Nitakujuza dawa ya kutibu vidonda vya tumbo, na kutibu vidonda vya tumbo sugu
DAWA YA VIDONDA VYA TUMBO
Dawa za vidonda vya tumbo zinategemea aina za vidonda alivyo navyo, mahala vilipo na sababu za vidonda hivyo. Kitu cha kwanza kuangalia ni sababu gani zilizopelekea vidonda hivyo?. kisha baada ya kuijuwa sababu ndipo maibabu yatafuata. Kama tulivyokwisha jifunza kuwa sababu kuu za vidonda vya tumbo ni bakteria aina ya Hypylori. Hivyo kama sababu ni hii mgonjwa atapewa dawa ya kuwauwa hawa bakteria. Pia kama sabau ni asidi tumboni atapewa dawa za kupunguza uzalishwaji wa hizi asidi. Dawa za vidonda vya tumbo ni kama zifuatazo:-
1.Dawa kwa ajili ya kuuwa bakteria. Hapa mgonjwa atapewa dawa kama:-
A.Amoxicillin (amoxil)
B.Clarithromycin (Biaxin)
C.Metronidazole (flagyl)
D.Tinidazole (tindamax)
E.Tetracyline
F.Levolaxacin
2.Dawa za kuzuia uzalishwaji wa asidi mwilini (proton pump inhibitors (PPIs))
A.Omeprazole (Prilosec)
B.Lansoprazole (Prevacid)
C.Rabeprazole (Aciphex)
D.Esomeprazole (Nexium)
E.Panztoprazole (Protonix)
3.Dawa za kupunguza uzalishwaji wa asidi tumboni (Acid blockers (histamine (H-2))
A.Famoditine (Pepcid AC)
B.Cimetidine (Tagamet HB)
C.Nizatidine (Axid AR)
4.Dawa zinzzolinda ukuta wa utumbo na tumbo
A.Cytoprotective agents
B.Sucralfate (Carafate)
C.Misoprostol (Cytotec)
TIBA MBADALA ZA VIDONDA VYA TUMBO.
Wataalamu wa afya pia wanakubali uwepo wa tiba mbadala katika kutibi vidonda vya tumbo. Zipo nyingi sana, miongoni mwazo ni:-
A.Bamia
B.Kitunguu thaumu
C.Asali
Kwa nini vidonda haviponi hata baada ya kutumia dawa?
Hii hutokea endapo:-
A.Kama mgonjwa hakutumia dawa kwa kufuata masharti vyema
B.Haswa kuna baadhi ya bakteria wa vidonda vya tumbo wana usugu wa kufa na dawa
C.Kama unatumia tumbaku
D.Kama unatumia dawa za NSAIDs
Pia mara chache vidonda vya tumbo vinaweza kusababishwa na:-
A.Uzalishwaji wa asidi kupitiliza
B.Mashambulizi mengie yasiyo ya H.pylori
C.Saratani ya tumbo
D.Kuwa na maradhi mengine
Umeionaje Makala hii.. ?
Albenza (albendazole) hutumika kutibu magonjwa ya minyoo ya ndani ikiwa ni pamoja na maambukizi ya minyoo ya tegu. Albenza inafanya kazi kukomesha kuenea kwa maambukizo ya minyoo kwenye chanzo, na kukata chanzo chao cha nishati, na hivyo kuzuia kuenea k
Soma Zaidi...Ibuprofen ni mojawapo ya dawa zinazotumiwa sana duniani kote! Ili kupunguza maumivu na kuvimba, agiza Ibuprofen leo na upate afya bora! Ni kiungo amilifu katika dawa za jina kama vile Motrin na zaidi. Ibuprofen pia inaweza kuuzwa kama: Advil Motrin,
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa zinazofanya kazi ya kupunguza maumivu kwa kawaida dawa hizi ufanya kazi kwa kupitia kwenye mfumo wa fahamu.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa ya propranolol katika matibabu ya magonjwa ya moyo, dawa hii ipo kwenye kundi la beta blockers na ufanya Kazi mbalimbali hasa kwa wagonjwa wa moyo.
Soma Zaidi...Ukiwa mjamzito uwe makini sana katika kuchagua matumizi ya dawa. Vinginevyobinawwza kuwa hatari. Hapa nitakujuza dawa ambazo ni hatari kutumia kwa ujauzito wako.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi dawa za kisukari, kwa sababu ya kuwepo kwa ugonjwa wa kisukari vilevile kuna dawa zake ambazo utumika kurekebisha sukari kama imepanda au kushuka.
Soma Zaidi...Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu dawa za kutibu kiungulia
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kundi la diuretics,ni kundi mojawapo kati ya makundi ya dawa zinazosaidia katika matibabu ya magonjwa ya moyo.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi aina mojawapo ya dawa ya penicillin ambayo ufanya kazi kwa mda mrefu, dawa hii kwa kitaamu huiitwa procaine benzyl penicillin.
Soma Zaidi...