Navigation Menu



Dua Sehemu ya 01

Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua?

Dua Sehemu ya 01

KITABU CHA DUA
Hiki ni kitabu cha dua na ni waqfu kwa ajili ya Allah. Hakiuzwi na na sio ruhusa kukiuza. Kwa anayetaka kukiprint ni bure awasiliane nasi pindi akitaka kufanya hivyo.

Tumeandika kitabu hiki kwa kutarajia radhi za Allah na kutoa mafundisho kwa waislamu na si vinginevyo.

DUA
Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani. Na dua ni ibada kama ibada nyingine.

Dua ni jambo lenye kupendeza kama walivyosema maulamaa na masalafi wema walotangulia. Umuhimu wa dua na msisitizo wake unapatikana katika quran na sunnah.

Dua zimesisitizwa sana katika quran na sunnah hata mtume akasema لِيَسْأَلْ أَحَدُكُمْ رَبَّهُ حَاجَتَهُ حَتَّى يَسْأَلَهُ الْمِلْحَ “na aombe mmoja wenu haya yake (dua) kwa Allah mpaka chumvi.…”. Hivyo si kuomba mambo kakubwa tu na matatizo tulonayo ila mpaka chumvi.

FADHILA ZA DUA

1.Dua ni ibada. Basi utambue ewe ndugu muislamu kuwa dua ni ibada. Imepokewa hadithi kutoka kwa Nuuman Ibn Bashir رضىالله عنه kuw Mtume wa Allah صليالله عليه وسلم amesema "‏ الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ“hakika dua ni ibada” (imepokewa na Tirmidh na ameisahihisha).

2.Dua ndio jambo tukufu zaidi kwa Allah kama Mtume صليالله عليه وسلم aliposema katika hadithi iliyosimuliwa na Abu Huraurah رضىالله عنه kuwa Mtume amesema “hakuna kitu kitukufu mbele ya Allah kuliko dua” (imapokewa na tirmidh, imam Ahmad na Alhaakim kwa isnad sahihi) لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اللَّهِ تَعَالَى مِنَ الدُّعَاءِ “

3.Allah anamchukia mtu ambaye hamuombi. Abuu Hurairah رضىالله عنه amesema kuwa Mtume صليالله عليه وسلم amesema "‏ مَنْ لَمْ يَسْأَلِ اللَّهَ يَغْضَبْ عَلَيْهِ ‏" “mtu yeyote ambaye hamuombi Allah, Allah humchukia mtu huyo” (amepokea hadithi tirmidh)

4.Allah anapenda kuombwa. Katika masimulizi ya Ibn Mas’ud رضىالله عنه Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “muombeni Allah katika fadhila zake, hakika Mwenyezimungu Mtukufu (غزّ وجلّ) anapenda kuombwa” (amepokea Tirmidh).

5.Dua ni malango wa rehema. Katika masimulizi ya ibn ‘Umar رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ مَنْ فُتِحَ لَهُ مِنْكُمْ بَابُ الدُّعَاءِ فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الرَّحْمَةِ وَمَا سُئِلَ اللَّهُ شَيْئًا يَعْنِي أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ أَنْ يُسْأَلَ الْعَافِيَةَ ‏"‏ “mwenye kufunguliwa mlango wa dua, hufunguliwa mlango wa rehema.…” (amepokea Tirmidh).

6.Dua huondosha mabalaa na majanga. Katika masimulizi ya Ibn ‘Umar, رضىالله عنه Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hakika dua hunufaisha kwa (hukinga) yale yanayoshuka (yanayotokea), na yale ambayo hayajashuaka ( hayajatokea). Basi jilazimisheni na (kuomba) dua enyi waja wa Allah.

ADABU ZA KUOMBA DUA.

1.kuelekea qibla. Amesimulia Abdallah Ibn Zayd رضىالله عنه kuwa “alitoka Mtume صلّي الله عليه وسلّم kwenda kuomba dua ya mvua akaelekea kibla”. (amepokea Bukhari).

