image

KITABU CHA AFYA (kisukari, saratani, vidonda vya tumbo, HIV na UKIMWI) DALILI NA CHANZO

KITABU CHA AFYA (kisukari, saratani, vidonda vya tumbo, HIV na UKIMWI) DALILI NA CHANZO

Darasa la Lishe

By Rajabu Athuman

AFYA NA LISHE

AFYA NA LISHE.
Hapa tutaona zaidi mahusiano yaliyopo katika afya na vyakula ambavyo tunakula. Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa vyakula tunavyokula hujulisha namna tulivyo kimwili na kiakili. Ijapokuwa uwezo wa akili hueza kusababishwa na kurithi kutoka kwa wazazi lakini vyakula pia vina nafasi kubwa katika hili. Kwa mfano ulaji wa samaki husaidia katika maendeleo ya ubongo na ukuaji salama wa kiakili hasa kwa watoto. Hapa tutaangalia zaidi aina za vyakula na atharizake kama visipopatikana kwa kiwango kinachotakiwa mwilini.


1.AINA ZA VYAKULA
1.VYAKULA VYA PROTINI
Hivi ni vyakula ambavyo vinakazi ya kuujenga mwili pamoja na kuukarabati mwili. Kupona kwa vidonda na makovu vyote ni kazi ya protini. Uotaji wa nywele mpya pamoja na kukuwa kwa kucha baada ya kuzikata vyoye hivi hufanyika shukrani kwa vyakula vya protini.


Unaweza kuvipata vyakula vya protini kutokana na maziwa, nyama, mayai, na samaki. Katika mimea pia unaweza kupata protini kwa kula maharage, mchele na baadhi ya nafaka zingine. Pia ulaji wa mboga za majani unaweza kusaidia kupatikana kwa protini. .


2.VYAKULA VYA FATI NA MAFUTA
Vyakula vya fati husaidia katika kuupa mwili nguvu. Fat husaidia kulinda seli zilizomo mwilini zisizurike. Vyakula hivi huupa mwili joto hususan wakati wa baridi. Na inashauriwa wakati wa baridi kula vyakula vya fat kwa wingi ili kuupa mwili joto. Vyakula vya fat pia husaidia kuganda kwa damu pindi mtu anapopata jeraha.


Vyakula vya fati ni maziwa, mafuta ya wanyama, mayai na nyama. Pia katika matunda fat inapatikana kwa wingi pia kwa mfano katika avocardo, olive, karanga , alizeyi pamoja na mafuta ya mimea yaani vegetable oil. Samaki ni chanzo kizuri cha fat. . .


3.VYAKULA VYA WANGA
Vyakula vya wanga ndio vyanzo vikuu vya nguvu ndani ya mwili. Vyakula hivi hupatikana kwenye starch. Mwili unatumia vyakula vya wanga katika hali ya glucose. Ambayo huenda maeneo mengine ya mwili kwa ajili ya kuzalisha energy.


Unawza kupata wanga kwa kula nafaka kama maharage, matama, mihogo. Pia asali, miwa na viazi ni vyanzo vizuri vya wanga. inashauriwa kwa watu wanaofanya kazi ngumu zinazohitaji nguvu kubwa wale vyakula hivi.


4.VYAKULA VYA MADINI
Mwili unahitaji vyakula hivi ili uwezesj\he matumizi ya vyakula vingine yawe mazuri tunahitaji viyamini kwa kuulinda mwili dhidi ya magonkwa. Mwili unahitaji madini pia ili uweze kujikinga na hatari zingine. Madini ya chuma ni muhimu katika kujenga seli nyekundu za damu.madini ya calcium ni muhimu kwa afya ya mifupa na meno Madini na vitamin hpatikana zaidi kwenye mboga za majani, na matunda.


1.Madini ya sodium (table salt) Madini haya unaweza kuyapata kwenye spinach, maharage,punje za maboga n.k.


