image

FAIDA ZA MATUNDA NA MBOGA MBALIMBALI KWA AFYA

FAIDA ZA MATUNDA Makala hii inakwenda kukuletea faida za matunda mbalimbali na mboga upatikanaji wake na faida zake kiafya.

FAIDA ZA MATUNDA NA MBOGA MBALIMBALI KWA AFYA

Ijue mboga na matunda na faida zake kwa afya yako

Bongclass-afya

FAIDA ZA MATUNDA NA MBOGA MBALIMBALI KWA AFYA

FAIDA ZA MATUNDA
Makala hii inakwenda kukuletea faida za matunda mbalimbali na mboga upatikanaji wake na faida zake kiafya. Pia utakwenda kuona matunda na mboga ambazo ni kinga dhidi ya maradhi hatari kama kisukari, saratani, maradhi ya moyo na mfumo wa fahamu pamoja na afya ya ubongo.


1.Faida za kula zabibu:
1.zabibu lina virutubisho vingi kama vitamini C , B6 na K na fat na madini ya shaba na manganese.
2.Ina antioxidanti zinazohusika kuondoa sumu za kemikali na vyakula mwilini
3.Hupunguza athari ama hatari ya magonjwa kama saratani, kisukari na maradhi ya moyo na mishipa ya damu
4.Huondoa stress na misongo ya mawazo
5.Hushusha shinikizo la damu
6.Hupunguza cholesterol mbay
7.Hushusha kiwango cha sukari kwenye damu
8.Husaidia kuimarisha afya ya macho
9.Huimarisha afya ya ubongo na utunzaji wa kumbukumbu
10.Husaidia kuboresha afya ya mifupa
11.Husidia kupunguza maambukizi ya baadhi ya bakteria, virusi na fangasi
12.Hupunguza kuzeheka mapema


2.Faida za kula nanasi
1.Nanasi lin virutubisho kama fati, protini, vitamini C, vitamini B6, madini ya chuma, manganeseum na shaba.
2.Hupunguza misongo ya mawazo (stress)
3.Nanasi ni rahisi kumeng’enywa tumboni
4.Hupunguza hatari ya ugonjwa wa saratani
5.Huboresha na kuimarisha mfumo wa kinga mwilini
6.Hupunguza maumivu ya viungio
7.Husaidia kupona haraka baada ya kufanyiwa upasuaji
8.Ni tunda tamu


3.Faida za kula palachichi
1.palachichi lina virutubisho kama wanga, vitamini C, E, K na B^. pia lina madini ya managesium na potassium.
2.Husaidia kuboresha na kuimarisha afya ya moyo
3.Huzuia kupata ugonjwa wa mifupa (kuwa dhaifu na kufunjika kwa urahisi)
4.Huzuia ama kupunguza kupata ugonjwa wa saratani
5.Huboresha afya ya watoto wadogo na ukuaji wao
6.Hupunguza misongo ya mawazo
7.Huondoa tatizo la kutopata choo kikubwa
8.Husaidia kuondoa sumu za vyakula na akemikali mwilini
9.Husaidia kuzuia maambukizi ya mara kwa mara ya virusi, bakteria na fangasi
10.Husaidia kuzukupata maradhi ya kisukari


4.Faida za kula epo (tufaha)
1.Tufaha lin virutubisho kama vitamini C, K, A, E, B1, B2 na B6. pia lina madini ya potassium.
2.Husaidia katika kupunguza uzito wa ziada mwilino
3.Husaidia kuboresha na kuimarisha afya ya moyo
4.Hupunguza athari za kisukari
5.Husaidia kuzuia saratani
6.Husaida kupambana na pumu
7.Husaidia kuboresha na kuimarisha afya ya mifupa
8.Hulinda tumbo dhidi ya majeraha kutokana na matumizi ya madawa
9.Husaidia kuimarisha afya ya ubongo


5.Faida za Embe
1.huzuia tatizo la kukosa choo kikubwa
2.Huimarisha mfumo wa king
3.Embe ni zuri kwa afya ya macho
4.Hupunguza cholesterol mbaya
5.Huboresha muonekano wa ngozi na kuifanya iwe na afya njema
6.Embe ni zuri hata kwa wenyye kisukari
7.Husaidia katika kupunguza uzito


