picha

MAZINGIRA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

MAZINGIRA

2.TAHADHARI KWENYE MAZINGIRA
Kama tulivyoona hapo juu, mazingira yetu ni sababu tosha ya kuathiri ubora wa afya zetu. Hivyo mtu ahakikishe sikuzote anaishi katika mazingira salama na safi. Wataalamu wa afya wanatueleza kusafisha mazingira yetu ya ilasiku ili tuweze kukabilia na na wadudu hatara.

Hakikisha hewa unayoipata ni safi na salama. Futa mavumbi ndani ya nyumba na nguo za kujifunika ziwe safi, kwa namna hii ni rahisi kukabilia na na mafua. Epuka moshi kutoka viwandani, pia usilale ukiwa na jiko la mkaa linalowaka na ikawa madirisha na milango umefunga. Unaweza kupata tatizo la kukosa oxkyjeni na kufariki dunia. Kaa mbali na wavuta sigara kwani hewa yao inaweza kukuathiri na wewe pia. Jambo la msingi hapa ni kuchukua tahadhari dhidi ya hewa ambayo tunaipata kwenye mazingira hetu.

Hakikisha unafyeka na kupunguza nyasi zilizo karibu na wewe. Fukia madimbwi na majimaji yoyote yalotuwama hata kama yapo kwenye kifuniko cha soda kwani hayo ni machache lakini mamia ya mbu yanaweza kuzaliana hapo. Mashimo ya kutupia taka yawe mbali kidogo na nyumba na kuwepo utaratibu wa kuchoma moto mashimo hayo bada ya muda. Usafi wa mazingira unaweza kuwa njia tosha ya kuanza harakati za kukabiliana na malaria na kipindupindu.

Watu wahakikishe wanakunywa maji safi na salama pamoja na kula vyakula ambavyo vimehifadhiwa kwa usalama. Usafi wa maji unaweza kuwa njia ya kupambana na typhod (taifodi) na maradhi mengine ya tumbo. Kuwepo na utaratibu wa kuyatibu maji kama yamepatikana sehemu ambazo sio salama na safi. Maji yanaweza kutibiwa kwa njia za kisasa kama kuweka madawa. Lakini pia unaweza kutumia njia ya kuyachemsha na kuyachuja na kuyatumia.

Sikuzote hakikisha unaishi katika mazingira rafiki na afya yako. Watu ambao tayari wanamaambukizi ya maradhi maalumu wanatakiwa waishi katika mazingira ambayo ni rafiki na hali zao.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu
Jiunge nasi WhatsApp
Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu image Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Views 811

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 web hosting     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Bongolite - Game zone - Play free game     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 ai web app    

Post zinazofanana:

CHUKUWA TAHADHARI KWENYE SHUGHULI ZAKO KULINDA AFYA YAKO

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
KITABU CHA MATUNDA

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
TAHADHARI KWENYE VYAKULA ILI KULINDA AFYA YAKO

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
AFYA NA MAGONJWA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Vipi kinyesi cha haja kubwa kinaelezea afya ya mtu

Katika somo hili tutajifunza ni Kwa namna gani afya Yako inaweza kuelezewa kupitia kinyesi

Soma Zaidi...
DONDOO 100 ZA AFYA

Pata dondoo 100 za Afya

Soma Zaidi...