Posti hii inahusu zaidi utumiaji wa pombe na sigara pamoja na madawa katika jamii.
Kutokana na nilivyoeleza hapo awali tutaona madhara na hathari zitokanazo pombe,sigara na matumizi ya madawa.ambayo yamekuwa hatari katika jamii zetu.pia jamii yetu inakabiliwa na kasi ya kuongezeka kwa vitendo vya ulevi,uvutaji wa sigara na utumiaji wa madawa ya kulevya .vitendo hivi huathiri kwa kiasi kikubwa afya na uwezo wa kufanya kazi wa watumiaji Aidha,vitendo hivi vinahusika na mmomonyoko wa maadili ya jamii zetu.pia matatizo haya yakiwa mengi uweza kupelekea kuathiri jamii nzima pamoja na kuwaambukiza watu wengine.
1.POMBE .hiki ni mojawapo ya kilevi kinachosababisha jamii kubwa kuathirika kutokana na unywaji wa kilevi hiki.pia pombe inapelekea kuharibu maadili ya watu endapo mtu atatumia kilevi hiki.kutokana na unywaji wa pombe asilimia kubwa ya watu wanaotumia kilevi hiki ni vijana walioko umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea.vipo viburudisho vya aina nyingi.baadhi ya viburudisho hivyo ni vizuri lakini vingine vinakuwa na madhara kwenye miili ya binadamu . kati ya viburudisho vyenye madhara ni pombe kama itanywewa kwa wingi (ulevi).kwa bahati mbaya pombe inapendwa na watu wengi .mambo mawili yanayoathiri wanywaji wa pombe ni aina ya kasi ya pombe wanachokunywa kulingana na uwezo wa miili yao kustahimili.pombe haina madhara kwenye mwili ikitumiwa kwa kiasi .kuna bahadhi ya pombe ambazo ni hatari kwa afya ya mwanadamu pombe ya kienyeji inayopikwa aina ya gongo.pombe hii ina madhara makubwa sana kwa sababu ni pombe ambayo haijapimwa kwa kiwango mahalumu na vyombo husika. Pombe hii haina ya gongo ni pombe kali muno haipaswi kutumika kwa watu sababu madhara yake ni makubwa alafu inapelekea watu kuhumwa pia kupoteza maisha yao.pombe ikishanywea ,huingia tumboni na hatimaye kwenye damu.kadri pombe inavyoingia kwenye damu tumboni.ndivyo inavyozidi kuingia kwenye damu.Damu inapokuwa na pombe nyingi hudhoofisha sehemu za ubongo.mtu aliyelewa hawezi kutawala matendo yake vizuri kwa mfano, anaweza kugombana,kubaka,kutoa matusi mabaya na kupigana.kitendo cha ulevi kinaweza kumletea binadamu madhara ya kiafya,kijamii na kiuchumi.
. Zifuatazo madhara ya unywaji wa pombe katika jamii.
njia za kujikinga na kuzuia utumiaji wa pombe katika jamii.
1.uaitumie pombe kwa sababu italeta madhara makubwa kama tulivyoelezwa apo awali.poa kama ni mtumiaji wa pombe.ni marukufu kutumia au kunywa pombe kiasi kikubwa,hili uweza kukuletea madhara pamoja na magonjwa tulivyoona hapo mwanzo yakiwemo.kisukari,ini,na ugonjwa wa moyo.
2.pombe ukitumia itaweza kuathiri wewe na maendeleo yako .pamoja na familia hili kuepukana na hili tatizo inabidi kuacha kutumia kilevi hiki sababu hakina faida yoyote ile baadhi ya kutupatia hasara kwenye jamii zetu .
3.tumia kinywaji kingine tofauti na kilevi.mfano juice ya matunda ambayo itaweza kukuletea afya mwilini mwako na kukujenga vizuri mwili wako.hii hazitapelekwa watu kugombana na kupigana bali italeta furaha kwenu.
4.kama unatumia pombe usiendeshe chombo cha moto.ukifanya hivyo hautaweza kuleta hajali katika jamii..