2.Kunyanyua mikono miwili juu. Amesimulia Abuu Musa رضىالله عنه kuwa “aliomba Mtume صلّي الله عليه وسلّم dua akanyanyua mikono yake mpaka nikaona weupe wa kwapa lake” (amepokea Bukhari). Na amesimulia Ibn ‘Abas kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema ‏ "‏ إِذَا دَعَوْتَ اللَّهَ فَادْعُ بِبُطُونِ كَفَّيْكَ وَلاَ تَدْعُ بِظُهُورِهِمَا فَإِذَا فَرَغْتَ فَامْسَحْ بِهِمَا وَجْهَكَ “muombeni Allah kwa matumbo ya viganya vyenu, wala msimuombe kwa migongo ya viganja vyenu.…”. (amepokea Abuu Daud na Bayhaqiy).

3.Kuanza dua kwa kwa kumsifu Allah na kumshukuru (kama kusema alhamdu lillah ….) na kumswalia Mtume صلّي الله عليه وسلّم. Amesimulia ‘Abdullah Ibn Mas’ud رضىالله عنه kuwa nilikuwa nikiswali, wakati Mtume yupo na Abuubakar na ‘Umar, basi nilipokaa nikaanza kumshukuru Allah na kumsifu na nikamswalia Mtume صلّي الله عليه وسلّم kisha nikajiombea dua, akasema mtume صلّي الله عليه وسلّم ‘omba utapewa, omba utapewa’”. (amepokea tirmidh kwa isnad sahih). Na katika masimulizi ya Fudailah Ibn ‘Ubayd رضىالله عنه amesema “hakika amefundisha mtume صلّي الله عليه وسلّم uma wake jinsi ya kuomba dua akasema ‘pindi anapoomba dua mmoja wenu basi aanze na tahmid (kumshukuru Allah) na thanaai (kumsifu Allah) kisha amswalie Mtume صلّي الله عليه وسلّم kisha aombe chochote anachotaka’” ‏"‏ إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِتَحْمِيدِ اللَّهِ وَالثَّنَاءِ عَلَيْهِ ثُمَّ لِيُصَلِّ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ لِيَدْعُ بَعْدُ بِمَا شَاءَ ‏"‏ (amepokea Abuu Daud, tirmidh, Ibn Hiban na baihaqy).

4.Kuanza kuomba dua kwa kujiombea mwenyewe. Kwa anayetaka kumuombea mtu mwingine dua anatakiwa aanze na kujiombea mwenyewe. Amesimulia Ubaiya Ibn K’ab رضىالله عنه kuwa عَنْ أُبَىِّ بْنِ كَعْبٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا ذَكَرَ أَحَدًا فَدَعَا لَهُ بَدَأَ بِنَفْسِهِ “alikuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم anapomkumbuka mtu na akataka kumuombea dua huanza kwa kujiombea mwenyewe kwanza.” (amepokea tirmidh kwa isnad sahih).

5.Kurudia rudia katika kuomba na kusisitiza maombi yako. Ila usiharakishe majibu kutaka kujibiwa haraka hata ukawa unamlaumu Allah. Amesimulia Abdallah ibn Ms’ud رضىالله عنه kuwa alikuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم anapenda kuomba mara tatutatu na (akawa) anaomba istighfar (msamaha) mara tatutatu. (amepokea Abu Daud kwa isnad salih).

6.Kuwa na yaqini juu ya kujibiwa na kujiepusha na yaliyo haramu. Mtu anatakiwa asiwe na shaka juu ya kujibiwa dua yake. Amesimulia Abuu Hurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ ادْعُوا اللَّهَ وَأَنْتُمْ مُوقِنُونَ بِالإِجَابَةِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ لاَ يَسْتَجِيبُ دُعَاءً مِنْ قَلْبٍ غَافِلٍ لاَهٍ ‏"‏ “muombeni Allah mkiwa na yakini juu ya kujibiwa na jueni kuwa Allah hakubali dua ya mtu ambaye moyo wake umeghafilika naye. (amepokea Tirmidh na Alhaakim).

