Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua?
KITABU CHA DUA
Hiki ni kitabu cha dua na ni waqfu kwa ajili ya Allah. Hakiuzwi na na sio ruhusa kukiuza. Kwa anayetaka kukiprint ni bure awasiliane nasi pindi akitaka kufanya hivyo.
Tumeandika kitabu hiki kwa kutarajia radhi za Allah na kutoa mafundisho kwa waislamu na si vinginevyo.
DUA
Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani. Na dua ni ibada kama ibada nyingine.
Dua ni jambo lenye kupendeza kama walivyosema maulamaa na masalafi wema walotangulia. Umuhimu wa dua na msisitizo wake unapatikana katika quran na sunnah.
Dua zimesisitizwa sana katika quran na sunnah hata mtume akasema لِيَسْأَلْ أَحَدُكُمْ رَبَّهُ حَاجَتَهُ حَتَّى يَسْأَلَهُ الْمِلْحَ “na aombe mmoja wenu haya yake (dua) kwa Allah mpaka chumvi.…”. Hivyo si kuomba mambo kakubwa tu na matatizo tulonayo ila mpaka chumvi.
FADHILA ZA DUA
1.Dua ni ibada. Basi utambue ewe ndugu muislamu kuwa dua ni ibada. Imepokewa hadithi kutoka kwa Nuuman Ibn Bashir رضىالله عنه kuw Mtume wa Allah صليالله عليه وسلم amesema " الدُّعَاءُ هُوَ الْعِبَادَةُ“hakika dua ni ibada” (imepokewa na Tirmidh na ameisahihisha).
2.Dua ndio jambo tukufu zaidi kwa Allah kama Mtume صليالله عليه وسلم aliposema katika hadithi iliyosimuliwa na Abu Huraurah رضىالله عنه kuwa Mtume amesema “hakuna kitu kitukufu mbele ya Allah kuliko dua” (imapokewa na tirmidh, imam Ahmad na Alhaakim kwa isnad sahihi)
لَيْسَ شَيْءٌ أَكْرَمَ عَلَى اللَّهِ تَعَالَى مِنَ الدُّعَاءِ “
3.Allah anamchukia mtu ambaye hamuombi. Abuu Hurairah رضىالله عنه amesema kuwa Mtume صليالله عليه وسلم amesema " مَنْ لَمْ يَسْأَلِ اللَّهَ يَغْضَبْ عَلَيْهِ "
“mtu yeyote ambaye hamuombi Allah, Allah humchukia mtu huyo” (amepokea hadithi tirmidh)
4.Allah anapenda kuombwa. Katika masimulizi ya Ibn Mas’ud رضىالله عنه Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “muombeni Allah katika fadhila zake, hakika Mwenyezimungu Mtukufu (غزّ وجلّ) anapenda kuombwa” (amepokea Tirmidh).
5.Dua ni malango wa rehema. Katika masimulizi ya ibn ‘Umar رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema " مَنْ فُتِحَ لَهُ مِنْكُمْ بَابُ الدُّعَاءِ فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ الرَّحْمَةِ وَمَا سُئِلَ اللَّهُ شَيْئًا يَعْنِي أَحَبَّ إِلَيْهِ مِنْ أَنْ يُسْأَلَ الْعَافِيَةَ " “mwenye kufunguliwa mlango wa dua, hufunguliwa mlango wa rehema.…” (amepokea Tirmidh).
6.Dua huondosha mabalaa na majanga. Katika masimulizi ya Ibn ‘Umar, رضىالله عنه Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema “hakika dua hunufaisha kwa (hukinga) yale yanayoshuka (yanayotokea), na yale ambayo hayajashuaka ( hayajatokea). Basi jilazimisheni na (kuomba) dua enyi waja wa Allah.
ADABU ZA KUOMBA DUA.
1.kuelekea qibla. Amesimulia Abdallah Ibn Zayd رضىالله عنه kuwa “alitoka Mtume صلّي الله عليه وسلّم kwenda kuomba dua ya mvua akaelekea kibla”. (amepokea Bukhari).
2.Kunyanyua mikono miwili juu. Amesimulia Abuu Musa رضىالله عنه kuwa “aliomba Mtume صلّي الله عليه وسلّم dua akanyanyua mikono yake mpaka nikaona weupe wa kwapa lake” (amepokea Bukhari). Na amesimulia Ibn ‘Abas kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema " إِذَا دَعَوْتَ اللَّهَ فَادْعُ بِبُطُونِ كَفَّيْكَ وَلاَ تَدْعُ بِظُهُورِهِمَا فَإِذَا فَرَغْتَ فَامْسَحْ بِهِمَا وَجْهَكَ “muombeni Allah kwa matumbo ya viganya vyenu, wala msimuombe kwa migongo ya viganja vyenu.…”. (amepokea Abuu Daud na Bayhaqiy).