6.Faida za limao ama ndimu na limao
1.hupunguza hatari ya kupata ugonjwa wa stroke yaani kiharusi unaopelekea kupapapaizi
2.Kushusha presha ya damu
3.Huzuia kupata saratani
4.Husaidia kuboresha afya ya ngozi
5.Huzuia kuata pumu
6.Husaidi katika ufyonzwaji wa madini ya chuma
7.Huboresha na kuimarisha mfumo wa kinga
8.Husaidia katika kupunguza uzito
9.Ni chanzo kizauri cha vitamini C
10.Lina virutubisho kama vitamini C, madini ya chuma, potassium, phosphorus na manganessium
11.Hilinda mwili dhidi ya maradhi ya kiseyeye


7.Faida za kula tikiti
1. hufanya mwili uwe na majimaji mengi na hii ni faida kubwa sana kiafya
2. Tikiti lina virutubisho kama vitamini C, A, B1, B5, na B6. Pia lina madini ya manganessium na potassium
3. Husaidia kuzuia saratani
4. Huimarisha afya ya moyo
5. Hupunguza misongo ya mawazo
6. Hupunguza udhaifu wa viungo kwa wazee
7. Husaidia kuboresha afya ya nywele na ngozi
8. Huimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula


8.Faida za Chungwa na Chenza (tangarine)
1.ni chanzo kizuri cha vitamini C
2.Huboresha mfumo wa kinga mwilini
3.Huzuia uharibifu wa ngozi
4.Huboresha presha ya damu
5.Hususha cholesterol mbaya
6.Husaidia kudhibiti kiwango cha sukari
7.Hupunguza hatari ya kupata saratani
8.Husaidia kuboresha afya ya macho
9.Huzuia tatizo la kufunga kwa choo


9.Faida za kula ndizi
1.ni chanzo kikuu cha vitamini B6
2.Pia ni chanzo kizuri cha vitamini C
3.Ndizi ni nzuri kwa afya ya ngozi
4.Madini ya postassium yaliyopo ndani ya ndizi husaidia kuboresha afya ya moyo na presha ya damu
5.Husaidia katika kuboresha na kuimarisha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
6.Ndizi humpatia mlaji nguvu
7.Ndizi zina virutubisho vingine kama protini, fati na madini
8.Huthibiti kiwango cha sukari kwenye damu
9.Husaidia katika kupunguza uzito zaidi
10.Huondosha sumu za vyakula mwilini
11.Husaidia katika kuimarisha afya ya figo


10.Faida za kula papai
1.hupunguza cholesterol mbaya
2.Husaidia katika kupunguza uzito
3.Huimarisha mfumo wa kinga
4.Ni tunda zuri kwa wenye kisukari
5.Husaidia kuboresha afya ya macho
6.Huondoa tatizo la kuziba wa choo ama kutokubata choo
7.Huzuia kuzeheka kwa haraka
8.Huzuia mwili kupata saratani


11.Faida za kiafya za nyanya
1.ni chanzo kizuri cha virutibisho kama protini, sukari, fat na pia nyanya zinatupatia maji
2.Pia ni chanzo cha vitamini C, K1 na B9. Pia tunapata madini ya potassium
3.Ni nzuri kwa afya ya moyo
4.Huzuia kupata saratani
5.Ni nzuri kwa fya ya ngozi
6.Ni nzuri kwa afya ya macho
7.Huzuia tatizo la kukosa choo
8.Ni nzuri kwa wenye kisukari


12.Faida za kiafya za Tangawizi
1.huondoa sumu za vyakula na kemikali mwilini
2.Huondoa kichefuchefu hasa kwa kichefuchefu cha mimba
3.Hupunguza maumivu ya viungio na misuli
4.Hupunguza maambukizi ya mara kwa mara
5.Huimarisha afya ya moyo
6.Hushusha kiwango cha sukari kwenye damu
7.Hutibu tatizo la kukosa hamu ya kula na kukosa choo
8.Hupunguza maumivu ya tumbo la chango kwa wakinamama
9.Hushusha kiwango cha cholesterol
10.Huzuia saratani
11.Huimarisha afya ya ubongo hasa kwa wazee