2.Madini ya chuma. Haya hupatikana kwenye maini, nyama, maharage, na mboga za majani. Madini haya ni muhimu kwa utengenezwaji wa hemoglobin yaani chembechembe nyekundu za damu.


3.Madini ya kashiam(calcium). Haya hupatikana kwenye maziwa,maini, mboga za majani na cheese. Madini haya husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno, misuli na utengenezwaji wa neva. Husaidia piaa kuwezesha kuganda kwa damu kwenye majeraha. Husaidia katika mfumo wa mmengοΏ½enyo wa chakula kwa kuzifanya enzymes kuwa active.


4.Madini ya phosphorus, haya hupatikana kwenye nyama, maziwa, samaki, na mayai. Husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno,misuli na shughuli za mfumo wa fahamu na utengenezwajiwa genetic materials.


6.Madini ya Potashiam (potassium) Hupatikana kwenye ndizi, machungwa,nyama na kaa. husaidia katika kurekebisha kiwango cha majimaji mwilini.


7.Madini yakopa ( copper) Haya hupatikana kwenye nyama, samaki, na maini.husaidia katika mifupa na utengenezwaji wa hemoglobin (chembechembe nyekundu za damu).


8.Madini yamanganese Madini haya hupatikana kwenye figo,maini, chai na kahawa. Husaidia katika utengenezwaji wa mifupa, na katika mmeng'enyo wa chakula kwa kufanya enzymes ziwe active.


9.Madini ya iodine Madini haya hupatikana kwenye chumvi na vyakula vya baharini kama samaki. Husaidia katika uzalishaji wa homoni ya thyroid.


5.VYAKULA VYA VITAMINI
Vitamin ni muhimu katika kuhakikisha kuwa mwili unatumia virutubisho vingine kufanya kazi zake. Kuna vitamin A,B,C,D,E na K. vitamin B vimegawanyika katika makundi kama vitamin B1,B2,B6, na B12. Ukosefu wa vitamin vyovyote kati ya hivi unaweza ukapelekea matatizo makubwa kwa afya ya mtu.


Vitamin A,D,E na K, vinaitwa fat soluble vitamin. Hivi nhuweza kuhifadhiwa ndani ya mwili. Hivyo hatuhitaji kula vyakula kuvipata kwa kila siku. Kwa upande mwengingine vitamin B na C huitwa water soluble vitamin, hivi havihifadhiwi ndani ya mwili, hivyo tunahitaji kula vyakula vyenye vitamin hivi kwa kila siku.


Vitamin A hupatikana kwenye maziwa, maini, karoti,machungwa, na mboga za rangi nya njano.. Vitamin B1 hivi hupatikana kwenye nyama, maini, mayai,hamira na mchele. Vitamin B2 hivi hupatikana kwenye nyama, maini, nafaka na hamira. Vitamin B3 hupatikana kwenye samaki, karanga,nyama, mchele usio kobolewa na hamira.. Vitamin B12 hivi hupatikana kwenye samaki,nyama, mayai,maziwa na maini.


Vitamin C hivi hupatikana kwenye matunda yenye uchachu kama limao na machungwa. Mboga za kijani,na nyanya. Vitamin D hupatikana kwenye mayai, maziwa, samaki na maini. Mitamini E hupatikana kwenye alizeti, butter, mchele na peanuts. Vitamin K hupatikana kwnye maini na mboga za majani.


Mtu atapata matatizo pia kama hata kunywa maji ya kutosha kwa siku. Maumivu ya kishwa huweza kusababishwa na kutokunywa maji ya kutosha. Choo kuwa kigumu huweza kusababishwa na uchache wa kunywa maji.


6.MAJI
Zaidi ya 70% ya mwili wa binadamu ni maji. Tunahiyaji maji ili tuweze kuishi. Mmaji ni muhimu kwa afya. Mtu anahitaji kunywa maji bilauri 8 mpaka 10 za maji. Mtu anaweza kuishi siku ziaizopungua 8bila kunya maji lakini anaweza siku nyingi zaidi bila ya kutokula chakula.