3.Kuanza dua kwa kwa kumsifu Allah na kumshukuru (kama kusema alhamdu lillah ….) na kumswalia Mtume صلّي الله عليه وسلّم. Amesimulia ‘Abdullah Ibn Mas’ud رضىالله عنه kuwa nilikuwa nikiswali, wakati Mtume yupo na Abuubakar na ‘Umar, basi nilipokaa nikaanza kumshukuru Allah na kumsifu na nikamswalia Mtume صلّي الله عليه وسلّم kisha nikajiombea dua, akasema mtume صلّي الله عليه وسلّم ‘omba utapewa, omba utapewa’”. (amepokea tirmidh kwa isnad sahih). Na katika masimulizi ya Fudailah Ibn ‘Ubayd رضىالله عنه amesema “hakika amefundisha mtume صلّي الله عليه وسلّم uma wake jinsi ya kuomba dua akasema ‘pindi anapoomba dua mmoja wenu basi aanze na tahmid (kumshukuru Allah) na thanaai (kumsifu Allah) kisha amswalie Mtume صلّي الله عليه وسلّم kisha aombe chochote anachotaka’” " إِذَا صَلَّى أَحَدُكُمْ فَلْيَبْدَأْ بِتَحْمِيدِ اللَّهِ وَالثَّنَاءِ عَلَيْهِ ثُمَّ لِيُصَلِّ عَلَى النَّبِيِّ صلى الله عليه وسلم ثُمَّ لِيَدْعُ بَعْدُ بِمَا شَاءَ " (amepokea Abuu Daud, tirmidh, Ibn Hiban na baihaqy).
4.Kuanza kuomba dua kwa kujiombea mwenyewe. Kwa anayetaka kumuombea mtu mwingine dua anatakiwa aanze na kujiombea mwenyewe. Amesimulia Ubaiya Ibn K’ab رضىالله عنه kuwa عَنْ أُبَىِّ بْنِ كَعْبٍ، أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم كَانَ إِذَا ذَكَرَ أَحَدًا فَدَعَا لَهُ بَدَأَ بِنَفْسِهِ “alikuwa mtume صلّي الله عليه وسلّم anapomkumbuka mtu na akataka kumuombea dua huanza kwa kujiombea mwenyewe kwanza.” (amepokea tirmidh kwa isnad sahih).
5.Kurudia rudia katika kuomba na kusisitiza maombi yako. Ila usiharakishe majibu kutaka kujibiwa haraka hata ukawa unamlaumu Allah. Amesimulia Abdallah ibn Ms’ud رضىالله عنه kuwa alikuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم anapenda kuomba mara tatutatu na (akawa) anaomba istighfar (msamaha) mara tatutatu. (amepokea Abu Daud kwa isnad salih).
6.Kuwa na yaqini juu ya kujibiwa na kujiepusha na yaliyo haramu. Mtu anatakiwa asiwe na shaka juu ya kujibiwa dua yake. Amesimulia Abuu Hurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema " ادْعُوا اللَّهَ وَأَنْتُمْ مُوقِنُونَ بِالإِجَابَةِ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ لاَ يَسْتَجِيبُ دُعَاءً مِنْ قَلْبٍ غَافِلٍ لاَهٍ "
“muombeni Allah mkiwa na yakini juu ya kujibiwa na jueni kuwa Allah hakubali dua ya mtu ambaye moyo wake umeghafilika naye. (amepokea Tirmidh na Alhaakim).
7.Usiharakishe kujibiwa. Isitokee mtu akawa na haraka ya kutaka maombi yake yajibiwe kama anavyotaka yeye kwa haraka hata akawa analaumu. Amesemulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم amesema
" يُسْتَجَابُ لأَحَدِكُمْ مَا لَمْ يَعْجَلْ يَقُولُ دَعَوْتُ فَلَمْ يُسْتَجَبْ لِي " “atajibiwa (dua yake ) mmoja wenu maadam hajaharakisha (kujibiwa) akawa anasema nimeomba na wala sijajibiwa”. (amepokea Bukhari na Muslim). Na katika masimulizi mengine ya Abuuhrairah kuwa mtume amesema “hataacha mja kujibiwa dua yake maadam hajaomba madhamdhi au kukata udugu”. (amepokea Muslim na Abuu Daud). Hii ina maana dua itajibiwa tu ila isiwe ya kuomba madhambi au kukata udugu.