13.Faida za kiafya za kitunguu thaumu
1.ina chembechembe za salfa ambazo ni dawa kubwa kwa afya ya mtu
2.Kuna virutubisho kama vitamini C na vitamini B6, pia madini ya manganese
3.Hupunguza usingizi
4.Hupambana na mafua
5.Hushusha presha ya damu
6.Huboresha afya ya moyo
7.Huborsha afya ya ubongo na kuondoa tatizo la kusahausahau
8.Huondosha sumu za vyakula na kemikali mwilini
9.Huboresha afya ya mifupa


14.Faida za kula pilipili
1.kuondosha kemikali mbaya mwilini
2.Hupunguza uwepo wa uvimbe mwilini
3.Huboresha afya ya ubongo
4.Hudhibiti kiwango cha sukarai mwilini
5.Hupunguza choleserol mbaya mwilini
6.Husaidia katika kupambana na saratani
7.Husaidia mwili katika kufyonza virutubisho kwenye chakula
8.Hupunguza maumivu
9.Hupunguza hamu ya kula


15.Faida za karoti
1.karoti ina virutubisho kama sukari, fati, protini, vitamini A, B, K na madini ya potassium.
2. Hupunguza hatari ya kupata saratani
3.Hususha cholesterol
4.Husaidia kupunguza uzito
5.Husaidia kuboresha afya ya macho
6.Karoti ni nzuri kwa afya ya mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
7.Husaidia kudhibiti ugonjwa wa kisukari
8.Husaidia kulinda na muimarisha afya ya moyo na mishipa ya moyo
9.Husaidia kuboresha na kuimarisha mfumo wa kinga mwilini
10.Karoti ni nzuri kwa afya ya mifupa


17.Faida za kiafya za kula Tango
1.tango lina virutubisho kama fati, protini, pia lina vitamini K na C pia kuna madini ya manganese na manganessium
2.Huondosha kemikali na sumu ndani ya vyakula
3.Hsaidia kuipa maji miili yetu
4.Husaidia kupunguza uzito mwilini
5.Husaidia kushusha sukari mwilini
6.Husaidia katika kupata choo vizuri


18.Faida za kiafya za nazi
1.nazi ina fati iliyo salama kwa afya (fatty acid)
2.Husaidia katika kuimarisha na kuboresha afya ya moyo
3.Husaidia katika uunguzwaji wa mafuta mwilini
4.Hupunguza njaa
5.Hupunguza kifafa
6.Huongeza cholesterol zilizo nzuri
7.Hulinda afya ya ngozi, nywele na meno
8.Huimarisha afya ya ubongo
9.Hupunguza mafuta mabaya kwenye tumbo (kitambi)


19.Faida za kiafya za kula maboga
1.boga lina virutubisho kama vitamini A, C, E na B. pia kuna madini ya chuma, potassium na manganessium. Pia boga lini protini na fati.
2.Boga lin antioxidanti ambazo huondosha sumu za vyakula na kemikali mwilini
3.Boga husaidia kuimarisha na kuboresha mfumo wa kinga
4.Husaidia kwa afya ya macho
5.Husaidia kupunguza uzito
6.Hupunguza athari ya kupata saratani
7.Husaidia katika kuimarisha afya ya moyo
8.Boga husaidia kuboresha afya ya ngozi
9.Hupunguza kuganda kwa choo


20.Faida za mbegu za maboga
1.mbegu za maboga zina virutubisho kama protini, fati, vitamini K na madini ya zink, shaba, manganese na manganessium.
2.Zina antioxidant ambazo hulinda seli dhidi ya uharibifu
3.Husaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani
4.Huimarisha afya ya korodani na kibofu
5.Husaidia kuboresha afya ya moyo,
6.Hudhibiti kiwango cha sukari
7.Ni nzuri kwa afya ya mifupa
8.Huzuia tatizo la kuziba kwa choo
9.Huongeza wingi wa mbegu za kiume
10.Husaidia katika kupata usingizi mwororo


21.Faida za kiafya za kula uyoga
1.uyoga una virutubisho kama protini, wanga, sukari, fati, madini ya chuma, caicium pia uyoga una maji kwa kiasi kikubwa, pia uyoga una vitamini D
2.Uyoga hupunguza athari ya kupata saratani
3.Hushusha cholesterol
4.Huzuia kupata kisukari
5.Huimarisha afya ya mifupa
6.Husaidi katika ufyonzwaji wa madini ya calcium na chuma kutoka kwenye vyakula
7.Huimarisha mfumo wa kinga
8.Hushusha kiwango cha sukari kwenye damu