Maji husaidia kurekebisha mifumo mbalimbali ndani ya mwili kama vile mfumo wa utoaji takamwili, mfumo wa chakula na mfumo wa damu. Maji husaidia katika kutibu maumivu ya kichwa amabayo yamesababishwa na unywaji mchache wa maji.


7.ROGHAGE (vyakula vyenye asili ya kambakamba)
Hii si katika aina vya virutubisho. Hivi ni vyakula ambavyo husaidia katika msukumo wa chakula tumboni. Husaidia katika kufanya haja kubwa itoke kwa usalama. Matatizo ya kuziba kwa choo au kupata hajakubwa kwa kiasi kidogo husababishwa na kutokula vyakula vyenye hali hii kwa kiwango kinacho hitajika.


Tunaweza kupata roughage kwenye nafaka zote zisizo kobolewa, matunda, maharage, kabichi spinach, mihogo na nyanya zisizo menywa na jamii zingine za vyakula hivi.


2.UPUNGUFU WA VYAKULA HIVI NA MADHARA YAKE.
Kama tulivyosema huko awali kuwa upungufu wa chochote katika vyakula hivi unaweza kuleta madhara zaidi. Halikadhalika kuzidi kwa baadhi ya virutubisho mwilini kunaweza kusababisha madhara. Kwa mfano madini ya chumvi yakizidi zaidi mwilini yanaweza kusababisha presha ya kushuka. Halikadhalika madini ya chuma yakizidi pia ni hatari. Mwili unahitaji virutubisho hivi kwa kiwango maalumu. Na mwili wenyewe unafanya kazi hii ya kuchukua kiwango unachohitaji na kinachozidi kinatoka kwa njia ya haja kubwa au ndogo. Sasa hebu tuone kwa ufupi vyakula hivi vinaleta adhari gani pindi virutubisho vikipungua.


1.UPUNGUFU WA VYAKULA VYA MADINI
1.Madini ya sodium (table salt) Upungufu wa madini haya utapelekea udhaifu wa misuli na udhaifu wa mifupa. Pia mapigo ya moyo kutokuenda vizuri husababishwa na upungufu wa madini haya.


2.Madini ya chuma. Upungufu wa madini haya hupelekea matatizo katika mfumo wa damu. Ugonjwa wa anaemia unamahusiano ya moja kwa moja na upungufu wa madini ya chuma. Madini ya zink, hupatikana kwenye kamba, kaa, nyama na hamira. Husaidia pia katika afya njemaya mfumo wa kinga (immune system) na uponaji wa majeraha.


3.Madini ya kashiam(calcium). Madini haya yakipunguwa mwilini mifupa na meno huwa na udhaifu. Halikadhalika damu hutoka kwa muda mrefu baada ya jeraha kabla ya kuganda.


4.Madini ya phosphorus,Husaidia katika uimarishwaji wa mifupa, meno,misuli na shughuli za mfumo wa fahamu na utengenezwajiwa genetic materials.


5.Madini ya Potashiam (potassium) husaidia katika kurekebisha kiwango cha majimaji mwilini. Upungufu wa madini haya unaweza kupelekea matatizo katika misuli.


6.Madini yakopa ( copper) Upungufu wa madini haya unaweza ukapelekea urahisi katika kupasuka kwa mishipa ya damu, matatizo mkatika mifupa na viungio (joints).


7.Madini ya manganese Upungufu wa madini haya unaweza ukapelekea kupoteza kwa joto mwilini, mifupa kuwa nyepesi, kutokwa na damu za pua na kupata kizunguzungu.


8.Madini ya iodine Husaidia katika uzalishaji wa homoni ya thyroid. Ugonjwa wa goita (goiter) husababishwa na upungufu wa madini haya.


