulikuwa unajiuliza kuwa ni vyakula ipi hasa vinaweza kukupatia protini kwa wingi ni vipi, makala hii ndio majibu yako kwa swali hilo.

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula kunazi/ lote tree

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula kunazi/ lotetree

Soma Zaidi...
Vyakula vya wanga

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu aina za vyakula vya wanga na umuhimu wake mwilini

Soma Zaidi...
Virutubisho vya mwili

Posti hii inahusu zaidi virutubisho vya mwili, ni aina tano za vyakula ambayo ufanya kazi mbalimbali kwenye sehemu za mwili wa binadamu.

Soma Zaidi...