7.Usiharakishe kujibiwa. Isitokee mtu akawa na haraka ya kutaka maombi yake yajibiwe kama anavyotaka yeye kwa haraka hata akawa analaumu. Amesemulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema "‏ يُسْتَجَابُ لأَحَدِكُمْ مَا لَمْ يَعْجَلْ يَقُولُ دَعَوْتُ فَلَمْ يُسْتَجَبْ لِي ‏" “atajibiwa (dua yake ) mmoja wenu maadam hajaharakisha (kujibiwa) akawa anasema nimeomba na wala sijajibiwa”. (amepokea Bukhari na Muslim). Na katika masimulizi mengine ya Abuuhrairah kuwa mtume amesema “hataacha mja kujibiwa dua yake maadam hajaomba madhamdhi au kukata udugu”. (amepokea Muslim na Abuu Daud). Hii ina maana dua itajibiwa tu ila isiwe ya kuomba madhambi au kukata udugu.

8.Kuitikia “aamiin”. Mwenye kuomba dua basi aitikie “aamiin” eidha awe mwenyewe pekee au yupo na kundi la watu. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم “atakapoomba dua mmoja wenu basi na aitikie ‘aamiin’ mwenyewe’”. (amepokea Ibn ‘Adiy).

MASHART YA KUKUBALIWA KWA DUA.
1.kuchunga adabu za dua kama zilivyotajwa hapo juu.

2.Kuwa twahara nje na ndani. Yaani kujiepusha na mambo maovu na machafu ya siri na yasiyo ya siri. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم “hakika Allah ni mzuri na anapenda (vitu) vizuri.…”. (amepekea Bukhari na Muslim) Hivyo mtu anatakiwa ahakikishe ni mzuri ndani na nje.

3.kujiweka mbali na yaliyo haramu yote, na kujiepusha kula na kunywa bya haramu au kuvaa vilivyo haramu. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم “ukitaka dua maombi yako basi kifanye kizuri chakula chako (kisiwe cha haramu) “ (amepekea Bukhari na Muslim). Na pia katika hadithi ndefu iliyo sahihi katika kuwa mtume anashangaa mtu ambaye chakula chake haramu, kinywaji chake haramu, a mavazi yake haramu. Isitoshe mtu huyu amechafuka na manywele yapo timtim. Vipi atajibiwa dua yake mtu huyu. (amepekea Bukhari na Muslim).

4.Kuzingatia nyakati ambazo dua hujibiwa. Tutaziona hapo mbele.

5.Sifa ya dua yenyewe. Tutaona dua zenye sifa ya kujibiwa.

6.Hali inayozunguruka dua. Tutaona hali ambazo dua hujibiwa.


        

Download app yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download

Download Now Bongoclass

           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu image Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Views 784


Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

DUA 32 - 40
32. Soma Zaidi...

ADABU ZA KUOMBA DUA
ADABU ZA KUOMBA DUA. Soma Zaidi...

AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...

darasa la dua
Soma Zaidi...

Adabu ya kukaa na kula katika nyumba za watu
"Si vibaya kwa kipofu, wala si vibaya kwa kiguru, wala si vibaya kwa mgonjwa, wala kwenu, kama mkila katika nyumba zenu, au nyumba za baba zenu, au nyumba za mama zenu, au nyumba za ndugu zenu, au nyumba za dada zenu, au nyumba za ami zenu, au nyumba za s Soma Zaidi...

Dua sehemu ya 04
Soma dua mbalimbali za kila siku ambazo unatakiwa uzijuwe. Dua 120 ambazo muislamu anatakiwa kuzijua Soma Zaidi...

Dua za kuondoa wasiwasi, woga na kujikinga na uchawi, na mashetani
Post hii itakufundisha dua za kuomba wakati wa woga, wasiwasi na kujikinga na wachawi na mashetani Soma Zaidi...

UKITAKA KUOMBA BASI MUOMBE ALLAH, UKIMKUMBUKA WAKATI WA RAHA ATAKUKUMBUKA WAKATI WA DHIKI, SHIDA NA TAABU
عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا قَالَ: "كُنْت خَلْفَ رَسُولِ اللَّهِ صلى الله عليه و سلم يَوْمًا، فَقَالَ: ي... Soma Zaidi...

Faida za swala ya Mtume
Hapa utajifunza fadhila za kumswalia Mtume (s.a.w) Soma Zaidi...

Al-Arba-uwn An-Nawawiyyah hadithi ya 5: kujiepusha na uzushi katika dini
Hadithi hii inakataza kuzusha mambo ambayo hayapo katika dini Soma Zaidi...