Kitabu cha Afya 01

Soma kitabu hiki cha afya sehemu ya kwanza upate kuijua afya yako.

Kitabu cha Afya 01

KITABU CHA AFYA

SEHEMU YA KWANZA
-NADHARI NA MTAZAMO JUU YA AFYA

Afya ni hali ya kuwa mzima kimwili na kiakili. Kuna mahusiano makubwa kati ya kuwa mzima kimwili na akili. Mtu anaweza kuwa mwili upo mzima kabisa lakini akaambiwa hana afya salama kwa maana anaweza kuwa akili yake haipo vizuri. Kuathirika kiakili pia ni ugonjwa na ndio maana kuna wagonjwa wa sikolojia.

Hivyo mtu mwenye afyqa ni yule a,baye ni mzima wa mwili na akili. Na tunaposema akili haimaanishwi mgonjwa wa akili ni yule mkichaa hapa na bali hata ambaye saikolojia yake haipo vizuri nae ni mgonjwa.

Ndani ya mwili wa binadamu kuna mifumo ambayo hiyo kazi yake ni kuhakikisha kuwa mwili haudhuriki kimwili na kiakili. Mifumo hii ipo kazini muda wowotw kupambana na mamilioni ya wadudu hatari waliopo kwenye mazingira yetu. Kwa mfano kwenye hewa kuna mabilioni ya wadudu kama bakteria ambao huambukiza maradhi.

Mwili unaweza kuthibiti maradhi kupitia njia zake nyingi kwa mfano;- katika mfumo wa damu kuna seli hai nyeupe za damu hizi zinapambana na vijidudu vya maradhi. Halikadhalika mna katika damu antibodies hizi zinafanya kazi hii pia. Kwenye mfumo wa mmeng’enyo wa chakula kuna asidi ambazo zinakazi ya kuuwa bakteria na vijidudu vingine vya maradhi. Kwenye mfumo wa upumuaji kuna uttelezi na vijinywele ambavyo hukamata vijidudu pamoja na mavumbi na kutolewa nje.

Hivyo mwili una mfumo madhubuti kabisa wa kuweza kupambana na maradhi. Na ikitokea umepambana na kushindwa hapo hutokea mtu akaumwa. Pia ijulikane kuwa kinga za mwili zinaweza kutengenezwa na mwili wenyewe au kuzipata kwa kutumia chanjo. Mwili huanza kutengeneza kinga hizi hata kabla ya kuzaliwa kwa mtoto na hivyo hivyo mwili huendelea kuzitengeneza kinga hizi wakati wa kukua na kuendelea kwa maisha baada ya kuzaliwa.

Pia wakati mwingine mapambano yanapokuwa makali ndani ya mwili huweza kutokea maumivu katika sehemu za mwili. Kwamfano mfumo wa lymph unapopambana vikali huweza kusababisha maumivu ya mtoki.



        

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Jifunze Main: Afya File: Download PDF Views 459

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
πŸ‘‰1 Madrasa kiganjani    πŸ‘‰2 kitabu cha Simulizi    πŸ‘‰3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰4 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰5 Kitau cha Fiqh    πŸ‘‰6 Simulizi za Hadithi Audio   

Post zinazofanana:

DARASA LA AFYA, AFYA YA UZAZI, MARADHI NA LISHE BORA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
Kauli za wataalamu wa afya

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu kauli mbalimbali za wataalamu wa afya

Soma Zaidi...
TAHADHARI KWENYE VYAKULA

Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote

Soma Zaidi...
KITABU HA MATUNDA

Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho

Soma Zaidi...
Dua Sehemu ya 02

Zijuwe nyakati ambazo dua inakubaliwa kwa haraka zaidi. Zijuwe nyakati ambazo ukiomba dua hitakubaliwa.

Soma Zaidi...
Sheria za kutunza usafi wakati wa upasuaji.

Posti hii inahusu zaidi sheria za kutunza usafi wakati wa upasuaji, iwapo sheria mojawapo ikienda kinyume ijulikane kuwa usafi haujaenda sawa na pengine kwa kitaalamu huitwa contamination.

Soma Zaidi...
dondoo za afya

Basi tambua haya;- 1.

Soma Zaidi...