Fahamu kuhusu dawa ya Albendazole

Post hii inahusu zaidi dawa ya Albendazole ni mojawapo ya dawa ambazo usaidia kutibu minyoo, na pia imefanikiwa sana kadri ya watumiaji wa dawa hiyo.

Fahamu kuhusu dawa ya Albendazole .

1. Dawa ya Albendazole ni mojawapo ya dawa ambayo imechaguliwa kutibu minyoo aina ya ascrarisisi, hookworm, maambukizi yatokanayo na minyoo,strongyloidiasis,trichuria,anterobiasisi na trichostrongyloidiasi hayo ni majina ya kitaalamu yanayotumika kuitwa na minyoo ambayo utibiwa na dawa ya Albendazole,

 

2. Kwa kawaida dawa hizi uwekwa kwenye tumbo lililowazi  ili kama wadudu wapo waweze kuuawa vizuri bila kujificha kwenye chakula na pia ushauliwa kutumiwa wakati wa asubuhi kabla mtu hajala chakula chochote na kwa kawaida dawa hizo utafunwa na pia kumezwa bila maji na baadae mtu anaweza kula chakula.

 

3. Pia  dawa hii huwa na maudhui madogo madogo ambayo ujitokeza baada ya kutumia dawa na maudhui hayo yakizidi ni vizuri kumwona daktari au mtaalamu wa mambo ya afya, na maudhui hayo ni kama kiungulia,kuharisha, maumivu ya kichwa, kichefuchefu na kutapika, kizunguzungu kwa hiyo kwa watumiaji wa dawa za Albendazole baada ya kuona dalili kama hizo ni matokeo ya dawa.

 

4. Kwa kawaida dawa hizi hazitumiki kwa watu wote, wengine wanaweza kutumia ila akina Mama wenye mimba changa na wajawazito hawapaswi kutumia na watoto chini ya miaka miwili hawapaswi kutumia dawa hii kwa sababu ya matokeo yake kwao kama mimba kutoka kwa wanawake wenye mimba changa na watoto wadogo wako kwenye hatari ya kupata ugonjwa wa degedege.

 

5. Kwa hiyo katika kutumia dawa hiii ni vizuri kabisa kufuata utaratibu wa wataalamu wa afya sio kutumia kiholela kwa sababu madhara yake yanaweza kuwa makubwa zaidi ikiwa dawa hii inatumika visivyo kwa hiyo ni lazima kuwaona wataalamu wa afya kabla ya kutumia dawa hizi.



Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2022/12/15/Thursday - 10:50:58 pm     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1934


Download our Apps
👉1 Kitabu cha Afya     👉2 kitabu cha Simulizi     👉3 Kitau cha Fiqh     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-