22.Faida za kiafya za kula bamia
1.Bamia lina virutubisho kama vitamini C, vitamini K, vitamini A na vitamini B. pia bamia lina protini, fati na madini ya magnesium.
2.Bamia lina antioxidant ambazo hulinda mwili dhidi ya maradhi
3.Hupunguza hatari ya kupata maradhi ya moyo
4.Hulinda mwili dhidi ya maradhi ya saratani
5.Hushusha kiwango cha sukari kwenye damu
6.Husaidia kwa wanawake wenye ujauzito na ukuaji wa mtoto


23.Faida za mbegu za papai
Mbegu za papai mara nyingi huliwa baada ya kukaushwa na kusagwa unga. Pia unaweza kuzikaanga kidogo ama kuzichemsha.
1.husaidia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kufanya kazi vyema
2.Husaidia kuzuia kupata saratani
3.Hulinda figo kufanya kazi vyema
4.Husaidia mwili katika kupambana na vijidudu vya maradhi
5.Husaidia kwa wenye kisukari
6.Husaidia katika kuondosha sumu za kemikali mwilini
7.Mbegu za papai zina virutubisho mbalimbali



24.Faida za kiafya za kula Ukwaju
1.ukwaju una virutubisho kama vitamini C, K, B6, B1, B2 na B3, madini ya chuma, potassium, magnesium na phosphorus.
2.Husaidia kuimarisha afya ya moyo
3.Husaidia kushusha presha ya damu
4.Husaidia mwili kupambana na mashambulizi ya bakteria, fangasi na virusi
5.Huzuia kuziba kwa choo na kuharisha
6.Husaidia katika kulinda afya ya ini
7.Husaidia wajawazito kuondoa kichefuchefu
8.Husaidia katika kuthibiti uzito
9.Hupunguza kasi ya kuzeheka haraka


25.faida za kiafya za kula karanga
1.karanga zina virutubisho kama protini, fati, vitamini B1, B2, B6, madini ya calcium, phosphorus, magnesium na sodium
2.Husaidia katika kudhibiti kisukari
3.Husaidia kuzuia saratani
4.Husaidia katika kutunza kumbukumbu na kuboresha afya ya ubongo
5.Huzuia unyonyokaji ama ukatikaji wa nywele
6.Husaidia katika kupunguza uzito
7.Husaidia katika ukuaji mzuri wa watoto
8.Huboresha afya ya ngozi
9.Ni nzuri kwa afya ya moyo


26.Faida z kiafya za pera
1.husaidia kushusha kiwango cha sukari kwenye damu
2.Husaidia kuimarisha afya ya moyo
3.Husaidia kupunguza maumivu ya tumbo la chango kwa wakinamama
4.Huboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
5.Husaidia katika kupunguza uzito
6.Husaidia kupunguza uwezekano wa kupata saratani
7.Husaidia kuboresha na kuimarisha mfumo wa kinga mwilini
8.Husaidia kuboresha na kuimarisha afya ya ngozi


27.Faida za kiafya za kula korosho
1.husaidia kuimarisha afya ya misuli na mishipa ya neva (mishipa ya fahamu)
2.Hupunguza hatari ya kupata kisukari
3.Husaidia matibabu ya saratani
4.Husaidia katika utengenezwaji wa seli hai nyekundu za damu
5.Huimarisha mfumo wa kinga
6.Husaidia katika kuimarisha afya ya kinywa (meno ) na mifupa
7.Hupunguza athari za maradhi ya anaemia yaani upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini
8.Hupunguza hatari ya kutengenezwa vijiwe kwenye kibofu


28.Faida za kiafya za kula fenesi
1.lina virutubisho vingi kama vitamini A, na C, pia kuna wanga
2.Huimarisha mfumo wa kinga
3.Ni chakula kinachotia nguvu
4.Huboresha afya ya moyo na mishipa ya damu na kuthibiti presha
5.Huzuai kukosa choo
6.Huzuia mwili dhidi ya kupata saratani
7.Huboresha afya ya macho
8.Husaidia kuimarish afya ya mifupa
9.Husaidia kuzuia pumu
10.Ni zuri kwa afya ya ngozi


