KUKUSANYIKA KATIKA DUA.
Ni jambo la kupendeza kuomba dua mkiwa kwenye kundi. Zipo dua ambazo siku zote zinaombwa watu wakikusanyika kama dua ya kuomba mvua. Kukusanyika kwenye dua ni sunnah katika sunnah zingine. Ijulikane kuwa pindi mtu akiomba dua kisha wengine wakaitikia aamiin huenda katika waloitikia akawepo walii wa Allah ambae ikawa sababu ya dua kujibiwa. Pia watu waliokuwepo kwenye kundi aombe mmoja na wengine waitikie aamiin na wanyanyue mikono yao.

Maswahaba Allah awaridhie walikiwa wakiombeana dua na walikuwa pia wakikusanyika kayika kuomba dua. Mtume صلّي الله عليه وسلّم alikuwa pia akiwahimiza maswahaba wake kuwa katika kundi wanapoomba dua na wengine waitikie aamiin. Amesimulia Habiib Ibn Salamah رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “halikusanyiki kundi la watu na wakaomba dua wengine na wengine wakaitikia ‘aamiin’ isipokuwa Allah ataijibu dua hiyo”. (amepokea tbrany, Bayhaqy na Alhaakim).

NAMNA AMBAYO ALLAH HUJIBU DUA.
Itambulike kuwa dua ambayo imefata vigezo na masharti ya dua itajibiwa tu. Ila pia itambulike kuwa dua hujibiwa katika njia kuu tatu ambazo ni kupewa alichoomba, kufutiwa madhambi au kulipwa siku ya qiama kwa kuingizwa peponi. Hivyo itambuluke kuwa mtu anaweza kuomba dua kisha asijibiwe huenda Allah anataka kumpa kheri zaidi au huenda ameshamjibu kwa kumfutia madhambi yake. Allah ndiye anaejua lile ambalo ni bora kwa wajawake katika wakati wowote ule.

Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema مَا مِنْ أَحَدٍ يَدْعُو بِدُعَاءٍ إِلاَّ آتَاهُ اللَّهُ مَا سَأَلَ أَوْ كَفَّ عَنْهُ مِنَ السُّوءِ مِثْلَهُ مَا لَمْ يَدْعُ بِإِثْمٍ أَوْ قَطِيعَةِ رَحِمٍ ‏"‏ “ “mtu yeyote anaeomba dua ila atajibiwa ima awahishiwe kujibiwa haphapa duniani, au acheleweshewe (kujibiwa hapa duniani na badala yake ) ajibiwe akhera au asamehewe madhambi yake kwa kiasi kile alichoomba, maadam hajaomba (jambo la) madhambi au kukata udugu aua hajafanya haraka ya kutaka kujibiwa hata akawa anasema ‘nimemuomba Mola wangu na hakunijibu’”. (amepokea tirmidh).

DUA YA KAFIRI NA DUA YA MUUMINI.
Itambulike pia kuwa Allah huenda akacheewa kujibu dua ya mja wake si kwa sababu hataki ni kwa sababu anapenda kusikia sauti na maneno ya mja wake pindi anapoomba. Na hii ni kwa sababu Allah anapenda kuombwa. Pia wakati mwingine mtu anaweza kuomba dua na akajibiwa hapohapo au kwa haraka bila ya kujali awe muislamu ama sio muislamu. Hutokea kuwa Allah akawa hapendi sauti na maombi ya kafiri hivyo akaijibu dua ile ili amnyamazize mdomo wake. Jambo la msingi ni kuwa Allah anapompenda mja anapenda pia kumsikiliza anayoyasema na anachokiomba. Na anapomchukia mja huwa hapendi hata kumuona akiomba hivyo humjibu ili anyamaze.

Amesimulia Jabir رضىالله عنه kuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hakika (Malaika) Jibril ndiye aliyepewa kazi ya kutekeleza haja za wanaadamu, basi pindi mja kafiri anapoomba dua Allah husema kumwambia Jibril ‘ewe Jibril mpe haja yake kwani mimi sipendi kusikia dua yake. Na pindi anapoomba dua Mja muumini Allah humwambia Jibril ‘ewe Jibril izuie haja yake (usimjibu dua yake) kwani mimi napenda kusikia dua yake’”. )amepokea Ibn Najar).         › WhatsApp ‹ Whatsapp