2.UPUNGUFU WA VITAMINI
1.Upungufu wa vitamini A hupelekea kukauka kwa ngozi, uoni hafifu na kuathirika kwa koo na ngozi


2.Upungufu wa vitamin B1 hupelekea kukosa hamu ya kula, udhaifu wa miguu, kupungua kwa hisia kwenye neva kudhoofu kwa misuli na kuathirika kwa akili.


3.Upungufu wa Vitamin B2 hupelekea kupata ugonjwa wa pellagra yaani vidonda vya mdomo na ulimi, ukuaji hafifu, kupasuka kwa nbgozi hasa sehemu za sikio na pua.


4.Upungufu wa Vitamin B12 husababisha matatizo katika uzalishaji wa seli hai nyekundu za damu. Na kusababisha aina ya ugonjwa wa anaemia


5.Upungufu wa vitamini C husababisha kutoka damu kwenye mafinzi, kuchelewa kupona kwa majeraha, maumivu ya viungo na kudhoofu kwa mishipa ya damu hasa kwenye ngozi.


6.Upungufu wa vitamin D husababisha kuleta matege.
7.Upungufu wa vitamin k husababisha kuchelewa kuganda kwa damu kwenye jeraha


UPUNGUFU WA MAJI
Maji yakipungua mwilini yanaweza kuleta madhara makubwa hata kifo. Hali hii ikitokea kuwa maji yamepunguwa kwa kiasi kikubwa sana kwa haraka mgonjwa ataongezewa maji. Hili linajulukana sana. Ila nataka kuongezea maarifa hapa kuhusu kupunguwa kwa kawaida nini adhari zake kwenye mwili. Endapo maji yakipungua kwa hali hya kawaida mtua ataanza kuhisi kiu.


Pia maji yanaweza kusababisha maumivu ya kichwa. Choo kuwa kigumu na hatimaye kutoka na damu kwa sababu ya kuchubua kuta za haja kubwa. Mkojo kuwa mchache na kutokwa na jasho kwa kiasi kidogo sana. Mtu anaweza kuhisi kuchanganyikiwa na kuhisi kama kichwa chaje ni chepesi sana. Pia athari nyingine unaweza kuziona kwenye ngozi pale ngozi inapopoteza uhalisia wake wa kujikunja na kusinyaa. Ngozi inakuwa ngumu na imekauka.


UPUNGUFU WA PROTIN
Ugonjwa wa kwashiakoo ni katika yanayoletwa na upungufu wa protini. Pia ukuaji hafifu wa mtoto na kupelekea kudumaa ni katika upungufu wa vyakula hivi. Kiriba tumbo hasa kinachotokea kwa sbabu ya kuvimba kwa ini. Hii huweza kupelekea ini kushindwa kufanya kazi. Misuli na nyama za mwili kushindwa kujaa kwa ufasaha. Wataalamu wanahusisha uimarikaji wa mifupa kuwa unategemea pia vyakula hivi. Hivyo upungufu wa protini huweza kusababisha udhaifu wa mifupa.


UPUNGUFU WA FATI
Kama hautapata fat ya kutosha kuweza kutengeneza omega-3 fat acid unaweza kupata upungufu wa vitamin A, D, E na K hivyo magonjwa yanayohusiana na upungufu wa madini haya hayatakuwa mbali nawe. Vyakula vya fati vina saidia katika kuiweka ngozi kuwa katika afya njema. Kama utakosa fati ya kutosha ngozi yako itashindwa kupata majimaji ya kutosha na hivyo kupelekea afya dhaifu ya ngozi.