29.Faida za kiafya za kula kabichi
1.kabichi lina virutubisho kama protini, vitamini K, A, B6 na C. pia lina madini ya chuma, calcium na magnesium.
2.Husaidia katika kupunguza mashambulizi ya mara kwa mara ya bakteria, virusi na fanasi
3.Husaidia katika kupona kwa haraka kwa majeraha
4.Husaidia kupunguza uharibifu wa seli dhidi ya kemikali mbaya
5.Huboresha afya ya mifupa, misuli na mishipa ya damu
6.Hupunguza uwezekano wa kupata saratani
7.Huboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kuzuia kukosa haja
8.Hufanya moyo wako uwe katika afya njema
9.Hushusha presha ya damu
10.Hushusha kiwango cha cholesterol



30.Faida za kiafya za kula kunde, maharage, njegere mbaazi na njugumawe
1.Tunapata virutubisho kama protini, vitamini B, A na K madini ya shaba, chuma, na manganese.
2.Husaidia kushusha sukari na kuboresha kiwango cha insulini
3.Hupunguza uwezekano wa kupata kisukari
4.Hupunguza cholesterol mbaya mwilini
5.Husaidia katika kupunguza uzito
6.Husaidia hatari ya kupata saratani
7.Hupunguza uwezekano wa kupata presha
8.Huboresha afya ya mifupa


31.Faida za kunywa maziwa
1.husaidia kuboresha afya ya ngozi
2.Huimarisha afya ya kinywa na meno
3.Huboresha afya ya mifupa
4.Husaidia katika ukiuari imara wa misuli
5.ni kinywaji kizuri kwa kupunguza uzito
6.Hupunguza stress na misongo ya mawazo
7.Hupunguza maumivu ya chango la wakinamama
8.Huondosha kiungulia
9.Huboresha mfumo wa kinga
10.Hupunguza mashambulizi ya mara kwa mara ya vijidudu vya maradhi



32. Faida za kiafya za kula Maini
1. husaidia katika kuipa miili yetu nguvu za kutosha
2.Huboresha afya ya ngozi
3.huimarisha afya ya mifupa
4.Maini ni chakula kizuri kwa afya ya moyo
5.Husaidia kuboresha afya ya ubongo
6.Ni chakula kizuri kwa ukuaji wa misuli
7.Huondosha sumu mwilini
8.Husaidia katika kulinda mwili dhidi ya saratani
9.Huupanguvu mfumo wa kinga



33.Faida za kiafya za kula mayai
1.Mayai yana virutubisho kama vitamini A, B5, B12, B2 B6, D, E na K. pia yai lina madini ya selenium, zinc na calcium
2.Husaidia katika kuongeza kiwango cha cholesterol zilizo nzuri
3.Husaidia katika ufanyaji kazi wa ubongo kuwa mzuri pia katika kutengeneza utando wa seli
4.Mayai huamini ka katika kupunguza hatari ya kupata maradhi ya moyo
5.Mayai ni chakula kizuri kwa afya ya macho
6.Mayai yana kiwango kikubwa cha protini iliyo bora kabisa
7.Pia mayai husaidia katika kupunguza hatari ya kupata kiharusi yaani kupalalaizi
8.Husaidia pia katika kupunguza uzito.


34.faida za kiafya za kula mahindi
1.mahindi yana virutubisho kama protini, wanga, madini ya chuma, vitamini B1, B5, B12, na vitamini C
2.Husaidia katika utengenezwaji wa seli hai nyekundu za damu
3.Husaidia katika kupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya anaemia
4.Ni chakula kinachoipa miili yetu nguvu
5.Husaidia katia kuongeza uzito
6.Husaidia katika kushusha kiwango cha sukari kwenye damu
7.Husaidia kwa afya ya mama mjamzito na mtoto aliyepo tumboni, pia husaidia katika kujifungua salama
8.Husaidia katika kuboresha afya ya ngozi


35.Faida za kiafya za kula samaki
1.samaki wana virutubisho kama protini, fati, vitamini kama vitamini D na madini mbalimbali kama iodine.
2.Hupunguza hatari ya kupata maradhi ya moyo kama shambulio la moyo na stroke
3.Ni chakula kizuri kwa ukuaji bora wa mtoto
4.Husaidia katika ukuaji wa ubongo na afya ya ubongo
5.Hupunguza stress na misongo ya mawazo
6.Ni chanzo kikubwa cha vitamini D
7.Hulinda mwili dhidi ya kupata kisukari
8.Huzuia pumu kwa watoto
9.Huboresha afya ya macho hasa kwa wazee
10.Husaidia kupata usingizi mwororo
11.Samaki ni chakula kitamu.