8.Kuitikia “aamiin”. Mwenye kuomba dua basi aitikie “aamiin” eidha awe mwenyewe pekee au yupo na kundi la watu. Amesimulia Abuuhurairah رضىالله عنه kuwa Mtume صلّي الله عليه وسلّم “atakapoomba dua mmoja wenu basi na aitikie ‘aamiin’ mwenyewe’”. (amepokea Ibn ‘Adiy).
MASHART YA KUKUBALIWA KWA DUA.
1.kuchunga adabu za dua kama zilivyotajwa hapo juu.
2.Kuwa twahara nje na ndani. Yaani kujiepusha na mambo maovu na machafu ya siri na yasiyo ya siri. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم “hakika Allah ni mzuri na anapenda (vitu) vizuri.…”. (amepekea Bukhari na Muslim)
Hivyo mtu anatakiwa ahakikishe ni mzuri ndani na nje.
3.kujiweka mbali na yaliyo haramu yote, na kujiepusha kula na kunywa bya haramu au kuvaa vilivyo haramu. Amesema Mtume صلّي الله عليه وسلّم “ukitaka dua maombi yako basi kifanye kizuri chakula chako (kisiwe cha haramu) “ (amepekea Bukhari na Muslim). Na pia katika hadithi ndefu iliyo sahihi katika kuwa mtume anashangaa mtu ambaye chakula chake haramu, kinywaji chake haramu, a mavazi yake haramu. Isitoshe mtu huyu amechafuka na manywele yapo timtim. Vipi atajibiwa dua yake mtu huyu. (amepekea Bukhari na Muslim).
4.Kuzingatia nyakati ambazo dua hujibiwa. Tutaziona hapo mbele.
5.Sifa ya dua yenyewe. Tutaona dua zenye sifa ya kujibiwa.
6.Hali inayozunguruka dua. Tutaona hali ambazo dua hujibiwa.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sunnah Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 647
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Madrasa kiganjani
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 kitabu cha Simulizi
NYAKATI AMBAZO DUA HUJIBIWA
NYAKATI AMBAZO DUA HUJUBIWA. Soma Zaidi...
Hadithi Ya 38: Anayeonyesha Uadui Kwa Rafiki Yangu Mtiifu Ninatangaza Vita Dhidi Yake
Soma Zaidi...
DUA ZA WAKATI WA SHIDA
DUA ZA WAKATI WA SHIDA 1. Soma Zaidi...
Dua za kuomba wakati unapokuwa na hasira ama ukiwa umekasirika
Post hii itakueleza ni dua gani unatakiwa uzisome wakati unapokiwa na hasira ama pale unapokasirika. Soma Zaidi...
Hadithi Ya 32: Kusiwe Na Kudhuriana Wala Kulipiza Dhara
الحديث الثاني والثلاثون "لا ضرر ولا ضرار" عَنْ أَبىِ سَعيدٍ سَعْدِ بْن مَالكِ بْن سِنَانٍ الْخُدريِّ رضي الله عنه أَنَّ رَسُولَ اللّ?... Soma Zaidi...
Mzazi na msafiri na mwenye kudhulumiwa dua zao hujibiwa kwa haraka
Wapo watu kadhaa ambao waliomba dua hazirudi. Hapa nitakueleza wawili ambao ni mzazi na msafiri. Soma Zaidi...
Hadithi Ya 22: Je, Nikiswali Swalah Za Fardhi, Nikafunga Ramadhaan
Soma Zaidi...
Mipaka katika kumtii mzazi, na mambo yasiyopasa kumtii mzazi
Soma Zaidi...
DUA ZA WAKATI WA HASIRA
DUA ZA WAKATI UNAPOKUWA NA HASIRA. Soma Zaidi...
MAANA NA FADHILA ZA KUOMBA DUA
DUA Kwa ufupi dua ni kumuomba Allah akuondoshee lililobaya, ama linalo kuudhi ama akupe jambo fulani. Soma Zaidi...
KAMA HUNA HAYA BASI FAJA UNACHOTAKA
عَنْ أَبِي مَسْعُودٍ عُقْبَةَ بْنِ عَمْرٍو الْأَنْصَارِيِّ الْبَدْرِيِّ رَضِيَ اللهُ عَنْهُ قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللَّهِ صلى الله عل?... Soma Zaidi...
ZIJUWE NAMNA ZA KUZUIA HASIRA, NA MADHARA YA HASIRA
28. Soma Zaidi...