Omega-3 fat acid ipo katik aina kuu mbili ambazo ni eicosapentaenoic acid na docosahexaenoic acid hizi husaidia katika ukuaji na maendeleo mazuri ya ubongo. Pindi ukikosa aina hizi za fat acid unaweza kupata matatizo ya kusahau na ukuaji hafifu wa ubongo. Omega-3 fat acid inaweza kupatikana kwenye samaki, nyama na vyakula vingine lakini si kwenye matunda wala mboga a majani. Fat acidi inasaidia katika kutengebezwa kwa pigment rhodopsin hizi husaidia katika kuboresha afya ya macho. Husaidia katika kuufanya ubongo uweze kutafasiri mwanga kuwa kitu unachokiona. Husaidia sana kwa wazee dhidi ya matatizo ya kutokuona.


MAGOJWA YANAYOHUSIANA NA VYAKULA
1.UGONJWA WA KISUKARI
kisukari ni ugonjwa unaotokea pale ambapo mwili unashindwa kuzalisha kabisha homon ya insulin au kushindwa kuzalisha homon hii kwa kiwango kinazotosha. Wakati mwingine kisukari kinatokea pale mwili unaposhindwa kutumia insulin inayozalishwa mwilini. Hii ni homon ambayo inakazi ya kuthibiti kiwango cha sukari ndani ya mwili kisiwe kikubwa au kuwa kidogo. Homoni hii huzalishwa na kongosho (pancreas. Homoni ya insulin huakikisha kuwa kiwango cha sukari ndani ya mwili kikiwa kikubwa hubadilishwa kuwa glucagon na huhifadhiwa kwenye ini. Na kiwango cha sukari kikiwa kidogo glucagon hubadilishwa na homon hii kuwa glucose (sukari) ambayo husambazwa sehemu zinazohotaji kuzalisha energy. .


2.UGONJWA WA SARATANI
Ugonjwa wa saratani hutokea pale seli za mwili zinapokuwa bila ya mpangilio maalumu na kusababisha uvimbe. Uvimbe huu huenda ukawa mkubwa zaidi na kusababisha uharibifu wa viungo vya mwili kama maini ubongo na mishfupa. Uvimbe huu pia hueza kusambaa mwilini na kusababisha vimbe mbalimbali ndani ya mwili.


Kikawaida seli ndani ya mwili huzaliwa na baadaye huweza kufa baada ya kipindi maalumu. Kwa mtu mwenye saratani seli hizi hazifi hivyo huendelea kukuwa bila ya mpangilio. Seli hizi huweza kuingia kwenye mfumo wa damu na kusambazwa kuelekea sehemu zingine za mwili na hatimaye kusambaa kwa saratani viungo vingine vya mwili .


3. UGOJWA WA MACHO
Ugonjwa wa macho ni katika magonjwa leo yanayosumbuwa sana. Yanasumbuwa watoto wazee na vijana. Tatizo hili limekuwa likisumbuwa pia wanafunzi. Watu wengi leo wamekuwa wakitumia miwani kwa ajili ya kuwawezesha kuona. Kuna wenye matatizo ya kutokuona ,bali na wapo wenye matatizo ya kutokuona karibu. Wengine macho yanatowa machozi na kuwasha sana. Macho kuwa mekundu na maumivu makali ni katika baadhi tu ya matatizo ya macho.


Wataalamu wa afya ya macho bado wanajitahidi kutafuta vyanzo halisi vya matatizo haya. Kwa kiasi wamefanikiwa na tiba zinatolewa kwa wenye matatizo haya. Japo kuna magojwa mengine ya macho bado haijatambulika ninini chanzo halisi lakini bado tiba zinatolewa. Wapo wanaopata matibabu kwa wajuzi wa dawa za mitishamba na wapo wanaopata matibabu kutoka hospitali. .


4. PRESHA NA SHAMBUKUO LA MOYO
Ugonjwa wa presha umekuwa ukisumbuwa watu wengi leomduniani. Watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha kwa sababu ya presha. Presha hutokea pale moyo unaposukuma damu kwa nguvu sana yaani presha ya kupanda. Pia hutokea pale moyo unapoksukuma damu kidogokidogo yaani presha ya kushuka. Presha ikipanda huweza kupasua mishipa na kusababisha mtu kutokwa na damu au kupata stroke (kiharusi).