36.Faida za kiafya za kula tende
1.tende zina virutubisho kama protini, fati, wanga, sukari, vitamini k, B na A. pia tende zina madini ya chuma, calcium, phosphorus, sodium, magnesium, sulfur na zinc
2.Tende ni chakula kizuri kinachoweza kukupa nishati ya kutosha na kwa haraka sana
3.Tende husaidia katika kuborsha na kuimarisha afya ya ubongo, na kutunza kumbukumba
4.Tende husaidia katika kuondoa tatizo la kukosa choo
5.Huboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
6.Husaidia katika kupunguza tatizo la ugonjwa wa anaemia (upungufu wa oksijeni mwilini)
7.Hulinda moyo dhidi ya maradhi
8.Ni chakula kizuri kwa wasiopata hamu ya kushiriki tendo la ndoa
9.Husaidia kuboresha afya ya macho hasa katika kusaidia kuona wakati wa usiku
10.Husaidia katika kutibu tatizo la kuharisha
11.Huboresha afya ya mifupa
12.Hulinda mwili dhidi ya saratani
13.Huongeza uzito


37.Faida za kiafya za kula muwa (miwa)
1.husaidia katika kuupa mwili nguvu kwa haraka sana
2.Husaidia kwa wenye tatizo la kisukari hasa kwa wenye type-1 diabetes
3.Hulinda mwili dhidi ya saratani
4.Husaidia katika kulinda afya ya figo
5.Husaidia katika kuboresha mfumo wa kinga
6.Hulinda mfumo wa mmeng’enyo wa chakula uwe katika hali salama.
7.Huboresha afya ya meno na kuzuia kuoza ama kubenduka kwa meno
8.Huboresha afya ya kucha
9.Miwa husaidia kuboresha afya ya ngozi.


38.Faida za kiafya za kula kisamvu
1.kisamvu ni kizuri kwa wanawake wajawazito kwani kina vitamini C vingi
2.Husaidia kupambana na kwashoorkor (kwashiakoo) aina ya utapiamlo
3.Majani ya kisamvu yakipondwa husaidia kuondosha homa na maumivu ya kichwa
4.Hutibu kuhara unasanga majani
5.Hutibu tatizo la macho kutokuona vyema unachemsha majani ya kisamvu pamoja na tangawizi na chumvi
6.Huongeza hamu ya kual chemsha kisamvu, tangawizi na chumvi kisha kunywa
7.Hutibu minyoo
8.Husaidia kuchelewa kuzeheka
9.Hutibu stroke
10.Huongeza stamina
11.Husaidia katika kupona kwa vidonda na majeraha kwa haraka
12.Huboresha mfumo wa kinga


39.Faida za kiafya za kunywa chai
1.hupunguza hatari ya kupata shambulizi la moyo na strike
2.Husaidia katika kupunguza uzito
3.Huimarisha na kuboresha afya ya mifupa
4.Huboresha afya ya meno
5.Huimarisha mfumo wa kinga
6.Husaidia katika mapambano ya saratano
7.Huboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula


40.Faida za kiafya zakula Spinachi
1.mboga hii ina virutubisho kama vitamini A, C, na K, pia madini ya chuma sodium, calcium and mangenesium. Pia mboga hii ina fati na wanga.
2.Husaidia katika kupunguza uzito
3.Huboresha afya na macho
4.Huboresha afya ya mifupa
5.Hushusha presha ya damu (hypertension)
6.Husaidia mwili kurelas
7.Husaidia katika mapambano dhidi ya saratani
8.Ni nzuri kwa afya ya ngozi
9.Hulinda mwili dhidi ya anaemia
10.Huboresha mfumo wa kinga