5.hepuka kukaa na watu wanaotumia kilevi hiki kwa sababu wanaweza wakakupa vishawishi vya ulevi endapo kama hautumii bali wape ushahuri waweze kuacha kutumia pombe.
6.usipokunywa pombe utapendwa na jamii pamoja na watu wote.pia utakuwa mwaminifu katika jamii nzima .pia itakuwa nafasi nzuri ya kuweka familia yako na jamii kwa ujumla hii itakuwa vizuri.
2.UVUTAJI WA SIGARA.
Sigara ina sumu kali iitwayo nikotini.kwenye moshi wa sigara ipo gesi iitwayo kabonimonoksaidi.Gesi hii ni sumu kali na ina uwezo wa kuharibu mishipa ya fahamu .lami ambayo ni mchanganyiko wa vitu mbalimbali ,vikiwepo vile vinavyosababisha saratani ,hutokana na kile kinachofanya moshi wa sigara kunatanata.ukiangalia kwenye jamii nyingi vitendo hivi vya uvutaji wa sigara vinatumiwa sana na vijana .wa kuanzia umri ule ule wa miaka 18.pia sigara ina madhara kwenye mwili wa binadamu:
yafuatayo ni baadhi ya madhara ya sigara kwenye mwili wa binadamu.
1.sigara zinauchakaza mwili wa binadamu.hii ni kweli kutoka uvutaji wa sigara .mwili wa binadamu unakuwa umechoka pia na kuchakaa tunaona pia sigara ni hatari kwa afya ya mwanadamu.hivyo sigara inaleta ugonjwa wa mapafu kusinyaa.
2.sigara zinafupisha maisha;kutoka na hili madhara sigara inafupisha maisha ya mwanadamu endapo atakuwa anavuta sigara .tunaona katika jamii yetu wanaovuta sigara maisha yao huaga ni mafupi sana.kwahiyo ni marufuku kutumia hiki kilevi cha uvutaji wa sigara.
3
.sigara zinaleta magonjwa ya saratani ya mapafu,moyo na kifua. Tunaona watu wengi wanaathirika mapafu kutokana na uvutaji huu wa sigara.hivo hivo watu wanauwezo wa kuhathirika sana endapo wataendelea kuvuta sigara katika jamii .
4.sigara zinaleta matatizo katika uzazi na kusababisha mtoto kuzaliwa kabla ya siku zake,kuzaliwa akiwa amekufa au kufa mara tu baada ya kuzaliwa.wakati mwingine mtoto huzaliwa na uzito pungufu .kwahiyo inatubidi kuacha kuvuta sigara kwa mama mjamzito katika jamii zao .hivo hivo inabidi watu kupewa elimu kuhusu kuvuta sigara .
UVUTAJI WA SIGARA:
Bangi ni mmea ambayo haina utofauti na sigara. lakini bangi ni mmea ambayo huota sehemu nyingi duniani .bangi inalevya zaidi kuliko sigara.Ulevi wa bangi huathiri fahamu na uwezo wa mtu kukanlbili mambo yake.muhimu katika maisha .Aidha ,mvutaji wa bangi hujisikia kuwa hali yake haina dosari.Akili ya mvutaji bangi inashindwa kuzingatia mambo kwa wepesi wake wa kawaida wakati muhusika hajitambui.Badala yake mhusika hujihisi kuwa katika hali ya raha na kujiona kuwa uwezo wa fahamu yake kutenda mambo mbalimbali ni mkubwa kuliko kawaida yake.
Baada ya kuvuta bangi ,mvutaji hujisikia kuwa na kichwa chepesi ,kizunguzungu,kuvuma masikio na pengine hujisikia anaelea angani .macho yake huwa mekundu na wakati mwingine hutoa machozi. Na hukwepa mwanga mkali.Mapigo ya moyo huwa ya haraka na shinikizo la damu huongezeka.
Madhara yatokanayo na uvutaji wa bangi.
1. Huathiri ufanisi wa kazi za mikono na akili,kwa mfano kushindwa kuwa makini anapoendesha gari ;hii inakuwa mikono yake haina nguvu za kufanya kazi kwa ufasaha kabisa .pia anapokuwa anaendesha gari .
