Dua Sehemu ya 02

Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa.

Dua Sehemu ya 02

NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA.
1.Theluthi ya mwisho ya usiku. Huu ni usiku wa manane usiku mkubwa. Muda huu mweye kuomba dua katu haiwezi kurudi kama anavyosimulia Abuuhurairah ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '" 'anashuka Mola wetu aliye tukuka kuja mbingu ya dunia kila usiku pindi inapobaki theluthi ya usiku ya mwisho kisha husema 'nani ataniomba nimjibu maombi yake, nani antaniomba nimpe na nani ataniomba msamaha nimsamehe'. (amepokea Bukahari, muslim na wengine).

2.Baada ya swala za faradhi. Anayetaka kuomba dua basi aombe baada ya kuswali swala ya faradhi, dua yake itajibiwa. ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '"' ' ' ' ' ' ' '"' Amesimulia Abuu Umama ' ' kuwa aliulizwa Mtume ' ' ' ' 'dua gani husikulizwa (zaidi na Allah? Akasema:) usiku mkubwa (theluthi ya mwisho ya usiku) na baada ya swala za faradhi'. (amepokea tirmith kwa isnad sahihi).

3.Kati ya adhana na iqama. Huu ni muda unaopatikana baada ya kuadhiniwa na mpaka kukimiwa kwa swala. Hapa mwenye kuomba dua itakuwa ni yenye kujibiwa. Amesimulia Anas ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema 'hairudishi (haiachi kujibiwa dua) kati ya adhana na iqama'. (amepokea Abuu Daud, Nisai na tirmith kwa isnad sahihi).

4.Wakati wa kusujudi. Hii ni dua inayoomwa wakati mtu akiwa amesujudi, dua hii pia ni yenye kujibiwa. Amesimulia Abuuhurairah ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema 'muda ambao mja anakuwa karibu zaidi na Mola wake ni pale akiwa amesujudi. Basi zidisheni dua (muda huu) na uweni na uhakika kuwa mtajibiwa. (amepokea Muslim na Daud).

5.Muda wa kukutana majeshi kwenye jihad, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na na muda wa kuiona alkaba. Amepokea Abuu Umamah ' ' kuwa Mtume ' ' ' ' amesema: 'hufunguliwa milango ya mbinguni na hujibiwa dua katika maeneo manne (nyakati): muda wa kukutana safu katika jihadi, muda wa kunyesha kwa mvua, muda wa kukimiwa kwa swala na muda wa kuiona alkaba'. (amepokea Tabrany).

6.Siku ya ijumaa. Siku ya ijumaa kuna muda ambao dua hujibiwa bila ya tatizo. Muda huu ni mchache sana na hakuna anaoujua. Zipo riwaya nyingi sana zinataja muda huu. Ila kuna riwaya zinaonesha muda huu ni baada ya swala ya al-'asr mpaka magharib. Ila ukweli ni kuwa muda huu ni mchache sana na haujulikani, jambo la msingi ni kujitahidi kumuomba Allah siku ya ijumaa yote huenda muda huo ungeupata.

HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA ITAJIBIWA.
1.Dua ya kumuombea aliye mbali. Chukulia mfano una ndugu yako yupo nchi nyingine ama mji mwingine kisha ukamkumbuka na ukataka kumuombea dua, basi dua hii itajibiwa tu. Mtume ' ' ' ' amesema 'hakika dua iliyo nyepesi (na haraka ) kujibiwa ni dua ya mtu kumuombea aliye mbali' (amepokea Abuu Daud na Tirmidh kwa isnad sahihi). Pia amesimulia Abuu Dardaa ' ' kuwa mtume ' ' ' ' amesema 'dua ya mtu muislamu ni yenye kujibiwa anapomuombea ndugu yake aliye mbali. Juu ya kichwa chake kuna Malaika anaitikia 'aamiin' na wewe upate mfano wa wake'. (amepokea Ahmd na Muslim).

2.Dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa. Hali za watu watatu hawa wakiomba dua Allah atajibu dua zao bila ya shaka. Mtume ' ' ' ' amesema ' "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '

3.'dua za watu watatu (hawa) ni zenye kujibiwa na hakuna shaka juu ya hili: dua ya mzazi, msafiri na mwenye kudhulumiwa'. (amepokea Abuu Daud, Ahmad na Tirmidh kwa sanad sahihi).

4.Dua ya mwenye swaum (funga), imamu muadilifu, na mwenye kudhulumiwa. Watu hawa dua zao zitajibiwa tu, kingozi muadilifu, mtu aliyekuwa kwenye funga na kabla hajafuturu na mtu aliyedhulumiwa. Amesema Mtume ' ' ' ' watu watatu dua zao hazirudi: mwenye funga mpaka afutauru, imamu muadilifu (kiongozi muadilifu), na mwenye kudhulumiwa.'.' (amepokea tirmidh kwa isnad sahihi).

SIFA ZA (MANENO NA MATAMSHI YA) DUA YENYE KUJIBIWA.
Hapa tutaona dua iliyo katika sura ambayo Allah ataijibu. Dua zenye kujibia wakati mwingine zina sura yake na sifa zake katika maneno na matamshi. Hebu tuone sifa hizo.