41.Faida za kiafya za kula mihogo
1.mihogo ina virutubisho kama vitamini C, protini, wanga, sukari, vitamini B, madini ya calcium, magnesium, sodium na phosphorus.
2.Husaidia katika kupunguza uzito
3.Huboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
4.Husaidia kuboresha afya ya macho
5.Hutibu tatizo la kuharisha chemsha mizizi yake kisha kunywa
6.Husaidia katika kupenesha vidonda
7.Hutibu homa na maumivu ya kichwa
8.Hutibu minyoo
9.Huongeza hamu ya kula
10.Huianguvu miili yetu kwa haraka


42.Faida za kiafya za viazi mbatata
1.ni chakula kizuri kwa afya ya mifupa
2.Husaidia kushusha presha ya damu
3.Ni chakula kizuri kwa afya ya moyo
4.Husaidia katika afya ya ubongo kauka kutunza kumbukumbu, kujifunza, kurelax
5.Husaidia katika ukuaji wa mtoto
6.Uboreshaji wa mfumo wa fahamu na kuboresha seli
7.Husaidia katika mapambano dhidi ya saratani
8.Huzuia tatizo la kukosa choo
9.Husaidia kupunguza uzito
10.Ni chakula kizuri kwa afya ya ngozi
11.Husaidia katika kuboresha mfumo wa kinga
12.Viazi mbatata vina virutubisho kama vitamini C na vitamini B6. pia fati, wanga na protini. Pia kuna madini ya chuma, zinc, potassium, magnesium, phosphorus na mengineyo mengi


43.Faida za kiafya za kula viazi vitamu
1.vina virutubisho kama protini, fati, wanga, vitamini C, B5 pia madini ya potasium, shaba na magnesium.
2.Husaidia kuboresha ufanyaji kazi wa ubongo
3.Huboresha hedhi
4.Husaidia katika kupambana na saratani
5.Husaidia kushusha sukari kwenye damu
6.Huboresha mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
7.Husaidia mwili kupambana na maambukizi ya mara kwa mara
8.Husaidia katika kupunguza uzito


44.Faida za kiafya za kula komamanga
1.komamanga lina virutubisho kama A, C, K na E.
2.Hulinda mili dhidi ya kemikali
3.Huzuia damu kutokuganda kwenye mishipa ya damu na moyo
4.Huboresha afya ya moyo na mfumo wa mzunguruko wa damu
5.Komamanga husaidia kupunguza tatizo la nguvu za kiume
6.Husaidia katika harakati za kupambana na saratani
7.Husaidia katika afya ya ubongo hasa katika utunzaji wa kumbukumbu
8.Hushusha presha ya damu
9.Huimarisha mfumo wa kinga
10.Hupunguza stress na misongo ya mawazo


45.Faida za kiafya za kula Asali
1.Asali ina virutubisho kama sukari, vitamini na madini mbalimbali
2.Asali huweza kuupa mwili uwezo wa kujilinda dhidi ya shambulio la moyo, presha,na saratani
3.Pia asali huboresha afya ya macho
4.Huongeza kiwango cha sukari kwenye damu
5.Hushusha presha ya damu
6.Huborsha na kuimarisha afya ya moyo
7.Ni dawa kwa aliyeungua ama kwa mwenye kidonda ama jeraha
8.Ni dawa ya kikohozi kwa watoto


46.Faida za kiafya za mbegu za mronge (moringa)
1.mbegu za mronge zina virutubisho kama vitamini A, B na C. Pia zina madini kama madini ya calcium, chuma na pia kuna fata kama amino acid.
2.Husaidia katika kupata usingizi mwororo
3.Husaidia katika kuondoa tatizo la kukosa choo
4.Husaidia katika kuthibiti kiwango cha sukari kwenye damu
5.Ni chanzo kikubwa cha madini ya chuma
6.Husaidia katika kuondoa tatizo la kupata maradhi ya anaemia yanayopelekea upungufu wa hewa ya oksijeni mwilini
7.Hupunguza maumivu ya viungo
8.Husaidia katika kuuwa seli za saratani mwilini.
9.Husaidia kuboresha afya ya ngozi
10.husaidia kulinda afya ya moyo na mishipa ya damu.
11.Husaidia katika kulinda afya ya ini


47.Faida za kiafya za kula kunazi (lote tree)
Tumia matunda na majani yake, majani unaweza kuyakausha na kusaga unga wake ama kuyachemsha.