2.hudidimiza hali ya uzazi ,kwa kuathiri homoni za kiume na kike; tunaona kuwa bangi ina huathiri sehemu kubwa ya mwanadamu .kwa hiyo inatubidi tuwe makini sana au tuache kuvuta bangi .
3.huathiri siku za hedhi kwa mwanamke.hii inatokana na mwanamke kuwa na athari hizo ambapo inatokea kuvuta bangi.hii tunaona matatizo mengi mfano,mwanamke anaweza kuvuta bangi ambapo akiwa kwenye hedhi uweza kupata matatizo mfano mimba wakati bangi imemuharibia siku zake.
4.mara nyingine husababisha kuzaliwa watoto walemavu.hii inatokana na kuwa bangi inapelekea kuharibu kizazi cha mwanamke .ambapo mama anajifungua mtoto mwenye matatizo .mfano wa matatizo ni kutokuwa na mkono.pia kicha kuwa kikubwa .,pamoja kutosikia vizuri kwa mtoto.
5.husababisha magonjwa mbalimbali ya akili.mfano mtoto kutokujua kuongea, kusikia,na kutotembea ni baadhi ya magonjwa ya akili.
6.huathiri maendeleo ya mtu binafsi na hata familia na taifa kwa ujumla pia Adi kifo .hii itapeleka kupoteza nguvu kazi ya taifa la tanzania.
4.MADAWA YA USINGIZI:
Tunashauri kuwa dawa za usingizi zitumike kama kitulizo kwa wagonjwa walio na dalili za wasiwasi mkubwa.hali yao inapotokana na dalili mbalimbali za ugonjwa zinazotokana na hali ya mashaka , wasiwasi na kukosa usingizi.
Bahadhi ya dawa hizi valiumu na genobabitoni ambazo hupatikana katika vidonge .matumizi ya muda mrefu ya dawa za usingizi yanaweza kusababisha athari za kisaikolojia na kimwili.
Matumizi ya kiwango kikubwa sana cha dawa za usingizi humfanya mtu apoteze fahamu na kusababisha kifo .kwa mfano kiasi cha vidonge 12 hadi 15 vya genobabitoni vinaweza kumuua mtu hasa vikitumiwa pamoja na pombe.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Jifunze Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2004
Sponsored links
👉1 Simulizi za Hadithi Audio
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 kitabu cha Simulizi
👉6 Kitabu cha Afya
TAHADHARI KWENYE VYAKULA
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
Kujiepusha na Vishawishi vya Zinaa
Kujiepusha na Vishawishi vya ZinaaKatika macho ya sheria kitendo cha zinaa kinahesabiwa pale wanapokutana kimwili mwanamume na mwanamke nje ya ndoa. Soma Zaidi...
YANAYOATHIRI AFYA KUTOKANA NA VIZAZI, FAMILIA NA KURITHI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
Dua Sehemu ya 01
Zijue fadhila za kuomba dua, tambua umuhimu na mahimizo juu ya kuomba dua? Soma Zaidi...
Namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji, ni mbinu mbalimbali ambazo utumika ili kujaribu kuepuka Dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji. Soma Zaidi...
Dondoo 100 za Afya
Soma Zaidi...
Dondoo za afya 41-60
Somo Hili linakwenda kukuletea dondoo mbalimbali za afya Soma Zaidi...
MAWAKALA WA KUSABABISHA NA KUSAMBAZA MARADHI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...
Namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji
Posti hii inahusu zaidi namna ya kuzuia dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji, ni mbinu mbalimbali ambazo utumika ili kujaribu kuepuka Dalili za hatari kwa aliyefanyiwa upasuaji. Soma Zaidi...
dondoo 100 za Afya
Basi tambua haya;- 61. Soma Zaidi...
Kitabu cha Afya 02
Kama tulivyosema hapo juu kuwa afya ni kuwa mzima kimwili na kiakili. Soma Zaidi...
utaratibu wa lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...