1.Dua ya nabii Yunusi. Mwenye kuomba dua na akatumia maneno aliyoyasema nabii Yunusi (amani ishuke juu yake) dua hii ni yenye kujibiwa. Amesema mtume ' ' ' ' 'dua ya nabii Yunus pindi alipokuwa kwenye tumbo la samaki (aliseme) 'LAA LILAAHA ILLAA ANTA, SUBHAANAKA INII KUNTU MINADHWALIMIINA' hakika hataomba mtu muislamu dua kwa kutumia maneno haya kitu chochote isipokuwa atajibiwa na Allah'. (amepokea tirmidh).

2.Kuomba dua kwa kutumia jina la Allah lililo kubwa. Allah ana majina mengi na mazuri. Lakini katika majina hayo lipo ambalo ni kubwa na ukiomba dua kwalo lakina utajibiwa. Kwa ufupi ni kuwa jina hili limefichwa na hakina yeyote anayelijuwa. Ila mtume ametowa ishara ya kuonesha wapi linapatikana na maneno gani mtu atumie kulipata jina hilo. Amesema mtume ' ' ' ' 'jina kubwa la Allah lipo kwenye aya sita za mwisho za surat hashri. (amepokea Dilamy kutoka kwa Ibn 'Abas). Pia katika mapokezi mengine ya Tabrany kutoka kwa Ibn 'Abas kuwa mtume amesema jina kubwa lipo kwenye aya ya 20 ya surat al-imran. Na pia zipo hadithi nyingi sana zinazoashiri wapi jina hilo lipo. Nitaleta chache tuu.

i) Aisha ' ' aliomba dua hii ' ALLAHUMMA INII AD'UKA LLAHA WA-AD'UKAR-RAHMANA, WA-AD'UKAL-BARRAR-RAHIIMA, WA-AD'UKA BIASMAAIKAL-HUSNAA KULLIHAA MAA 'ALIMTU WAMAA LAM A'ALAM AN TAGHFIRA LII WATARHAMNII' Mtume akacheka kisha akasema 'hakika jina kubwa lipo ndani ya dua hii. (amepokea Ibn Maajah kutoka kwa 'Aisha) hadithi hii ni ndefu nimeikatisha na kuchukua hiyo dyua tu.

ii)hadithi ya Anas' 'kuwa' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '.' ' ' ' ' ' ' ' "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '"amesimulia Anas ' ' kuwa alikuwa amekaa na mtume ' ' ' ' wamekaa msikitini na kulikuwa na mtu mmoja anaswali kisha akaomba dua kwa kusema ' ALLAHUMMA ANNII AS-ALUKA BIANNALAKAL-HAMDA, LAA ILAAHA ILLA ANTAL-MANNAANU BADI'US-SAMAAWATI WAL-ARDH YAA DHALJALALI WAL-IKRAM YAA HAYYU YAA QAYYUUM' akasema Mtume ' ' ' ' umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo anapoombwa kwalo atajibu'. (amepokea tirmidh kwa isnad gharib).

Iii)amesimulia Abdillah Ibn Buraydah ' ' kutoka kwa baba yake kuwa Mtume ' ' ' ' alimsikia mtu mmoja akisema 'ALLAHUMMA INNIASALUKA BIAN-ASHHADU ANNAKA ANTALLAHU LAA ILAAHA ILLA ANTA. AL-AHADUS-SWAMADUL-LADHII LAMYALID WALAM YUULAD, WALAM YAKUN LAHU KUFWAN AHAD' akasema Mtume ' ' ' ' hakika umemuomba Allah kwa jina lake kubwa ambalo akiombwa hutoa na akiombwa dua hujibu. (amesimulia Abuu Daud,tirmidh,Ibn Maajah na Ibn Hiban).

Iv). Mtume amesema ' ' ' ' ' ' '{' ' ' ' ' ' ' ' '}' ' ' ' ' '"'Jina kubwa la Allah linapatikana kwenye aya hizi' waillahukum ilahu wahidu laa ilaaha illa huwar-rahmanir-rahiim' na mwanzoni mwa surat al 'Imran

3.dua ya Mtume ' ' ' ' ni yenye kujibiwa. "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '"' Katika hadithisahihi mtume amesema Nabii yeyote ameomba dua yake na akajibiwa. Na nikaifanya dua yangu mimi ni shifaa kwa umati wangu sikku ya qiama. (amepokea Bukhari, Muslim na tirmidh kutoka kwa Anas).

4.Dua wakati wa raha hujibiwa wakati wa shida. Hii ni sifa ya dua yenye kujibiwa mbayo watu wengi hatujui. Nikuwa pindi unapopata neema na raha hapo ndipo pa kumuomba Allah na Allah atakujibu wakati unapopata matatizo kwa kukufariji na kukuondlea matatizo. Amesimulia Abuuhurairah ' ' kuwa mtume ' ' ' ' amesema "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '" ' 'mwenye kutaka kujibiwa dua yake wakati akiwa na shida basi azidishe kumuomba Allah wakati wa raha'. (amepokea Tirmidh kwa isnad gharib). Na katika mapokezi mengine amesema Mtume ' ' ' ' "' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' '" 'Mwenye kupenda kujibiwa dua zake wakati wa shida na taabu basi na azidishe dua wakati wa raha' (amepokea tirmidh)



         › WhatsApp ‹ Whatsapp



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 282


Download our Apps
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-