1.husaidia katika kupunguza maumivu
2.Husaidia katika kupunguza maumivu ya tumbo
3.Ni tunda zuri kwa afya ya mfumo wa upumuaji
4.Husaidia katika kuondosha sumu za vyakula na makemikali mwilini
5.Husaidia kurefresh mwili
6.Husaidia katika kutibu maradhi ya ngozi
7.Hupunguz maumivu ya chango kwa wakinamama
8.Husaidia katika afya ya hedhi
9.Husaidia katika ujauzito kwa mama na mtoto
10.Husaidia katika kushusha joto la mwili



48.Faida za kiafya za kula Zaituni
1.zaituni lina virutubisho kama protini, sukari, fati, pia lina vitamini E, madini ya chuma, shaba, calcium na sodium
2.Husaidia katika kulinda mwili dhidi ya saratani na mashambulizi ya vimelea vya maradhi
3.Huboresha afya ya moyo
4.Husaidia kuboresha afya ya mifupa
5.Husaidia katika kudhibiti fati kwenye damu
6.Hususha presha ya damu


49.faida za kiafya za ubuyu
1.ubuyu una virutubisho kama vitamini C na B, pia ubuyu una madini ya calcium, chuma, potassium na magnesium. Pia ubuyu una protini na fati
2. Husaidia katika kupunguza uzito
3.Husaidia kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu
4.Hupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya saratani na kisukari
5.Husaidia mwili kupambana na mashambulizi ya mara kwa mara
6.Huborsha mfumo wa mmeng’enyo wa chakual
7.Husaidia mwili kujilinda dhidi ya maradhi ya moyo
8.Hulinda utumbo na tumbo dhidi ya vidonda vya tumbo.


50.Faida za kiafya za peasi (pear)
1.peasi lina virutubisho kama vitamini C, B na K, pia madini ya chuma, magnesium na calcium. Pia peasi lina fati na protini
2.Husaidia kulinda mwili dhidi ya kisukari
3.Hulinda mwili dhidi ya maradhi ya moyo
4.Hulinda mfumo wa mmengenyo wa chakula dhidi ya uaribifu
5.Hulinda afya ya mishipa ya damu
6.Husadia katika kuondosha sumu mwilini
7.Huzuia athari za kemikali mwilini
8.Huboresha afya ya mfumo wa kinga


51.faida za kiafya za stafeli (soursop)
1.stafeli lina virutubisho





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Vyakula Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1260


Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Simulizi za Hadithi Audio     👉4 kitabu cha Simulizi     👉5 Kitau cha Fiqh     👉6 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-

Faida za kiafya za kunywa chai
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kunywa chai Soma Zaidi...

Fahamu Vitamini E na nz kazi zake, vyakula vya vitamini E na athari za upungufu wake
Katika makala hii nitakwenda kukupa somo linalohusu vitamini E, kazi zake, chanzo chake na madhara ya upungufu wake Soma Zaidi...

Vyakula murajabu kea mwenye presha ya kushuka
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula murajabu kea mwenye presha ya kushuka Soma Zaidi...

Faida za kula tikiti
Ukubwa wa tikiti unasadifu yaliyopo, kwani kuna fgaida akubwa sana za kiafya katika kula tikiti Soma Zaidi...

Faida za kitunguu thaumu
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kitunguu thaumu Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula papai
Soma Zaidi...

Vyakula vyenye maji mengi kwa wingi
Soma Zaidi...

Faida za kiafya za kula Fenesi
Soma Zaidi...

Faida za juice ya tende.
Posti hii inahusu zaidi faida ya juice ya tende,ni juice inayotumiwa na watu wengi sana na wengine wanajua kabisa faida zake na kuna wengine hawajui wanaitumia kama mazoea tu, ila kuna ambao hawajui kabisa basi zifuatazo ni faida za juice ya tende kwa wal Soma Zaidi...

Madhara ya mafuta mengi mwilimi
Post hii itakufundisha madhara ya kuwa na mafuta mengi mwilimi Soma Zaidi...

Faida za kula papai
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula papai Soma Zaidi...

NI ZIPI KAZI ZA PROTINI MWILINI?
Makala hii inakwenda kukuletea kazi kuu za protini na vyakula vya protini katika miili yetu. Mkala hii itakusaiidia kujuwa namna ya kupangilia lishe yako kiusalama zaidi baada ya kujuwa kazi za protini katika miili yetu. Soma Zaidi...