Posti hii inahusu zaidi namna ya kutunza chumba cha upasuaji, chumba cha upasuaji ni tofauti na vyumba vingine kwenye hospitali kwa hiyo vinahitaji uangalizi wa hali ya juu sana ili kuepuka aina yoyote ya uchafu kuwepo kwenye chumba hicho, zifuatazo ni na
Namna ya kutunza chumba cha upasuaji.
1.Chumba cha upasuaji kinapaswa kuwa na mjengo wa aina yake , kinapaswa kiwe na hewa maalum inayohitajika, madirisha hayapaswi kuwa wazi yanapaswa walau kubwa na wavu ili kuzuia wadudu au uchafu wowote kuingia hasa wakati wa upasuaji na wavu huo ufanyiwe usafi mara kwa mara, pia panakuwepo na sehemu mbalimbali kwenye chumba hicho ili kuweza kuwaruhusu wahudumu kufanya kila kitu kwenye sehemu yake.
2.Chumba cha upasuaji kinapaswa kuwa kwenye hali ya usafi kwa wakati wote.
Usafi kwenye chumba hiki unapaswa kufanyika kila siku walau mara mbili na zaidi kutegemeana na hali ya wagonjwa wanaohudumiwa kwenye sehemu hiyo na kila kitu kinapaswa kusafishwa iwe meza, sakafu na kufuta mavumbi kwenye sehemu mbalimbali na ikitokea labda kuna damu yoyote imetoka kwa mgonjwa inapaswa kutolewa mda huo huo na sehemu hiyo inapaswa kusafishwa na kemikali ambayo inaweza kuua wadudu wote kwa hiyo kemikali inapaswa iwe na nguvu sana.
3. Kutunza vizuri vifaa vilivyomo kwenye chumba cha upasuaji.
Tukumbuke kwamba vifaa vinavyotumika kwenye chumba hiki uweza kutumika mara nyingi kwa hiyo usafishwa kwa utaalamu wote mpaka wadudu wanaungua wote na kuweza kutumika tena kwa mgonjwa mwingine kwa hiyo vinapaswa kubaki kwenye hali ya usafi wa hali ya juu sana ili kuweza kuepuka Maambukizi. Kwa hiyo mtunza vifaa na msafishaji wa vifaa wanapaswa kuwa na elimu ya kutosha kwa kazi hiyo ili kuzuia kusambaa kwa maambukizi kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine.
4.Chumba cha upasuaji kinapaswa kwa na kila aina ya nguo zinazotumika wakati wa upasuaji.
Nguo zenyewe ni pamoja na kofia inayozuia nywele zisianguke kwenye mwili wa mgonjwa wakati wa upasuaji, maski inayozuia uchafu wowote kutoka puani wakati wa kupiga chafya na uchafu kutoka mdomoni, gauni linazuia uchafu wowote kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa wahudumu inawezekana kuwa ni damu au majimaji yoyote, gloves ambazo zinazuia kugusa damu au majimaji ya wagonjwa ambayo yanaweza kuwa na virusi vinavyoweza kutoka kwa mgonjwa kwenda kwa mhudumu au kwa mhudumu kwenda kwa mgonjwa.
5.Kwa hiyo tunapaswa kujua kuwa katika chumba cha upasuaji mgonjwa anayeingia pengine uweza kupasuliwa sehemu kubwa sana na ni rahisi wadudu wanaweza kuingia kwa namna moja au nyingine kwa hiyo wakiingia wanaweza kusababisha madhara makubwa zaidi kuliko ya kwanza kwa hiyo chumba hiki uwekwa kwenye hali ya juu kwa usafi na wahudumu wa hapo wanapaswa kuwa na maarifa makubwa kwa hiyo ni vizuri na haki kukiweka chumba hiki kwenye hali ya juu ya usafi.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiw ana App yetu. Bofya liln hapo chini kuweza ku download
Download NowJe! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Views 1426
Sponsored links
👉1
Simulizi za Hadithi Audio
👉2
Kitau cha Fiqh
👉3
Madrasa kiganjani
👉4
Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5
kitabu cha Simulizi
👉6
Kitabu cha Afya
Umuhimu wa kuvaa nguo za upasuaji.
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa nguo za upasuaji, tunajua wazi kuwa, wakati wa upasuaji tunapaswa kusafisha chumba na mazingira yake lengo ni kuhakikisha kuwa tunazuia wadudu wasisambae au kuingia kwenye mwili wa binadamu. Soma Zaidi...
MAGONJWA 7 YALETWAYO NA MBU: MALARIA, DENGUE, HOMA YA ZIKA, HOMA YA MANJANO
Soma Zaidi...
HUDUMA ZA KIAFYA KATIKA JAMII
Umuhimu wa huduma za kiafya katika jamii Soma Zaidi...
KAULI ZA WATU MASHUHURI KUHUSU AFYA
Soma Zaidi...
VIJUE VITAMINI, CHAZNO CHAKE, NA KAZI ZA VITAMINI MWILINI
Soma Zaidi...
Zijuwe faida za kiafya za kula Zabibu
Kula zabibubkina faida nyingi kwa afya yako. Soma Zaidi...
DONDOO 100 ZA AFYA
Pata dondoo 100 za Afya Soma Zaidi...
Nguo zinazovaliwa kwenye chumba cha upasuaji na kazi zake
Posti hii inahusu zaidi nguo za kuvaliwa kwenye chumba cha upasuaji na kazi zake, hizi ni nguo ambazo wahudumu wa afya wanapaswa kuzivaa wakati wa upasuaji kwa ajili ya kuwakinga na Maambukizi kati ya wahudumu wa afya na wagonjwa pia Soma Zaidi...
darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...