Miongoni mwa sababu za ugojwa huu ni pamoja na kuzidi kwa uzito mwilini na vyakula tunavyokula. Kikawaida kuzidi kwa uzito pia ni matokeo ya vyakula ambavyo tunavila. Hivyo kwa ajili ya kupambana na tatizo hili ni lazima kuanza kubadilisha mfumo mzima wa vyakula. Kama ville vyakula ambavyo vina mafuta mengi. soma zaid


5. VIDONDA VYA TUMBO
Vidonda hivi hutokea ndani ya mfumo wa mmeng'enyo wa chakula. Huweza vikatokea kwenye tumbo la chakula, kwenye utumbo mdogo au kwenye utumbo mkubwa. Vidonda hivi hutambulika kwa dalili nyingi na maumivu makalisana. Maumivu haya hutokea kwa muda kasha hupowa. Wakati mwingine yanakuwa ni makali sana kiasi mtu atafikiri anakaribia kufa.


Miongoni mwa dalili za vidonda vya tumbo ni kupata maumivu ya tumbo mara kwa mara. Tumbo hili huuma kati ya kifua na tumbo. Kukosa hamu ya kula, vidonda hiviu vikizidi mtu anakonda sana na kukosa nguvu. Tumbo kujaa gesi, kutapika ,maumivu ya moyo na kupoteza uzito. Zipo dalili nyingi ila dalili hizi zinatofautiana na aina ya vidonda na sehemu vilipo .


6.MAGONJWA YANAYOHUSIANA NA UPUNGUFU WA VITAMINI NA MADINI
Kama tulivyoona hapo juu kuhusu upungufu wa vitamini na madini. Yapo maradhi mengi sana ambayo yanasababishwa na upungufu wa vitamini na madini. Pia tambuwa kuwa wakati mwingine kuzidi kwa madini na vitamini flani mwilini kunaweza kusababisha maradhi. Kupata orodha ya magonjwa haya usiache kusoma kitabu chetu cha Afya.



Pata kitabu Chetu Bofya hapa





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 796


Sponsored links
πŸ‘‰1 Kitau cha Fiqh     πŸ‘‰2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰3 Madrasa kiganjani     πŸ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio     πŸ‘‰5 Kitabu cha Afya     πŸ‘‰6 kitabu cha Simulizi    

Post zifazofanana:-

Umoja wa mataifa unazungumziaje afya
Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu Mambo ya kiafya yanayozungumzwa na umoja wa mataifa Soma Zaidi...

UGONJWA WA MALARIA NA TAKWIMU ZA ATHARI YAKE KIDUNIA
Malaria ni katika maradhi ambayo husambazwa na na mbu jike aina ya anopheles. Soma Zaidi...

kitabu cha afya
Jifunze sifa na aina za matunda, vijuwe viruturubisho Soma Zaidi...

dondoo 100 za afya
Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

MAWAKALA WA KUSABABISHA NA KUSAMBAZA MARADHI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Dondoo za afya 1-20
Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya Soma Zaidi...

YANAYOATHIRI AFYA KATIKA VYAKULA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

Umuhimu wa kupiga push up kiafya
Posti hii inahusu zaidi umuhimu wa kupiga push up kiafya, ni mambo au faida zipatikanazo ki afya kwa wapigaji wa push up kama ifuatavyo. Soma Zaidi...

kitabu cha afya
Soma Zaidi...

Madhara kwa wasiofanya mazoezi
Posti hii inahusu zaidi madhara mbalimbali ambayo yanaweza kutokea kwa watu wasiofanya mazoezi, mazoezi ni kama tiba kwa namna Moja au nyingine ila Kuna madhara ambayo yanaweza kutokea kwa wale ambao hawafanyi mazoezi. Soma Zaidi...

MAWAKALA WA MARADHI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...